JamiiForums Premium Member Subscription | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JamiiForums Premium Member Subscription

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mike Mushi, Jun 20, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF

  Awali ya yote, niwashukuruni nyote!

  Tumeliongelea hili jambo kwenye andiko hii, Na sasa ni utekelezaji wake.

  Lengo kubwa la kuanzisha utaratibu huu ni kuiwezesha JamiiForums kujiendesha kwa ufanisi zaidi ndani na nje ya Tanzania.

  Tunayo mikakakati tuliyoianda ya jinsi gani tunafikiri JF inatakiwa iende, na tunaahidi kuwashirikisha kwanza "Premium Members" wetu kabla haijaanza kutekelezwa.

  Hizi alama maalumu zitadumu kwa mwaka moja.

  Baada ya mazungumzo marefu ya jinsi ya kupanga hii michango tulikubaliana hivi


  Annual Membership Subscriptions

  JF Bronze Member 20,000 - 99,000

  JF Gold Member 100,000 - 249,000

  JF Platinum Member 250,000 - 490,000

  JF Tanzanite Member 500,000 - Na zaidi...


  [​IMG]


  Utaratibu wa Malipo  M-Pesa

  Tumefanikiwa kupata utaratibu mzuri sana wa kulipia kupitia M-Pesa. Utalipia Subscription Fee kama vile unavyonunua Luku au DSTV na kutuma kwenda kwenye number 888 888


  Jinsi ya Kutuma


  1. *150#

  2. Bonyeza 4 (Pay Bill)

  3. Bonyeza 1 (Enter Business Number)

  4. Weka 888888

  5. Enter Reference No. (tumia 1234)

  6. Enter Amount (Weka kiasi unachotaka kutuma)

  7. Weka password yako na kisha utume.

  Ukishatuma, tuma PM kuja kwangu Mike McKee ukituambia receipt no. uliyoweka na jina lako unalotaka liwekewe Premium Member au tuma email kwenda premium@jamiiforums.com ukituambia receipt number.


  CRDB Bank

  Account Name: Jamii Media Company Limited
  Account Number: 0150413278400
  Branch: CRDB Waterfront


  Ukishaweka pesa tuma SMS kwenda number hii 0755 642 929 kutuambia jina gani umetumia wakati unaweka hela, na nikiasi gani umeweka, na kutuambia jina unalotaka liwekewe alama maalumu (premium membership).

  Sisi tutaithibitisha kwa alama maalum (icon) na kukuwekea kwa hilo jina.

  Kwa wale watakaotumia malipo kwa njia ya mtandao (online transfer) ya CRDB, wanaweza wakatutumia receipt kwenda kwenye email ya premium@jamiiforums.com


  WesternUnion

  Name: Mike Mushi
  Address: P.O.BOX 4203 Dar es Salaam
  Phone: 0755 642 929
  Email: premium@jamiiforums.com


  PayPal

  Tuma kwenda kwenye email hii premium@jamiiforums.com  Maswali na Majibu


  Alama maalumu kwa mtumiaji(Verified User) ni nani?

  Verified Users ni wale wanachama wa JF wanaotumia majina yao halisi. Sisi tuna hakikisha kujua kwamba yale majina ni yao kweli na kuwawekea alama maalumu inayoonesha kweli anayeandika kwa jina hili ni yeye halisi.

  Naweza kulipia kwa kidogokidogo?

  Malipo kidogokidogo yanaruhusiwa kwa wale Platinum na Tanzanite members na zinatakiwa kukamilishwa ndani ya miezi minne.

  Nataka kuchangia ila sitaki kuwekwa kwenye makundi

  Unaweza ukachangia kwa kutumia viwango hapo juu na usiwekwe kwenye hayo makundi ila ukawekewa "alama" ya premium member inayoonekana hapo juu.

  Kuna faida gani nikiwa Bronze Member na nikiwa Tanzanite Member?

  Lengo la hii program ni kuwezesha JF, hapa kinachofanywa ni uchangiaji na sisi tunachofanya ni kukutunuku "badge" kutoka na ulichochangia ili kutambua na kuthamini uchangiaji wako.

