JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Mnaotaka muwekewe namna ya kubadili username hilo msahau kabisaaa, niliwahi kua kwenye mtandao mmoja wa live talk kulikua na hiyo option ya kubadili username looh mtu anakucopy name yako anakuchafua atakavyo kisha anarudisha jina lake wewe unaanza kuhaha kujisafisha maana watu wanajua ni wewe, ilikua mbaya sana.... kwa humu pia wanadhibiti hayo mambo ya multiple usernames.

Kitufe cha Dislike, cha nini sasa kama hujapenda post au comment ya mtu pita kimya kimya au sonya huko ulipo basi endelea na mada zingine.

Guys, mkumbuke hii ni FORUM.
Multiple username/ID haina madhara na haiwezi kuzuiwa kanwe maana haivunji sheria za Jf
Hata wewe unaweza kuwa na ID zaidi ya 10 ilimradi huzitumii vinaya(kutukana,kujianzidhia mada n.k)
Sio kila mwenye multiple ID ana lengo baya wengine ID za biashara,Chitchat na verified user)
 
Naomba pia muongeze jukwaa la
SAFARI (Travel)

Hapo member watatoa uzoefu wa maeneo mbalimbali waliyowahi au wanatarajia kusafiri, jinsi ya kuomba na kupata visa, maisha ughaibuni n.k Pia member wanaweza share
Diaries zao za safari, picha mbalimbali za maeneo waliyotembelea nk
 
Wazo zuri but tatizo ni pale ambapo mtu ameguna au ameandika nimewahi siri, au ngoja waje na watu wanamwagia likes.... Hebu fuatilia uzi wenye pages nyingi humu ndani utashangaa kweli...
Utaratibu huu ukianza nadhani watu watawapotezea hao.
Hata hivyo, kwa kipindi hiki naona watu wameanza kupuuza hao watu wanao wahi na kiandika hivyo
 
Tuko pamoja...alafu usisahau kitufe cha kugundua stori za uwongo wakitusumbua kuwapa ushauri.
 
Mkuu Maxence Melo habari yako
Swali langu ni hili je kipi kiliwashawishi kufanya utafiti na kukusanya maoni nje wanajamiiforums wenyewe. Kwa maelezo yako inaonekana mmefanya utafiti physically yaani mtaani. Je hamuoni maoni mliyopata si mengi kuliko mngeamua kufungua uzi humu wa kukusanya maoni?

Maoni yangu
1.Kwa kuwa sasa east africa community nchi wanachama zimeongezeka basi mngefanya busara kuweka jukwaa moja tu la east african community kuliko kuweka Ugandan forum ambalo limepoa na Kenyan forum ambalo kazi yao ni kuweka ligi na wabongo hakuna la maana wakenya wanajadili zaidi ya chuki.

2.Kuhusu Private Message
Najua muundo wa pm mliuchukua kutoka google mail ila sasa tungependa muondoe muundo ule umekuwa na mlolongo kwenye kuandika hasa kile kipengele cha SUBJECT. Sioni mantiki ya kuandik kichwa cha habari kwenye ujumbe mfano namtongoza dem pm basi nianze na kichwa cha habari eti MTONGOZO.

3.Changamoto dhidi ya serikali
Kutokana na changamoto mlizopitia za kuzuiwa kutoa huduma na kushambuliwa kimtandao,kwa maoni yangu hayo yote yametokana na thread za kisiasa za kuishambulia serikali na chama kikongwe. Jamiiforums sio siasa tu na si wote tulio na interests za kisiasa kama ilivyo dini. Naona umefika wakati sasa jukwaa la siasa liwe kama jukwaa la dini au la wakubwa kwamba mtu anayetaka kuingia humo basi aombe kwa hiari yake na sisi tusio na lengo la kuingia humo basi tubakie na majukwaa yetu pendwa.

