JamiiForums yapata tuzo ya Uhamasishaji wa Uhuru wa Maoni/Taarifa nchini kutoka UTPC

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Umoja wa Klabu za Wanahabari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs) umetoa tuzo ya mwaka 2019 ya Daudi Mwangosi kwa taasisi ya JamiiForums leo hii katika ukumbi wa Raha Leo pale Zanzibar.

Tuzo hii imepewa jina la mwanahabari nguli aliyefariki akiwa katika harakati za kutimiza majukumu yake ya kuhabarisha umma, Marehemu Daudi Mwangosi.

Tuzo hii hutolewa kila mwaka kwa mwanahabari au taasisi ambayo imetimiza vigezo vya juu vya utoaji habari na kuchochea uhuru wa kutoa na kupokea taarifa.

Mwaka huu, tuzo hii imetolewa visiwani Zanzibar ambapo Mkurugenzi Mkuu, Maxence Melo ameipokea kwa niaba ya Watendaji wote wa taasisi.

JamiiForums inapenda kutoa shukrani za dhati kwa UTPC kwa kuwapa heshima hii na inaahidi kuendelea kupigania uhuru wa kujieleza, haki ya kupata habari, usiri wa taarifa binafsi na ulinzi wa kidijitali.

Kwa nafasi ya pekee, tunathamini na kutambua mchango wa watumiaji na wadau wa JamiiForums katika kupata tuzo hii.

Kwa niaba ya JamiiForums Mkurugenzi Mkuu, Maxence Melo - ametoa shukrani mbalimbali baada ya kupokea tuzo amabazo tutapandisha si punde.

IMG-20190906-WA0018.jpg

Sehemu ya Hotuba ya Maxence Melo:

Anaanza na Salamu kwa mgeni rasmi na wageni wote.

Sisi kama JamiiForums (wadau na waendeshaji) tunashukuru sana kwa fursa hii. Nichukue nafasi hii kwa kusema wanahabari tunakutana na changamoto kubwa sana. Inatia faraja kuwa tunayopitia yanaonwa na yanaleta tija.

UTPC wamekuwa wakinialika kwenye siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani lakini miaka 2 iliyopita nimeshindwa kwenda kwa sababu huwa kesi yetu ilikuwa inatajwa ama kusikilizwa mahakamani tarehe hiyo.

Na leo nimeomba ruhusa mahakamani. Naishukuru Mahakama na dola kwa ruhusa.

Tasnia ya Habari imekutana na changamoto ya sheria mpya na mabadiliko ya mifumo. Unaweza pitia mambo ukadhani kwamba “It’s not worth it” lakini haya ndo mambo tunayotakiwa kuyasimamia.

JF imepitia changamoto. Lakini tumeweza kukabiliana na hali. Tusimamie maadili, tunachokiamini. Kwa sisi JF kama ‘Alternative media’ kuonekana na UTPC tunasema Asanteni sana.

Tuwapongeze wanaotumia mitandao kwa ujumla pia.

Nawapongeza watendaji, bodi ya wakurugenzi na zaidi niwapongeze wanahabari, members wa JamiiForums (wanaotumia mtandao wetu wa JF na walio katika kurasa zetu za kijamii).

Nawapongeza wanahabari wa Tanzania kwa uvumilivu katika tunayoyapitia. Tunapitia changamoto nyingi lakini tunaendelea kufanya kazi kwa weledi kabisa.

Asante kwa ubalozi wa Sweden!

Maxence Melo amesema tuzo hiyo si ya JamiiForums pekee bali ni kichocheo kwa wanahabari wote kwa maelezo kuwa tasnia ya habari Tanzania haiko salama licha ya uvumilivu mkubwa walionao wanahabari.

Hii ni tuzo ya tatu kwa Jamii Forums, 2019. Tuzo ya kwanza ilitolewa kwa Mkurugenzi wake, Maxence Melo na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu na ya pili ikitolewa na CPJ


1.jpg
2.jpg


4.jpg
5.jpg

10.jpg
 
C2E9694F-5CAF-4547-8AB2-F8BB5DADB4FE.jpeg


Kwa ufupi, napenda kusema:

Asanteni watanzania, asanteni wadau wa JamiiForums (members wa JF na wale wanaofuatilia kurasa zetu ktk social media), asanteni sana wadau mbalimbali mnaoendelea kuwa nasi katika safari yetu, asanteni sana Bodi ya Wakurugenzi ya JamiiForums, asanteni Menejimenti na Watendaji wote wa JF (pamoja na wale waliowahi kushiriki safari hii kwa namna moja ama nyingine aidha wakaishia njiani au wakatangulia mbele za haki). Tunawashukuru UTPC kwa kuthamini kazi yetu.

Safari hii tunaisafiri pamoja na changamoto tunazokumbana nazo zinatuathiri sote.

Poleni ambao nimeona mkilalamikia kufungiwa (ban) katika JF. Niwahakikishie, sio kitu tunakipenda lakini nashauri mjaribu kuzipitia sheria zilizopitishwa tangu 2015 hadi 2019 mkaelewe kwanini pengine tunalazimika kuwalinda kwa kufanya maamuzi ya kuwafungia kwa muda. Suluhu ya hili inakuja soon.

Mwisho, nizidi kuomba ushirikiano wenu katika hatua inayofuata kwani bila ushirikiano wenu ni ngumu kufanikisha zaidi. Mwenyezi Mungu azidi kutubariki.
 
Jf hongereni sana, kuhakikisha kuna Uhuru wa watu kuongea na kuhakikisha kunakua na haki na usawa bila kujali.

God bless you muendelee kufanya vizuri na mpate tuzo nyingi zaidi.
 
Kama bado hii ni jamii forum ninayoifahamu toka kipindi hichoo..nadhani ni memberbased forum.....Hii tuzo ni yetu sote nasio amepokea kwaniaba ya watendaji wa taasisi ya jamii forum, JF Si chochote ukitutoa wanachama.
Ni kama unaposikia ndege yetu imekamatwa afrika Kusini, sio kwamba ni mali yetu wote hiyo ni lugha tu ya kisiasa
 
Back
Top Bottom