JamiiForums yamwezesha Kupata Ng'ombe Bora wa Maziwa

Lakini wakati anasubiriwa azae. Namshauri muuzaji amshauri mteja juu ya malisho sahihi kipindi hiki cha gestation.

Maziwa na kiwele hujengwa haswa kipindi cha mimba ya uzao wa kwanza.

Ng'ombe nyingi zitokazo Meru na maeneo jirani yake huwa zimelishwa migomba sana na hazipendi pumba. Kigamboni migomba sio mingi sana kama niko sahihi, lazima afundishe ng'ombe kula pumba na virutubisho vingine vingine mapema sana kabla mimba haijawa kubwa.

Meru ni eneo lenye ubaridi, nashauri kwa huyo mteja wa kigamboni azingatie maji kwa kipimo, kigamboni kuna joto sana kulinganisha na alipotoka mfugo. Kila saa atasikia kiu, lakini kumpa maji mengi sana kwa siku kutaathiri maziwa.

Kila la kheri mteja
Mdau nimekuelewa sana unaonekana ni mfugaji mzoefu. Niko na swali. Kwanini umesema kunywa maji mengi sana kutaathiri maziwa? Je, umebase kwenye wingi wa maziwa au wepesi wa maziwa?
 
Usemayo yanaweza kuwa kweli sana.

Lakini Meru hiyo hiyo zipo Institutions kama mbili hivi zinazohusika na mifugo na ni za serikali.

Kuna
1. National Artificial Insermination Centre - Uzalishaji kwa chupa

2. LITI - Tengeru

Uwepo wao hawa umechangia sana Meru kuwa na Mbegu bora za Ng'ombe. Lakini wao pia wana assist sana kwenye ununuzi wa mifugo.

Uwepo wa madalali ni changamoto kila mahali
Niliwahi kusikia hata mikoa ya nyanda za juu kusini zinafaidika na miradi ya aina hii ya mbegu nzuri za ng'ombe wa maziwa kutoka ulaya ila sijafanikiwa kuzifahamu hizo institutions.
 
Nisaidieni wakuu nini tofauti ya Freshian na Eshian/Asian
Kwa uelewa wangu mdogo nikionao Freshian wako na rangi nyeusi na mabaka/ madoa meusi wako na sifa ya kuwa na uwezo mkubwa sana wa kula chakula pia kutoa maziwa mengi sana. Ashian huwa na rangi nyekundu na vinywele vilivyosimama katikati ya kichwa. Wanakula kiasi hata wingi wa maziwa yao ni kwa kiasi. Ngoja wadau wabobezi waje wafafanue zaidi
 
Asante mkuu
 
tmp-cam--559373284.jpg
 
Shida je ni Pure?tatizo sio Rangi mkuu ishu ni.kupata pure.
 
Kwa kawaida Freshian aina ya Zulu na Kiwi kutoka South Africa wanakamuliwa lita 24-26 kwa siku kwa ulishaji mzuri lkn ukiwa na malisho ya kutosha na ulishaji wa kisasa unaweza kukamua hadi lita hadi 30 kwa siku. Ninaposema kwa siku namaanisha mikamuo miwili asubuhi na jion
Hii mbegu ndio ninayoitaka kwa mwanza majani yapo ya kutosha je nikiitaji ngombe mmoja mwenye mimba nitampataje na je naweza kuja huko meru kulipia na kumpakia kwa gharama zangu mwenye mimba??
 
Back
Top Bottom