Jando la bureee! Kwanini wanaume wengi wamebakia empty souls wapo ndoani kama makasha tu!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!

Huu ubuyu wa leo si wa babu Issa wa sheikh Kiponda. Nimeupata kimagumashi magumashi kama bakhati tuuuu! Ilianza siku kama siku zingine tu ofisini, kupiga sogaaa, soga na wewe. Ndo mdau kuuza cd ya kilichomkuta jana yake. Huyo mdau ana mchumba kabisaa keshalipa mahari basi tu mambo hayajakaa level angeshaoa kitamboo. Huyo mchumba yupo chuo bt ghetto kwa mshkaji anaachaga nguo, taulo, michupi na mivitu kibao. Sasa mshkaji tumuite H, anaona ubahili kukodi guest so kazi za nje kama shombe hayupo anazipiga humo humo ghetto kishkwambi tu. Anaficha nguo za shombe sandukuni chinii, anaweka zake juu baridaaa.

Juzi kachukua kazi ya Udsm ya nje, ikaenda ikapika fresh, akatumwa machungwa, huku nyuma ikamsachi ikatoa nguo zote za shombe chini sandukuni na kuzimwaga kitandani. Anarudi akakuta kishanukaa. Hakupaniki wala nini, anaongea kama kawaida bibie kavimba kama kobraaa anaetaka kupasuka. Wakala, baadae akajiwahi H kujimimina kwa ile kazi ya nje. Mi sijapenda ulivonisachi sio ustaarabu, na hizo nguo za x wangu, tumeachana aliziacha humu, nasubiri siku aje azitoe. Sikukwambia coz ni mambo personal na nishaachana nae kitamboo sema vitusiwezi kuvitupa. Blah blah blah blah! Kajimiminaaa hatariii. Mtoto kajaa wavuni na mechi katoa desipe all the evidence to convict, katoa mchezo na performance ya hatariiiii! Hahaaaa! Basi mi ndo nikawa namjaza upepo you the man! Usingepewa mchezo ningekuona lafa tu! Basi ikawa firauni kakutana na firauni, kijiwe kikageuka ufirauni untd!

Kumbe pembeni kuna baba la baba yuko 45 huko, ana mke na watoto kaweka phone masikioni tukajua haskii kumbe anafatilia kwa ukaribu huu ubuyu. Ndo kujisahau na kuchangia! Tobaaaaa! Eti kijana umecheza kama pele, jioni uje unywe na sisi pub flani? Makubwaaaaa! Kiutani utani H akawa kapata pass to the champions league. Nikasema silegei naunga trella.Nikadakia boss na mimi nije? Akakaza we bado kazurure na watoto wenzio, nikakomaa mi mkubwaa wewe, nikampa story moja ikamuacha mdomo wazi, akasema kumbe watoto wakubwa nyieee, mje mje mbadilishane mawazo na wakubwa wenzenu. Nikamwambia H hapa hamna kulegea, we are going to impress, tukiharibu boss atatuharibia cv humu ndani kwenye rank za ufirauni.

Usiku tukaenda tukakuta watu wazima mastriker wa old times. Professional! Hawakosei wala hawabahatishi, ndo nikasikia sasa hili jandoo la bureee! Nikameza neno kwa neno, kiukweli ile elimu dunia mimi binafsi imenipa mwanga na kuniongezea ranks. Boys 2 men mmoja akawa anasemaje kuna mtu kahama kwa mkewe, alihamia kwa kimada, kimada kikamtenda, sahivi anaishi mwenyewe na 48, watoto wake hajawazoeaa, hana furaha, hana amani, yupo tu kama kasha tupu. Hela anayo furaha hana, amani hana, mpaka sukari imempata. Ndo kubwa la maadui likatoa somo, ukiwa umri wetu huu wa ubachela ukitaka kupata vyote, uendeleze uanachama wa CHAWABATA (Chama cha wala bata Tanzania) ili ubakie kijana wa roho daima na uwe mume/mke bora at the same time mzazi boraaa na uzeeke as a winner katoa pointers muhimu.

