TUSHIRIKISHANE JamiiForums na Tushirikishane, CHADEMA na UKUTA

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,014
8,368
MIAKA mingi iliyopita JamiiForums ilikuja juu na agenda ya ufisadi katika nchi hii, na kwa namna moja au nyingine kwa mtu yoyote aliye makini atakuwa anakumbuka kuwa JamiiForums ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kusaidia vyama vya upinzani nchini kushikia kidedea agenda hii na kufanikiwa kwani ni kupitia JamiiForums watu viongozi wengi wa upinzani walipata taharifa zilizo sahihi dhidi ya agenda ya ufisadi.

Pamoja na kwamba kupitia JamiiForums, agenda hii ilimulikwa sana na walioandikwa wengi wao waliishia kuendelea kutamba mitaani ila JamiiForums kupitia member wao walitimiza wajibu wao na kwa namna moja au nyingine hata wale wezi waliomulikwa walau hata kama hawakushitakiwa na utawala uliopita, walipunguza kidogo na kwa utawala huu, kidogo wale walioanikwa sasa wanaishi matumbo joto.

Katika ili hatuna budi kuipongeza JamiiForums kwani imekuwa chachu ya ufanikiwaji wa agenda hii!

Kufanikiwa kwa JamiiForums, ni sawa na kufanikiwa kwa CHADEMA katika agenda zao mbalimbali mathalani ile ya Movement for Change, Operation Sangara na nyingine. Wengi hapa mtashangaa kwanini nafananisha mafanikio haya ya vitu viwili tofauti, ila ninazo sababu ambazo zinanisukuma kufananisha vitu hivi viwili.

Ni hivi majuzi tu tuliona CHADEMA ikija na UKUTA kama program mpya, ila tangu ianze kuhubiriwa hakuna kilichofanyika mpaka leo ingawa lengo la agenda hiyo lilikuwa zuri kwa ustawi wa vyama vya upinzani nchini. Kimsingi CHADEMA kwa mara ya kwanza ilishindwa kabisa kupenya katika kutekeleza agenda hiyo. Kushindwa huku kuna madhara makubwa sana.

Je, JamiiForums itajenga historia ya pekee baada ya mradi wa TUSHIRIKISHANE kufanikiwa?

Pengine wapo mtakaokuwa mnajiuliza kuwa huu ni mradi gani? Kwa siku ya leo mimi kama mwanahabari nilikuwa miongoni mwa wajumbe tuliohudhuria katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa TUSHIRIKISHANE, huu ni mradi unaolenga kuwawezesha wananchi kujua ahadi zilizoahidiwa na viongozi wao na kuweza kuwaadhibu pale itakapoonekana hawajatimiza wajibu wao.

Agenda hii, sio nyepesi ni agenda ngumu na mbaya kwa watawala, maana kupitia wajumbe wa warsha hii, JamiiForums inalenga kutengeneza mabalozi watakaokuwa wanawakumbusha wananchi dhidi ya uwajibikaji wa viongozi waliowachagua ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Kwa mujibu wa mmoja wa wawasilishaji agenda hii, nimemsikia akisema kuwa sasa kwakuwa JamiiForums kwa kiasi kikubwa imefanikisha kuibua agenda ya ufisadi nchini na kwakuwa imefanikiwa basi kwa sasa tunataka wananchi wa nchi hii ambao wamekuwa wapiga kura kujua kuwa wanastahili kuheshimiwa na waliowachagua kwa kuwatimizia walioyaahidi.

Mradi huu, kwa mujibu wa mtoa mada unaanza kwa kufanyika katika baadhi ya majimbo nayo ni Bukoba Mjini, Nzega Mjini, Kigoma Mjini, Mtama, Kigamboni na Arumeru Mashariki. Kwa leo nilikuwa katika jimbo la Kigamboni kama mkazi wa jimbo lile. Tulikuwa na baadhi ya madiwani kutoka jimbo la Kigamboni, cha ajabu mbunge wetu hakuwepo wala hakuweza kutuma mwakilishi wa kuja kumwakilisha. Hili ni pigo namba moja kwa mbunge huyu.

Haiwekezekani mbunge awe 'busy' na Katibu wake awe busy. Kwa wabunge ambao mradi huu unapita katika majimbo yenu niwasihi sana kuwa mshirikiane na JamiiForums msidharau kwani mdharau mwiba, mguu huota Tende. Wapo watawala waliodharau agenda ya ufisadi kupitia JamiiForums, sasa kama nyie wabunge mwadharau nilichokiona leo walahi mnajiapalia kaa la moto.

Pamoja na mradi huu kutoka JamiiForums, ninayo machache kwenu, nayo ni-;

Kwanza katika kuwasilisha kwenu nitaomba kujua ni kwa jinsi gani mnategemea kufanya kazi kwa kushirikisha wananchi wa jimbo husika?

Pili, ni kwa jinsi gani mmejipanga kuhakikisha viongozi wazembe hawatumii nguvu zao kuwawajibisha kwa kutumia nguvu zao?

Tatu, ni kwanini msingeanzia kwa majukumu ya madiwani kwa wananchi maana wao ndio wenye wananchi na sio wabunge?

Nne, je waratibu wa mradi watakuwa na nguvu gani ya kutohongeka na kujikuta wanapaka mafuta mtu aliyeshindwa kutimiza wajibu wake kwa wananchi?