4.Mapato kupitia matangazo madogomadogo
Jamiiforums kwa sasa ni kijiji kila kitu kinapatikana humu sasa naomba mfikirie kuhusu kuongeza mapato ya mtandao wenu kupitia matangazo madogomadogo. Sisemi hili kama kuwakandamiza wanaopost matangazo ila kutokana na utapeli unaofanyika kwa baadhi ya watu humu kuweka matangazo feki ya bidhaa zao. Ufike wakati sasa mchukue hatua ya kumonitor matangazo haya yaani mkae katikati ya muuzaji na mnunuaji. Muanzishe kitengo cha matangazo ili mimi nikitaka kuweka tangazo basi inabidi nililete kwenu mfanye uhakiki wa bidhaa na bei halafu ndio mliweke mtandaoni,pale anapotokea mteja basi awasiliane na Mimi kwa ajili ya negotiations na mambo mengine lakini itakapofika hatua ya malipo basi nyie muhusike na mtapata commission kwa kila mauzo. Hapo kutakuwa na faida tatu
Mosi,mtapata faida ya commission
Pili,kutakuwa na biashara halali
Tatu,itavutia wauzaji wengi kutangaza bidhaa zao hapa.

5.Kuhusu utapeli wa forex uliojitokeza siku kadhaa nyuma
Kuna member fulani alileta masuala ya forex humu jukwaani kwa nia ya kufundisha (mentorship). Kimsingi alikuwa na lengo zuri lakini kuna walakini ukitokea katika namna ya uwasilishaji wa baishara yake. Kwanza akaanza kuwarubuni watu kwa maneno matamu pia akatengeneza kikundi chake cha kuwashawishi watu na baadhi ya alioshirikiana nao ni members humu na wanajulikana. Wakaanza kazi yao na hakika mwanzo waliwapata wengi kweli humu lakini mwisho wa siku watu wakatapeliwa na kuanza kulalamika. Hao hao matapeli wakaanza kutengeneza ID tofauti tofauti ili kujisafisha lakini wakashindwa na mwisho starring wako akakimbia na madolari. Lengo la kuandika haya si baya ila kuwapa tahadhari viongozi wa jf muwe makini na pia mjitahidi kuwalinda wanachama wenu dhidi ya matapeli dizaini hii kwa kuwa mlifika hatua hadi ya kuhongwa na matapeli wa forex kwa kigezo cha shukrani.

Yangu ni hayo tu
Jembekillo
Haaahaaa nmecheka hapo kwenye unamtongoza demu unaweka subject MTONGOZO
 
Mkuu msisahau dislike button maana kuna mijitu huwa inalipwa kupost ujinga tu hapa janvini!
Nafikiri wakiweka utaratibu wa comments kujipanga kutokana na likes (kupendwa) itaondoa hilo tatizo la watu kupost ujinga.
Mana comment yake itakuwa ya mwisho, na comments zenye hoja kuwa mwanzoni.

Nimependekeza huko mwanzoni na Max kasema atalifanyia kazi.
 
Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
mkuu kipengere cha kubadili username msisahau
 
Multiple username/ID haina madhara na haiwezi kuzuiwa kanwe maana haivunji sheria za Jf
Hata wewe unaweza kuwa na ID zaidi ya 10 ilimradi huzitumii vinaya(kutukana,kujianzidhia mada n.k)
Sio kila mwenye multiple ID ana lengo baya wengine ID za biashara,Chitchat na verified user)
Nilimaanisha mfano mimi ni culture gal mtu anaweza akabadili jina lake na kujiita culture gal akawatukana watu humu kisha akatulia zake, nyote mtajua ni mimi kumbe mtu kaamua kuharibu tu.
 
Asante Max.

Mi napendekeza kitu katika uzi, zile reply zenye like nyingi ndizo ziwe zinaonekana za kwanza.

Yani katika uzi, reply zinazo ongoza kwa like ziwe zinajipanga na kuonekana mwanzoni.

Hii itasaidia watu kujenga hoja, majibu kupatikana kwa wepesi, na watu kujikita katika uandishi mzuri.

Unakuta mtu kauliza swali lkn unakuta jibu sahihi lipo #80 , mwanzoni ni masihara matupu.

Sasa huyu wa #80 akifikiiwa watu watampa like na kuonekana wa mwanzoni.

Kiufupi, mpangilio wa reply usiwe kutokana na mtu kawahi, bali hoja zilizopendwa na watu wengi (likes).

Cc Maxence Melo
Hapana mtu akiwa kwenye seat yake asinyang'anywe vinginevyo weka alama sehemu yako mapemaaa.
 
Back
Top Bottom