  Lengo letu ni mwakani tuweze kutoa packages nzuri kwa kila package. Na sisi pia inatupa mwangaza wa kutambua ni watu kiasi gani wapo, na wenye nia ya kuchangia na kununua hizo packages zitakapoanza.

  Kwa kipindi cha mwaka mzima kuna vitu vingi vitakuwa vinaanzishwa na vingi mtakuwa mnatuambia "premium members" mnataka nini.

  Hivyo vitu watakaokuwa wa kwanza kujua na kuvitumia kabla havijaanza kuwa wazi ni hawa premium members wetu. Maana yake maoni, ushauri unaanza kutolewa na hawa kwanza.

  Kuchangia JF na kuwa premium member kunakupa nafasi wewe kuwa mmoja ya wanachama muhimu watakaoongoza mabadiliko na kuwa mmoja wa watakaoshuhudia mabadiliko hayo ya JF.

  Je Subscption fee yangu ya mwaka mzima inaanza lini?

  Subscription fee yako ya mwaka mzima inaanza pale utakapolipia. Kama utalipa July, itakwisha july mwaka kesho.

  Kwanini hakuna malipo ya TigoPesa na Airtel Money?

  Utaratibu kama tulioupata Mpesa ndio tulikuwa tunautaka kama huo TigoPesa, sasa TiGo wamesimamisha hiyo huduma mpaka mwezi wa nane. Hatuna tunachoweza kufanya ni kusubiri mpaka mwezi wa nane. Njia ya kawaida ya kuchukua line ya tigopesa na kuiweka hapa sio salama na wote tunafahamu hii, mtu anaweza kudurufu laini na akaenda kuchukua hiyo pesa.

  Airtel Money bado tupo kwenye mchakato wa kupata utaratibu mzuri, na itakapokamilika itawekwa hapa.

  Je, inamaana nisipolipia premium members sitoweza tena kuipata JF?

  Hapana, JF itaendelea kuwepo kama kawaida.

  Hamuoni kuweka hizi "levels" mtaleta matabaka ya waliokuwanacho na wasiokuwa nacho na wachangiaji watawaogopa Tanzanite au Platinum members?

  Kwanza lazima tuelewe kwamba "levels" zipo kama "incentive" ya kuwapa hao waliochangia na kiasi gani wamechangia pia kuvutia wengine wachangie. Hii ni kama harambee hivi. Na pia unaweza ukachangia na pia usitake kuwekewa hiyo "alama" ya premium member wala hizo "badge" za levels ukabaki kama kawaida.

  Na pia kama kweli utaogopa username ya mtu yenye "alama" ya tanzanite na utashindwa kuongea au kubishana kwenye mada kwasababu unaogopa labda anapesa, sasa hapo tatizo ni kwako wewe. Inakuwaje unaogopa username ya mtu na inakunyima wewe uhuru?

  Na kama kweli italeta matabaka na itaondolea watu uhuru wa kuongea, basi itakuwa haina faida na hatutasita kuisitisha.

  Mwisho wa siku, kama wewe ni tanzanite member na hufuati sheria za JF, unapata BAN kama kawaida.
   
 2. mwitaz

  mwitaz JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Umesomeka na umeeleweka
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,498
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  nini privileges za platinum and tanzanite over the other premium status
   
 4. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu, maelezo yote yameandikwa hapo juu kwenye maswali na majibu
   
 5. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Je kuna option ya kununua hisa (stake) za JF?
  Kiujumla wazo lako (lenu) ni jema.
   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,498
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  hapana.... it seems swali langu haliko clear

  what is there for me? umesahau tulivyo? huwa tunapenda vya fasta, lol
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 64,185
  Likes Received: 62,311
  Trophy Points: 280
  Lengo letu ni mwakani tuweze kutoa packages nzuri kwa kila package. Na sisi pia inatupa mwangaza wa kutambua ni watu kiasi gani wapo, na wenye nia ya kuchangia na kununua hizo packages zitakapoanza.