Tano, leo mmesema kuwa mmeshapitia majimbo mbalimbali, kwanini hamjaanzisha uzi maalumu ili kuwapa taarifa wana JamiiForums ili kuweza kujua kuwa kwa sasa JamiiForums inajielekeza nguvu katika kuhakikisha wananchi wanajengewa uwezo wa kuwapiga chini viongozi wao pale watakapo prove kuwa hawajatimiza wajibu wao?

Ushauri!

Wanarsha wote wawe na mtandao wao, waweze juana kutoka katika majimbo teule ili kubadilishana uzoefu.

Naomba msiwahusishe wanahabari wengi wa nchi hii, sio wote maana wengi wao wamekuwa wakinunuliwa wakati wa uchaguzi na viongozi wale wale ambao walikuwa wakiishi kama miungu na kuwapaka mafuta kwa uchafu walionao na kujikuta wanakuwa wasafi bandia na kupewa fursa tena.
Ninaomba wanaohudhuira warsha hii baada ya warsha wapewe vyeti vyenye mhuri wa JamiiForums ili iwe chachu katika maisha yao.

NB: JamiiForums mkifanikiwa kwa hili mimi nitashauri muunde chama cha siasa kitachoitawala Africa na si Tanzania miaka 20 ijayo!

Tukutane kesho kwa kuwajuza kitakacho jili kwenye siku ya pili ya warsha ya TUSHIRIKISHANE!

sifileo!


========

Ufafanuzi zaidi kuhusu TUSHIRIKISHANE..

Mtandao wa JamiiForums.com umezindua rasmi mradi wa unaowashirikisha viongozi wa kuchaguliwa(hususani wabunge na madiwani), Serikali(Halmashauri) na Wananchi katika kurahisha upatikanaji wa maendeleo.

Mradi huu unaotambulika kama "Tushirikishane" una malengo ya kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi.

Pia Tushirikishane inalenga kuzisaidia Halmashauri kuboresha utoaji huduma za jamii kwa ufanisi zaidi. Mwitikio(maoni, ushauri na kero) wa wananchi katika mnakasha wa Jimbo/Halmashauri utachukuliwa kwa umakini na viongozi hawa ili kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa wananchi.

Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums.com, Bwana Maxence Melo aliwapongeza viongozi wa Wilaya, watendaji wa Halmashauri, Madiwani na Mbunge kwa mwitikio mkubwa walioonyesha katika kuupokea mradi wa Tushirikishane.

Maxence aliwafahamisha kwamba Mradi huu utatekelezwa katika majimbo sita (6) kwa kuanzia na Bukoba Mjini limekuwa Jimbo la kwanza katika kuanza utekelezaji wake. Jimbo la Pili katika mradi huu limekuwa la Nzega, litafuatiwa na la Kigoma mjini na kisha Sengerema. Majimbo ya Mtama, Kigamboni na Arumeru Mashariki yatafuatia.

Alifafanua kuwa mradi huu utachukua miezi 9 na hivyo Wabunge wanaohusika kwenye mradi huu wanatakiwa kukubaliana na wananchi juu ya ahadi zisizozidi 4 za kuweza kuwa sehemu ya mradi huu zinazoweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa mradi huo.

Bwana Maxence pamoja na timu yake ya wataalam walikuwa Bukoba Mjini kwa siku tano kuendesha warsha iliyowawezesha wadau kuuelewa mradi kwa ufasaha, kutambua majukumu yao na kujua njia zitakazotumika katika kutekeleza mradi kwa faida yao.

Warsha ya Tushirikishane ilifanyika Bukoba Hotel na wadau wanaowakilisha Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wapiga kura na wananchi wa Bukoba Mjini, Madiwani wa vyama vyote pamoja na Mbunge wa Jimbo walishiriki.

Malengo ya Tushirikishane

Pamoja na lengo kuu tajwa hapo juu, Mradi huu una malengo mahususi yafuatayo:
i. Kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi wa kuchaguliwa na serikali yao (kwa njia ya mtandao, magazeti, redio, televisheni na mikutano ya wazi)
ii. Kurahisisha upatikanaji wa habari na taarifa za umma zikiwa kwenye lugha rahisi
iii. Kuchochea majadiliano ya wazi, yenye tija na staha kati ya wananchi na viongozi wao
iv. Kusaidiana na viongozi wa kuchaguliwa katika kutengeneza nyenzo za muhimu katika kutekeleza ahadi.

Matarajio ya Mradi

Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:

i. Kujengeka kwa utamaduni wa majadiliano yenye staha kati ya viongozi na wananchi kwenye mitandao ya kijamii
ii. Kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika utekelezaji wa sera na ahadi za wakati wa Uchaguzi.
iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa sera na ahadi za kipindi cha uchaguzi.

JamiiForums itakuwa inakuletea matukio yote kuhusiana na mradi huu kwa kadiri utekelezaji wake utakavyokuwa unaenda katika kila Jimbo.

Kupata habari kwa undai zaidi kuhusu Tushirikishane inavyo fanya kazi, Fungua hii Link=>JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"
 
Mkuu sifi leo hata mimi nilikuwepo kwenye warsha ya Kigamboni. Naona mbunge wetu kajitahidi kutimiza ahadi moja. Mwezi huu kivuko kipya kinakuja.

Screenshot from 2017-01-10 06:29:11.png
 
Back
Top Bottom