Jana mheshimiwa rais kanilet down vibaya sana

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Huku nikiwa nahangaika kupinga hoja ya kumtambua mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama mtu dhaifu siku hiyo hiyo ya jana, nikiwa naangalia Taarifa ya Habari TBC1 ikatangazwa kwamba Mheshimiwa Rais amewaahidi viongozi wa chama cha Basket Ball nchini kwamba akienda marekani atawaombea kwa uongozi wa chama cha mpira wa kikapu Marekani ili kiweze kuwapa msaada.

Shit! nikajiuliza inamaana huyu mzee kumbe ni kweli akienda huko nje anaenda kukutana na very low profiled institutions kulinganisha na nafasi yake, kama ni hivyo barozi wetu huko marekani anafanya kazi gani, waziri wa michezo anafanya kazi kama ni kweli wanasiasa au viongozi wa serikali wanahitajika kudevelop relations kati ya vyama hivi viwili vya michezo, au hata ao akina mziya na fares kazi zao ni nini?

Na nikajiuliza swali la ziada kwamba, inamaana mheshimiwa rais bado amebakiwa na uwezo wa kupanga safari ya kwenda marekani ghafla namna hiyo katikati ya kipindi kigumu kwa serikali yake kuitetea bajeti yake bungeni?

Katika hili mheshimiwa rais amenisononesha sana,
 
Rais wa mambo ya marekani na mataifa ya ughaibuni Bwana Kikwete ndiye kasema hayo? ina maana yeye kwenda Marekani kwa mwaka ni sawa na kwenda chumbani kwake tu.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Ninaamini kabisa mataifa ya nje pamoja na kujifanya wanatusifia huwa wanatudharau sana. Madini yote tuliyonayo tutashindwa kweli kuhudumia hivi vilabu vyetu vya michezo bila kutegemea misaada kutoka nje?
Narudia tena JK na serikali yake ni dhaifuu hadi kufikiri.
 
Huku nikiwa nahangaika kupinga hoja ya kumtambua mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama mtu dhaifu siku hiyo hiyo ya jana, nikiwa naangalia Taarifa ya Habari TBC1 ikatangazwa kwamba Mheshimiwa Rais amewaahidi viongozi wa chama cha Basket Ball nchini kwamba akienda marekani atawaombea kwa uongozi wa chama cha mpira wa kikapu Marekani ili kiweze kuwapa msaada.

Shit! nikajiuliza inamaana huyu mzee kumbe ni kweli akienda huko nje anaenda kukutana na very low profiled institutions kulinganisha na nafasi yake, kama ni hivyo barozi wetu huko marekani anafanya kazi gani, waziri wa michezo anafanya kazi kama ni kweli wanasiasa au viongozi wa serikali wanahitajika kudevelop relations kati ya vyama hivi viwili vya michezo, au hata ao akina mziya na fares kazi zao ni nini?

Na nikajiuliza swali la ziada kwamba, inamaana mheshimiwa rais bado amebakiwa na uwezo wa kupanga safari ya kwenda marekani ghafla namna hiyo katikati ya kipindi kigumu kwa serikali yake kuitetea bajeti yake bungeni?

Katika hili mheshimiwa rais amenisononesha sana,

Wewe mwenye dhaifu kweli hata neno balozi linakushinda kuandika?
 
haya ndo mambo ambayo ndugai anatakiwa ayajue na kutambua kuwa JK ni dhaifu
 
Sangarara https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...li-yangu-bungeni-post4081317.html#post4081317

Sio Uko Mkuu.
Hemu nieleze toka mwaka 2007, ni wakati gani CHADEMA imewahi kutulia na kuwapa nafasi watanzania japo kusikiliza Rais ama serikali inahoja gani? every day wako mtaani, mara operation sangara, mara mapinduzi ya pili, mara list of shame nchi nzima wanazunguka bila kukoma.

Hii imesababisha watendaji wa serikali na Rais Mwenyewe kuwa kama wamepigwa ganzi, sababu wakitaka kushughulikia swala la Richmond DR SLAA anaibuka na IPTL, wakianza kushughulikia mkakati wa kilimo kwanza, ghafla anaanzisha hoja za meremeta, recently wameanza kuzungumzia mambo ya uchaguzi wa mwaka 2015, haya yote yanasababisha serikali kushindwa kuelewa ifanye nini hawa watu watulie, haya kuna hili la katiba mpya, wamesababisha out of everybody's plans Taifa limejikuta kwenye mchakato wa kuandaa katiba mpya, sio Rais, chama chake wala watendaji wa serikali walikuwa wamejiandaa na hii kitu this soon, matokeo yake serikali inashindwa kuliandalia budget Mnyika anamuita Rais Dhaifu. Nani wa kulaumiwa

Sangarara https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...li-yangu-bungeni-post4081317.html#post4081317

Kwa hiyo CHADEMA ikiingia madarakani hao watumishi wataresign wote, au wataacha huo ushenzi ghafla? Ni kweli ilihitajika kumtaja Rais kwenye list of shame ili kuwadhibiti watumishi hawa? lets seat down and think reasonably, unajua ni damage kiasi gani ilifanyika kichwani mwa kikwete pale mwembe chai? well ni kazi ya chama cha upinzani, lakini this time imetucost sana.sababu we have reduced our own president to nothing, then we are abusing our own creation.

walichokifanya CHADEMA na wanachoendelea kukifanya ni sawa sawa kabisa na kumkata mtoto mdogo mikono sababu kaiba mboga.

Sangarara https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...li-yangu-bungeni-post4081317.html#post4081317

Ndio maana mara zote huwa nasema kwamba Sheria ya vyama vya siasa ingeboreshwa zaidi ili kumfanya msajiri wa vyama vya siasa awe na nguvu ya kuregulate political environment.

Wanachokifanya CHADEMA sasa ni destruction ya mfumo mzima wa utawala chini ya CCM, Wao wanafurahi sababu wanagain influence zaidi, lakini wananchi tunataabika sana na madhara wanayokisababishia chama cha mapinduzi na serikali yake.

Jana ulikuwa busy kumtetea ama umesahau!!!
 
haya ndo mambo ambayo ndugai anatakiwa ayajue na kutambua kuwa jk ni dhaifu

ndugai hajasema kuwa rais wa tanzania si dhaifu. Na sidhani kama hajui kuwa rais wa tanzania ni dhaifu. Nilichokielewa mimi ni kwamba ndugai pamoja na magamba wenzie hawakubaliani na mnyika kutoa matamshi yale bungeni. Mnyika angetoa kauli ile mahali pengine popote pale huenda hakuna ambae angempinga
 
Ndoto za mwanafunzi mcheza mpira wa kikapu wa sekondari hazitofautiani kabisa na rais wake.
 
Hivi huko Marekani kuna nini maana haiwezi kupita wiki mbili bila rais Kikwete kwenda Marekani mbaya zaidi anaenda kuomba huku nchini ameyapa msamaha wa kodi makampuni ya madini, simu na makampuni mengine makubwa ya kibepari.

Ama kweli nimeamini kuwa Kikwete ni dhaifu kuliko marais wote waliopata kuingoza nchi hii tangia tupate uhuru.
 
Back
Top Bottom