  Kwanini hii package isitolewe mwaka huu badala ya mwaka kesho na hivyo kuwavutia wanachama wengi kuchangia!? Kuna kipingamizi gani kinachozuia hili?
   
 8. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,670
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  Hongera sana mkuu Mike McKee kwa maelexo yako ya hapo mwishoni yanayosema kuwa haijalishi wewe ni premium member au non premium member under JF all of us are the same na wote tunaoaswa kufuata sheria za JF na endapi tutazivunja sheria lazima ifuate mkondo wake. Big up sana mkuu, kilichobakia ni utekelezaji tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapana. Hakuna hiyo option kwa sasa.

  Hii ni uchangiaji. Kuchangia JF na kuwa premium member kunakupa nafasi wewe kuwa mmoja ya wanachama muhimu watakaoongoza mabadiliko na kuwa mmoja wa watakaoshuhudia mabadiliko hayo ya JF.

  Mkuu, Ni ni uchangiaji na kuiwezesha JF. Baada ya hapo ndio hizo packages nzuri zitakuja.
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Verified User ni ya Nini?
   
 11. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,920
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Safi sana mkuu kwa maelezo.

  Swali langu, kwenye ku-introduce huduma mpya na mambo mengine, umesema mtachukua ushauri wa premium members; kwa vile mara nyingi maoni yanapishana, kuna uwezekano wa premium members kupewa nguvu ya kupiga kura kwenye maamuzi ya JF? Yaani maamuzi ya mwisho yatokane na kura za wazi zilizopigwa na premium members.
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna members wanao tumia jina zao halisi kwa kujiunga JamiiForums na kuchangia hoja mbali mbali. Kuna utaratibu wa kuthibitisha kua members hao are who they claim to be. Baada ya kujiridhisha kua ni wenyewe, wanapewa status ya verified member ambayo inaonekana pamoja na premium membership yao.
   
 13. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #13
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu, Maelezo nimeandika hapo juu na ninarudia tena.

  Alama maalumu kwa mtumiaji(Verified User) ni nani?

  Verified Users ni wale wanachama wa JF wanaotumia majina yao halisi. Sisi tuna hakikisha kujua kwamba yale majina ni yao kweli na kuwawekea alama maalumu inayoonesha kweli anayeandika kwa jina hili ni yeye halisi.

  Oxlade-Chamberlain Wazo lako ni zuri. Mawazo hayafanani na muda mwingine inabidi sisi tutumie busara kuchagua kipi kifanyike na kipi kisifanyike. Kuwa na kura kwenye maamuzi ya JF ni jambo jema itatupa sisi nafasi ya kujua idadi kamili ya watu wanaopendelea mawazo fulani ila hii isitunyime sisi wakati mwingine kufanya maamuzi magumu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,920
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa mkuu, pale kwenye maamuzi magumu mtatumia nguvu yenu kufanya maamuzi ya mwisho. Kama marais wanavyofanya lol.

  Naona kama premium members watashirikishwa kwa njia ya kura itaonesha zaidi umuhimu wao na pia watapata nafasi ya kutoa mapendekezo na kuyajadili kwa pamoja na mwisho kutoa maamuzi kwa kupiga kura.
   
 15. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #15
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kweli Mkuu. Wazo lako ni zuri sana. Tutalifanyia kazi, mfano tukiwa na ideas zaidi ya tatu na tunataka kujua tuanze na ipi, tunaweza kutumia njia ya kura.
   
 16. D

  Daniel Muhina Member

  #16
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi niliyejiunga juzi naweza lipia na kupata hizo incetives kama ulivyo ziita?
   
 17. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,539
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Hemu nitoe ushamba package nini?
   
 18. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #18
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndio Mkuu inawezekana

  Sijakuelewa mkuu
   
 19. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa sisi tunaoishi kama upepo humu, tutalazimika kuwa na ALAMA MAALUMU?
   
 20. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuishi kama upepo humu maana yake ni nini mkuu
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...