Jana kombani na werema walistahili kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jana kombani na werema walistahili kujiuzulu

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Najijua, Apr 6, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jana kwa mara ya kwanza serikali iliwasilisha rasimu ya muswada wa katiba mpya bungeni, kwa mshangao mkubwa viongozi waliopinga na kusema serikali haina pesa ya katiba mpya ndio aliyesimama kuwasilisha!kwa mtazamo wangu jana ile ile Kombani alistahili kujiuzulu kwa kuwa yeye alishapinga hilo mwanzoni, je sasa serikali imepata wapi pesa?anasimamiaje kazi ambayo aliyoipinga hapo awali?uwajibikaji upo wapi hapo?

  Mwingine ambaye alistahili jana kujiuzulu kiungwana kabisa ni Jaji F.Werema, mwanasheria mkuu wa serikali, aliyedai haoni shida ya katiba ya sasa na kuishauri serikali kufanyia marekebisho tu sehemu zinazodaiwa zina kasoro, je leo hii anaisadiaaje serikali kwenye katiba mpya wakati hii ya kwanza yeye haoni kama inashida?si atarudisha yale yale tunayo yasemea? ndio maana ameshirki kuweka vipengele vitano ambavyo havitakiwi kujadilika katika katiba mpya navyo ni
  1. Madaraka ya Raisi
  2. Bunge
  3. Tume ya Uchaguzi
  4. Mahakama
  5. Usalama wa taifa

  kama tunaambiwa tunaandika katiba mpya ila kuna mambo hayajadiliki kwanini wanaiita katiba mpya?

  Hivi Kombani na Werema dhamira haziwasuti wakati tupo katika mchakato huu?kwa roho safi wajiuzulu tu jamani,

  Au wanataka tuuingie myaani kupinga uwepo wao katika mchakato huu, kwa kuwa hatuna imani nao tayari
   
 2. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hakuna katiba mpya tanzania na hatutaipata miaka ya karibuni....tunaongeza viraka kwenye katiba ya zamani.
   
 3. m

  msambaru JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Huu ni ukarabati tu jamani katiba mpya huwa haziji kama zali la mentali, hawa majuha wamejipanga kukaba maeneo yanayowaweka pazuri na itapita kama kawaida yao.
   
 4. A

  Awo JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Bunch of nincompoop!
   
Loading...