Jamuhuri ya Afrika ya Kusini (SADC Super Power) walitusaidia wakati wa ajali ya MV Bukoba. Mbona tumewasahau katika janga hili la Mlima Kilimanjaro?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
9,836
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania eti;

asasaaaaaaaaaaa.jpg

Sijataka kuongelea kuhusu Kenya kwa maana wadau wataanza kuhusisha hili suala na mambo ya utalii kwamba watalii wakiona moto Mount Kilimanjaro basi watakimbilia nchi jirani.

AJALI YA MV BUKOBA KWA UFUPI KIDOGO
=====

MVBUKOBAA.jpg

According to a report issued by the government’s probe commission, over 700 people perished while 114 others were lucky to survive the accident. The government was overwhelmed by the crisis and sought assistance from South Africa for concerted efforts to remove the bodies of those trapped in the sunken ship.

TANZANIA - SOUTH AFRICA RELATIONS IN A NUTSHELL
=====
ASASASDDDDDDDDDD.jpg

Picha hapo juu ni Mh. Rais Dk. J.P Magufuli akiwa na Waziri wa mashauri ya kigeni Prof. Palamagamba Kabudi wakikabidhi vitabu vya kiswahili kwa Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kusini Mh. Ramaphosa katika harakati ya kuhakikisha lugha hii tamu inakuwa na kuenea kwa haraka zaidi nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika ya Mashariki.

AJALI YA MOTO MLIMA KILIMANJARO
=====

download.jpg

Wazima moto nchini Tanzania wanapambana kujaribu kuudhibiti moto unaouteketeza mlima mrefu zaidi barani Afrika, mlima Kilimanjaro. Kulingana na shirika la mbuga za kitaifa Tanzania TANAPA moto huo ulianza Jumapili.

Hapo Jumapili Shirika hilo la mbuga za kitaifa lilichapisha picha ambayo haionekani vizuri kwenye mtandao wa Twitter ikisema ni moto unaouteketeza mlima Kilimanjaro.
=====

Mbona safari hii tumewasahau ndugu zetu wa South Africa (in terms of asking for logistical support) katika janga hili la mlima Kilimanjaro?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Uzi wa mwaka jana huu>>> Ajali ya moto msitu wa Amazon: Wataalam Wizara ya Maliasili, Jeshi la zimamoto wamekaa kimya tu mpaka sasa. Mahusiano na umma imekaa vipi hapa?
 
chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
7,636
2,000
Naona hii misitu duniani inawaka moto tu. Na hapo kilimani baridi yote iliokuwepo sielewi. Isijekuwa chini ya ardhi kunafukuta! Huu mlima uko monitored vizuri lakini au kuna haja ya kuwaleta wanajiolojia kuja kuutizama tena? Mana mara siku zake zinakaribia.

Majirani zetu wanachekelea mlima kuwaka moto, si rahisi kusema kusaidia labda Tour operators wao waende serikalini kwao wawaambie watoe msaada.
 
kasulavenance

JF-Expert Member
Jan 23, 2020
731
1,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania eti;

Jamuhuri ya Afrika ya Kusini (SADC Super Power) walitusaidia wakati wa ajali ya MV Bukoba. Mbona tumewasahau katika janga hili la mlima Kilimanjaro?

Sijataka kuongelea kuhusu Kenya kwa maana wadau wataanza kuhusisha hili suala na mambo ya utalii kwamba watalii wakiona moto Mount Kilimanjaro basi watakimbilia nchi jirani.

AJALI YA MV BUKOBA KWA UFUPI KIDOGO
=====

View attachment 1601514

According to a report issued by the government’s probe commission, over 700 people perished while 114 others were lucky to survive the accident. The government was overwhelmed by the crisis and sought assistance from South Africa for concerted efforts to remove the bodies of those trapped in the sunken ship.

TANZANIA - SOUTH AFRICA RELATIONS IN A NUTSHELL
=====
View attachment 1601512

Picha hapo juu ni Mh. Rais Dk. J.P Magufuli akiwa na Waziri wa mashauri ya kigeni Prof. Palamagamba Kabudi wakikabidhi vitabu vya kiswahili kwa Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kusini Mh. Ramaphosa katika harakati ya kuhakikisha lugha hii tamu inakuwa na kuenea kwa haraka zaidi nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika ya Mashariki.

AJALI YA MOTO MLIMA KILIMANJARO
=====

View attachment 1601529

Wazima moto nchini Tanzania wanapambana kujaribu kuudhibiti moto unaouteketeza mlima mrefu zaidi barani Afrika, mlima Kilimanjaro. Kulingana na shirika la mbuga za kitaifa Tanzania TANAPA moto huo ulianza Jumapili.

Hapo Jumapili Shirika hilo la mbuga za kitaifa lilichapisha picha ambayo haionekani vizuri kwenye mtandao wa Twitter ikisema ni moto unaouteketeza mlima Kilimanjaro.

Mbona tumewasahau ndugu zetu wa South Africa (in terms of asking for logistical support) katika janga hili la mlima Kilimanjaro?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Uzi wa mwaka jana huu>>> Ajali ya moto msitu wa Amazon: Wataalam Wizara ya Maliasili, Jeshi la zimamoto wamekaa kimya tu mpaka sasa. Mahusiano na umma imekaa vipi hapa?
TTanzania sasa ni Nchi kubwa ni aibu hata kuzima moto mpaka tutafuta msaada.Wanajeshi wetu kazi yao ni nini wakati hatuna vita.Hapa ndio wangesaidia
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
9,836
2,000
Wanajeshi wetu kazi yao ni nini wakati hatuna vita.Hapa ndio wangesaidia
Jeshi siku zote lipo vitani mkuu. Kitendo cha Tanzania kuwa katika hali ya utulivu na amani licha ya kuzungukwa na nchi za jirani zilizojaa makundi ya waasi pamoja na political instabilitites, hiyo ni kazi nzuri sana ya TPDF/JWTZ pamoja na taasisi zingine...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom