Jana nimeona BBC Swahili usiku wakizidi kuudhalilisha upinzani Afrika

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Kikeke alimuuliza swali repota wake kutoka Dar kuwa huyo rais wa Zambia je unadhani atashirikiana na viongozi wengine wa vyama tawala ambavyo ni vya ukombozi akiwa na maana vyama kama CCM, ZANU PF na ANC.

Jamaa wa BBC akajibu kuwa ni swali zuri sana hila siwezi lijibu mpaka tuje tumuone mwenyewe kwani hawa viongozi wa kiafrika wanabadirika badilikaga sana, na kutolea mfano Rais wa Malawi kuwa juzi katika ziara yake Uingereza alibeba familia yake yote wakiwemo wakwe,wajomba, babawadogo, mashangazi na mashemeji zake kwenda ziara Uingereza na hata kuwaacha wataalamu kama katibu wa wizara ya mambo ya nje ambaye si ndugu.

Hii vile vile inafanana na makamu wa kwanza wa Rais wa Zimbabwe ni marehemu Tshangilai yeye alivyoteuliwa katika ule muhafaka na Mugabe hakuwai kuonekana wala kusikika ama kutetea au kuchangia tu yale aliyokuwa akisema atayafanya kutokana na ugumu wa maisha ya Zimbabwe. Badala yake watu walimwona tu akisababisha foleni kubwa katika miji ya Bulawayo na Harale kwa misafara yake ya magari wazimbabwe walibaki midomo wazi.

Na tabia kamahizi zimewai pia kuonekana kwa Mwaikibaki wa Kenya, Chiluba hata yule aliyemtoa Mzee banda Malawi na wengine wengi.

Vipi mna chochote cha kuchangia kuhusu upinzani wa Afrika?
 
Amesahau na wa hapa kwetu ambao badala ya kusimamia sera zao, ilani zao na kauli zao. Wao walichofanya au wanachofanya ni kusimamia tu masilahi ya matumbo yao. Wapinzani wa Afrika Mungu anazidi kuwaumbua mmoja baada ya mungine.

images (7).jpeg

2878995_images_9.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: tyc
CDM walijiona wanapendwa sana na Mabeberu kumbe walikuwa wanatumika tu kama condoms kutetea maslahi ya mabeberu baada ya JPM kukata mirija yao, saivi Samia ameshawahakikishia mabeberu maslahi yao kulindwa CDM wasitegemee tena support yoyote ya maana.
 
Tanzania kulikuwa na mtu mmoja toka chama cha ukombozi (chama Cha Magaidi --ccm) alisukumiwa ikulu akajiita jiwe. Huyu aliteua
-mpwa wake kuwa pay master general
..mpwa wake kuwa katibu uvccm
..nafasi zote nyeti aliwapatia watu wa kabila lake.
 
Mbona hujasema chochote kuhusu Samia alivyobeba makada wenzake wa ccm kwemda nao huko Zambia kwenye uapisho wa HH?
. Hajui kuwa Samia alienda Zambia na genge lake la Intaramwe akaacha wataalamu hao anao wazungumzia. Samia atakuwa katoka upinzani kwa akili hizi za ki uvivu ccm.
Makaburi alisema eti kuna watu wanafikili kwa kutumia Makalio huko Lumumba naanza kuelewa.
 
Kimsingi naunga mkono uchambuzi huu. Wapinzani walioshinda chaguzi wameshindwa ku deliver kama walivowaaminisha watu wao. Mpaka sasa hakuna maendeleo makbwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yaliyohubiriwa.
Aibu sana kwa kweli
 
Huku kwetu jamaa amenaswa akijihusisha na ugaidi. Eti naye anajidai ni kiongozi wa upinzani kumbe ni muhuni tu.
 
