mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
Wanajf, salaam!!!
Napenda kuungana na watu wote tulioipokea taarifa ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma tarehe 27/4/2017. Hii inaonesha jinsi gani serikali inajivunia kutoa huduma kwa wananchi.
Pamoja na sifa hizo nachukulia taarifa ya uhakiki wa vyeti hivyo kama imejaa ubaguzi, uonevu na unyanyapaa kwa baadhi ya watanzania, ingawa kimsingi walikosea na KUVUNJA sheria za nchi kwa kufoji, kuiba au kula njama wakati wakitafuta vyeti hivyo.
Ubaguzi, uonevu na unyanyapaa ninaozungumza umetokana na mambo yafuatayo:-
1. Kutofanya uhakiki kwa wakuu wa wilaya, mikoa na Wabunge ambao nao ni watumishi hakuingii akilini mwangu (Mhe. Dkt John Pombe Magufuli jana watu wengi - CCM, CDM, NCCR, CUF, ACT na wasio kuwa na vyama walielekeza macho na masikio nchini Kolomije) - hapa ndiyo ilikuwa muhimili mkubwa wa Uhakiki na matokeo yake. Umaarufu wa rais ungeongezeka kama angetoa tamko la kuagiza sehemu hizo zihakikiwe.
2. Kufanya kazi bila ubia - kazi ya rais haipaswi kuonekana as if anapotekeleza ana ubia na mtu - kitendo cha kutolishughulikia sakata la kughushi vyeti kuhusu Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda linatia giza na kutafsiriwa kwa hisia tofauti tofauti ikiwemo kundi moja la watu kutaka kulifananisha na ukabila, uchama nk nk - hali si hatari tu bali linavunja sura ya taasisi ya Ikulu.
Maoni/Ushauri:-
1. Mhe. Dkt JPM aangalie upya jinsi ya kushughulikia sakata hilo - pamoja na kuwa anajinasibu kuchukia siasa na wanasiasa lakini afahamu kuwa nafasi yake ni ya kisiasa. Chama cha MAPINDUZI tunahitaji tena kupata ridhaa ya wananchi mwaka 2020 kupitia chama chetu.
2. Matamko mengine si lazima ayatoe kwa kuwa humchonganisha kwa wananchi - mfano mzuri ni kusema kuwa yeye a nachukia wanasiasa. Hii si nzuri kabisa.
Hongera zake iwapo wafanyakazi wataongezewa mishahara wakati wakulima bajeti ya pembejeo ikiwa ndogo. Maybe next budget wakulima nao wataneemeka kwa mkazo wake.
Msakila KABENDE