JamiiForums kuwa na waangalizi katika uchaguzi mkuu

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Wana jf nilimsikia mkurugenzi wa kituo cha kisheria na haki za binadamu akitaja JF kama moja ya taasisi zitakazotoa waangalizi wakati wa uchaguzi mkuu.

Nilisikia JF itatoa watu 60 watakaojiunga na wa taasisi nyingine wakati wa uchaguzi hapo 31.10.

Je wewe utakuwa mmoja wao?
 
chodechode wana JF tuitumie hii nafasi ingawa hata wasingetupa tarifa tungezi toa tu....sipati picha tarehe 31-10-mida kama hii hapa JF itakuwa je
 
Mimi ni mmoja wapo lakini sio kupitia LHRC tuliomba Tume na kupitishwa
 
chodechode wana JF tuitumie hii nafasi ingawa hata wasingetupa tarifa tungezi toa tu....sipati picha tarehe 31-10-mida kama hii hapa JF itakuwa je

Patakuwa pamefurika kupita kiasi. Popote ulipo mwanajamii hakikisha unashiriki katika kulinda kura kwa kila hali. Jiandae na camera yako, hata kama ni ya simu, kuchukua picha mara moja ya tukio lolote ambalo si kawaida na kuzitundika hapa.
 
Watakaobahatika kwenda waende maeneo ambayo waangalizi hawapo na wakae mpaka wajue matokeo na kuhakikisha yamebandikwa ukutani..................wasiwe watalii kama hawa wa kimataifa ambao hupitapita tu na hawasubiri kumla ng'ombe wote wanabakiza mkia bila ya kujua hapo ndiyo dhambi kubwa hufanyika....kuhesabu kura na kubandika matokeo yake..............
 
Ningependa kufanya hivyo ila kwa vila sijawa na uhakika wa safari yangu ya kurudi Dar, inawezekana nikawa naondoka mchana ule ule baada ya kupiga kura wakati usimamizi unakuhitaji mtu ukae pale mpaka matokea ya kuhesabu kura yamekwisha.
 
On a serious note kuna haja ya kuunga mkono ilo

Ni kweli, wengi wetu tunaunga mkono hii hoja, na miongoni mwetu humu humu jf, wako members ambao tayari ni waangalizi kupitia taasisi mbalimbali na miongoni mwao, wapo kwenye kundi la waangalizi wa kimataifa, hivyo naamini wote wataiupdate jf as much as they can
 
Good note...For that matter we shall get a witnessed word from horse's mouth!
Kimsingi kila mtu na hasa mwana JF ana jukumu hilo, maana tutatakiwa wote hatimaye kutoa taarifa kwa maeneo yetu!
 
Patakuwa pamefurika kupita kiasi. Popote ulipo mwanajamii hakikisha unashiriki katika kulinda kura kwa kila hali. Jiandae na camera yako, hata kama ni ya simu, kuchukua picha mara moja ya tukio lolote ambalo si kawaida na kuzitundika hapa.

aaaaaaaa,sio mfurike hapa toka asubuhi kupiga domo badala mkapige kura,au wenzetu mko mbali mnapiga kelele za kampeni ambazo hazisaidiiii?
Tunataka sanduku la kura lijae kura,sio jf ijae kura za maoni afu hamfanyi chochote kama mko mbali rudini home mfanye mabadililko sio kila siku tap tap tap tap kwenye computer
 
kumbee mziki wa JF unakubalikaaa.. maana kuna watu huwa wanakandia ati kijiwe cha CHADEMA? hii ni "house of Great Thinkers"
 
Jamani mlioko Bongo hakikisheni mnawabana jamaa wa NEC, na vyombo vyote vya dola. Usione rahisi kuachia tonge mdomo. CCM wanajua utamu wa madaraka. kwa hiyo hawako tayari kuachia kilani hivyo.
 
aaaaaaaa,sio mfurike hapa toka asubuhi kupiga domo badala mkapige kura,au wenzetu mko mbali mnapiga kelele za kampeni ambazo hazisaidiiii?
Tunataka sanduku la kura lijae kura,sio jf ijae kura za maoni afu hamfanyi chochote kama mko mbali rudini home mfanye mabadililko sio kila siku tap tap tap tap kwenye computer

Big up bro.Wana JF waelewe kupiga kura lazima ufike kituoni, labda 2060 tutakuwa kwenye mfumo kama huu wa kutumia mtandao kupiga kura.Ila kuipa ushindi Chadema mwaka huu upigaji kura kupitia mtandaoni 2020 will be must!!.
If your able to check your Registration Status through NEC Web why Not vote too?
 
Naitamania nafasi hiyo sana, kwamaana mwaka huu watu, majeshi, na vyombo vya serikali na wanazi wa ccm wengi tu lazima waumbuke kwa mipango yao itakayowatafuna.
wao wenyewe wanasalitiana halafu wamezidiwa

Natamani kuwa mwagalizi ili haki itendeke
 
aaaaaaaa,sio mfurike hapa toka asubuhi kupiga domo badala mkapige kura,au wenzetu mko mbali mnapiga kelele za kampeni ambazo hazisaidiiii?
Tunataka sanduku la kura lijae kura,sio jf ijae kura za maoni afu hamfanyi chochote kama mko mbali rudini home mfanye mabadililko sio kila siku tap tap tap tap kwenye computer

e bwanae ningekugongea thanks sema hii kitu nnayotumia hapa iph 4 haina kitufe cha kukugongea
 
Mie nitakuwa wakala wa chama changu. Ole wake mtu alete deal za kijinga. Nitamchomoa figo moja hapo hapo kituoni. Bahati nzuri nina mafunzo ya kun fu.
Nitajaribu sana kuleta habari zakituoni kwangu

aaaaaaaa,sio mfurike hapa toka asubuhi kupiga domo badala mkapige kura,au wenzetu mko mbali mnapiga kelele za kampeni ambazo hazisaidiiii?
Tunataka sanduku la kura lijae kura,sio jf ijae kura za maoni afu hamfanyi chochote kama mko mbali rudini home mfanye mabadililko sio kila siku tap tap tap tap kwenye computer
:thumb::thumb::thumb:
 
Back
Top Bottom