Mzee wa Usafi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 644
- 292
Kuna kizazi mimi nimekipachika jina kwa kiingereza kinaitwa " Lost Generation" hawa ni vijana walio maliza vyuo kati ya 2010 na sasa. Mara baada ya mtikisiko wa kiuchumi wa 2008 na 2009,hakuna ajira za maana zimepatikana hapa Tanzania kutoka serikalini au sekta binafsi....hivyo kuna vijana wengi sana mtaani ambao bado wana lelewa kwa ndugu na jamaa zao hata baada ya kupata shahada zao. Hiki kizazi ndo kina shabikia tumbua tumbua ya vyeti wakidhani wao wataneemeka kwa kupata nafasi hizo.....kimantiki serikali haina uwezo wa kuajiri zaidi ya wafanyakazi 50000 kwa mara moja. Sekta binafsi ambayo inatarajiwa kutoa angalau nafuu nayo iko katika hali mbaya sana kwa sasa....hivyo wale wanao shangilia ndugu zao wanapokosa ajira wasishangae kuendelea kudunda mitaani. Ahadi za wanasiasa sisi wakubwa zenu tuna zifahamu mno...wakati wazee wetu wakipitiwa na Fyagio La Chuma....enzi za Mwinyi wengi ya hao vijana walikuwa bado wana jisaidia kinyesi cha njano.....Tafuteni mbinu mbadala
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app