1.Mke si rafiki yako mke ni mkee! Ukianza urafiki na mke atataka kukukali kichwani, kupanga sheria, kuingilia utawala wako. Urafiki wa mke na mume mwishowe ni kuwa mtumbwa au bwelegeje wa mkeo. Yaani wanawake walivo ukimuachia mwanya kidogo tu umeumia. Ukimpa lift hakawii kupiga honi. Unamformat tu katika maadili ya kuwa mke, na heshima itawale mda woteeee. Dai heshima yako kwa gharama yoyote. Mpende mkeo sawa ila heshima muhimu na definition of positions muhimu. Jaribio lolote la kijitwalia mamlaka lizime kama switch.

2. Fanya wajibu wako kwa gharama yoyote. HQni HQ pape heshima yake maana ndo panakudefibe wewe mwanaume ni mtu wa aina gani. Wape mkeo na wanao the best you can give. Mkeo lazima umle hata kama umemkinai, umemchoka, vyovyote vile dozi ibakie pale pale , ukimpa kazi kazi kweliiii as if she is the only one that matters, katika performance you give all you have got. Despite age, despite anything. Problema zingine kama mwanaume unadeal nazo binafsi tu, unakomaa kuzitatua kimya kimyaaa. Ndani huoneshi udhaifu despite umri kwenda wala nini. Hata ukichachua nje unambakishia maza dozi yake pale pale.

Keep your wife busy na mu encourage to find her passion in life, dreams, ambitions and persue it. Kama hana create some for her. Ujue wanawake zile years za uzazi na ulezi, tuna sacrifise future kujenga familia. Anasahau kujifikiria yeye kabisaaaa! Kila kitu akilini kinakuwa mume na watoto. Sasa kwa mume ile kwako ni danger ndo mnaanza kufarakana mana anaona yeye kapoteza vingi wakati wewe you got everything you ever wanted in life. Ndo visirani vinaanza na kuchokana. Sasa hutakiwi kuruhu hii, unamtafutia hobby au ambition ambayo itaondoa focus yake kwako, kuhamia kwenye hio hobby au ambition. Kama hajasoma unamuhimiza arudi shule, shule itamkeep busy muda wa kununa hana. Kama ana kazi unamuongezea biashara juu. Au umfungulia mradi just to keep her focused and have a purpose in life other than kuwa mkeo. Siku zitaenda fasta hatarii mpaka utafurahi.

Kufanya maamuzi magumu ya kutomtenganisha mkeo na ubinadamu wake. Kutambua tu yule kama binadamu wengine anaweza kukosea na kufanya blander za hatari kama wanawake wengine. Na kujiwekea tu moyoni kuwa hata ikitokea hivo ni mambo ya kawaida tu ya kibinadamu na utajitahidi kuelewa situation na kutafuta suluhu bora ukikumbuka miaka lukuki aliotenda mema ikuongoze na sio hilo kosa moja. Yani unakaa unaweka uwezekano yes mkeo kama binadamu wengine anaweza kukoseaa vikubwa yet still hata ikitokea upate ujasiri wa kumchukulia kama life partner. U Nelson Mandela sio issue. Unasamehe dunia nzima kasoro mkeo, mama wa watoto wako! Loooh! Haitakiwi. Boys 2 men wanakwambia imetokea sanaa iliwauma kimtindo but wakakomaa na cimitment.

Habari ndo hiyooo!
 
lara1

Naona umepata bando ehhh 😁😁😁😁😁
Miss u sana
 
Last edited by a moderator:
Duuu..... lara1 again.
karibu sana mkuu, ila samahani,
hivi ulienda kugombea viti maalumu..?
maana watu wakienda kutangaza nia wanapotea
sana hapa jamvini kama wewe ulivyofanya...
 
Last edited by a moderator:
lara1

Naona umepata bando ehhh 
Miss u sana
Hahaaaaa! Nilitekwa na hawa Boys 2 Men nimewakimbia ndo kidogo napata nguvu za kuandika! Aaaaaaah! Kule si kula bata ni kuwa mtumwa wa bata!
 
lara 1 katika Ubora wake nasubiri huo ubuyu kwa hamu zote...
 
Last edited by a moderator:
Fundi wangu umewasili, Hii jando noma Lara1, If u wea a man, huyo WIFE Angekula Treatment moja matata sana, Ntakupa dem wangu umpe kichen party moja matata,
 
Nakukubali sana lara moko yaani ww ni mtt fln hv amazing wa ushuani lkn unaji mix sana kitaa
 
Nzr Sana, mkeo lazima umjali, darasa moja matata kwetu wanaume.
 
Back
Top Bottom