Jamiiforums tuanzishe Scholarship kama mchango wetu kwenye maendeleo ya Elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamiiforums tuanzishe Scholarship kama mchango wetu kwenye maendeleo ya Elimu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by green29, Apr 26, 2010.

 1. green29

  green29 JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Wanajamii wenzangu, natoa hili wazo kama mtanzania.

  Wapo wenzetu wengi wanaoishi kwenye mazingira magumu na wanasali na kuomba ili siku waamke wakute wamebahatika kujikuta wako shule/chuo wanapata elimu. Nahisi Jamiiforums, ikiwa si chama cha siasa bali ni Kusanyiko la Watanzania wanaoipenda Tanzania, inayo nafasi kubwa kuchangia katika kutatua matatizo kama haya kwa namna nyingi ikiwa ni pamoja na kusaidia kwa vitendo(kuonyesha mfano) au kwa kupiga domo.

  Nashauri tuanzishe Scholarship ambayo mtanzania yoyote (mwenye sifa tutakazoamua hapa)anaweza kuomba na kuweza kwenda shule kwa jasho la watanzania. Kwa mfano mayatiima, walemavu wenye nia na "proven exceptional skills" lakini wamekosa economic means.

  Chanzo cha pesa ni michango yetu.

  Naamini hii pia itasaidia kuitangaza JAMIIFORUMS kama mkombozi wa mtanzania
   
 2. green29

  green29 JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Natoa hili wazo kama "wazo mbegu" lakini naamini wapo watu wengi wenye uzoefu na mawazo kama haya na wanaweza kulipanua hili wazo kiufundi zaidi na tukafanya kitu kikubwa. Tunaweza kulenga zaidi vyuo vya nyumbani na nguvu ikiwa kubwa tunaweza kufanya jambo kubwa zaidi. Kuna uwezekano mkubwa wapo watanzania wengi wenye moyo na nia ya kuchangia lakini kwa sababu hakuna coordination mechanism au "vision" /"mission" hili jambo halipo Tanzania.
   
 3. G

  GodHaveMercy Member

  #3
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah! Hilo bonge la wazo, green! Ulijuaje?
   
 4. joellincoln

  joellincoln Senior Member

  #4
  Apr 27, 2010
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wazo zuri sana si kuchangia kwenye miharusi tu nafikiri tuanze kufocus na kwenye maeneo kama haya kwa kweli tutakuwa tumepiga hatua nzuri. Labda tupate mawazo zaidi kutoka kwa wadau tujue hii inaweza kufanyikaje.
   
 5. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,653
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Ok. Mkifanikiwa kwa hili, ningeomba mnipe Scholarship ya kusoma Mwissi Primary School so that I may grow up into a Big Time Politician and (God willing) build a big-ass mansion one day on none other place than Toure Drive itself ...
   
 6. green29

  green29 JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Uko sahihi, michango yetu kwenye maharusi inaonyesha kuwa linapokuja suala la ELimu pia uwezo tunao, na sababu tunazo, ni kujenga kwenye nia tu. Michango ya harusi tunachanga kwa muda mrefu na kuila na kuinywa kwa siku moja. Kuwekeza kwenye elimu tunaleta mageuzi ya kudumu kwenye Taifa.
   
 7. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Hey, Mwissi? Hii shule iko wapi ndugu. i think I know the place!
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kwanza Kabisa kabla ya wewe kwenda mbali huko ulikosema kwanza ningependa wewe Utowe Mchango wako hapa Jamii Forums Utoke wewe kwenye JF Senior Expert Member Uwe Wewe JF Premium Member Waswahili Wanasema hivi Mkono Mtupu Haulambwi Towa Mchango wako hapa na hao pia wanaokujibu watowe Michango yao kisha tuangalie hilo wazo lako asanteni.
   
Loading...