Kikeke naye ni wa kufanyiwa rejea? Katika ile interview yake na Rais Samia, aliweka weledi pembeni, akataka awafurahishe serikali ili akistaafu BBC afikie pazuri.
Ni kweli kuna mifano kadhaa ya wapinzani ambao hawakufanya vizuri walipoingia madarakani.

Lakini pia ni kweli kwamba sehemu kubwa ya vyama vilivyopigania Uhuru, vimeboronga vikiwa madarakani.

Na kwa upande mungine, watu kama Mandela na Mbeki walifanya vizuri. Sina hakika na Ghana. Kwa hiyo tusiwahukumu wapinzani wooote kwamba eti wataboronga wakipata fursa ya kuongoza. Hiyo inaweza kuwa kisingizio kwa vyama kama ccm kubaki madarakanitu hata kama waneishiwa mbinu za kuleta maendeleo. Kila uchao uchumi mbovu.

Cha msingi ni kujenga taasisi imara. Vyombo huru vyavhabari, Bunge huru, Mahakama huru, Tume huru ya uchaguzi. Hapo serikali yoyote ikiingia madarakani, itabanwa mbavu iwajibike. Rais unaenda na mashemeji ulaya safari ya kikazi? Mbona media itakushughulikia, mitandao ya jamii nfio usiseme. Bungeni hoja zitajengwa, na waziri mkuu atalazimika kujibu bungeni kuhusu safari hizo na waka spika hatomkingia kifua. Waziri mkuu anaweza kupigwa chini na Rais kulazimishwa kuunda upya serikali. Na akizidi kuleta ujinga, ataondolewa madarakani na Bunge. Wapinzani na wabunge wa chama tawala wataungana. Hamna anayetaka ujinga.

Hayo yote yanawezekana. Tuanze na Katiba Mpya
 
. Hajui kuwa Samia alienda Zambia na genge lake la Intaramwe akaacha wataalamu hao anao wazungumzia. Samia atakuwa katoka upinzani kwa akili hizi za ki uvivu ccm.
Makaburi alisema eti kuna watu wanafikili kwa kutumia Makalio huko Lumumba naanza kuelewa.
Da kijana kuwa na akili basi hata kidogo, kwa hii mada kuzungumzia CCM au chama tawala si mada, CCM imekaa sana madarakani tumeichoka.
Tunachotaka kuona hapa ni tofauti kati ya hiyo CCM na Chadema au wapinzani sasa kama wote wa
Kimsingi naunga mkono uchambuzi huu. Wapinzani walioshinda chaguzi wameshindwa ku deliver kama walivowaaminisha watu wao. Mpaka sasa hakuna maendeleo makbwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yaliyohubiriwa.
Aibu sana kwa kweli
Nipe 10
ko sawa kuna haja gani ya kuwapa wapinzani nchi? sijui unaelewa au wewe uko kwenye mipasho, jadili na akilizako pia.
Yaani hapa ni kuwa vyama tawala ni wahuni lakini wapinzani ambao tayari wamechukua nchi na ambao bado wanataka kuchukua nchi nao wanatuonyesha uhuni wa hari ya juu mpaka inashangaza.
 
Da kijana kuwa na akili basi hata kidogo, kwa hii mada kuzungumzia CCM au chama tawala si mada, CCM imekaa sana madarakani tumeichoka.
Tunachotaka kuona hapa ni tofauti kati ya hiyo CCM na Chadema au wapinzani sasa kama wote wa

Nipe 10
ko sawa kuna haja gani ya kuwapa wapinzani nchi? sijui unaelewa au wewe uko kwenye mipasho, jadili na akilizako pia.
Yaani hapa ni kuwa vyama tawala ni wahuni lakini wapinzani ambao tayari wamechukua nchi na ambao bado wanataka kuchukua nchi nao wanatuonyesha uhuni wa hari ya juu mpaka inashangaza.
Sorry, yako inaishia nipe 10 mwanagu.
nimetuma vibaya hiyo nyingine.
 
Back
Top Bottom