Jamiiforums is accessible worldwide. Tunawaomba mtusaidie kuitangaza vema Tanzania yetu walau mara moja tu kila mwezi (Tarehe15 au 28)

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Kama umekuwa ukifuatilia threads zangu nyingi za humu jamiiforums nimekuwa nikishauri mbinu mpya na mbadala ambazo zinaweza kutumika katika kuitangaza vema nchi yetu hususan kupitia njia za kwenye mitandao ya kijamii/social media platforms.

Leo ombi langu kubwa lipo kwa uongozi wa jamiiforums ambao kwa heshima na taadhima zote ninawaomba wao pia washiriki katika campaign hii kuitangaza vema nchi yetu walu mara moja tu kwa kila mwezi aidha iwe Tarehe 15 kati kati ya mwezi au Tarehe 28 ya mwisho wa mwezi.

Ninapendekeza, kuwa na tangazo (banner) la kivutio chochote cha utalii baada ya comment/reply ya kwanza ya kila thread au kwenye homepage baada ya hayo maneno "recommended" na "trending"
View attachment 1170064
Ninafahamu fika ya kuwa hii ni biashara and when it comes to business nothing goes for free, ila tunawaomba kwa heshima na taadhima and for the sake of Patriotism, just help us on this.

NB: NSSF naombeni fao langu la mkupuo kwa maana maisha ni magumu sana huku mtaani. Mungu anawaona mjue?

OUR MOTTO
==========
KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YAKO UNAANZA NA WEWE. JIULIZE UMEIFANYIA NINI LA MAANA NCHI YAKO MPAKA LEO HII.
TBCCM ipo wapi?
si watangazie huko?
 
Ùko wizaran kuna bajeti ya kutangaza utaĺii kwanini wizara isitumie ilo fungu kuwalipa JF ili iwe win win situation, Jf ipate hela ya kujiendesha

Kwanza si Ndege zipo za kuitanga utalii
 
Kwanza washauri wafute kesi za Jamiiforums ndipo tujadili hili mkuu.
 
Bodi ya utalii ni bure kabisa, like seriously mnaomba vya bure kirahisi hicho akati hela ya matangazo mnayo? Hii nchi hii ujanja ujanja mwingi sana. Futa thread boss hayo mambo yanaenda kibiashara watu wanakaa chini wanaweka mpunga mezani. Mmemsumbua sana Max huko mahakamani afu mnataka awe mzalendo kwa kuweka matangazo yenu bure wtf?
 
Wazo zuri, Iongezwe Forum inayogusa masuala yote ya usafiri, hoteli na utalii.
 
Wakamfutie mkurugenzi jf kesi zake kwanza
Acha kupotosha watu, pia acha kucheza na biashara za watu. Yaani jifunze adabu na kitu cha mtu. Ungekuwa Mstaarabu Usingeandika haya hapa, wenzio wanatafuta wahusika wanakaa mezani wanaangalia wasaidianeje sio kwa style hii.. au unadhani Mnaogopwa? Yaani watumie hela yao kutengeneza artwork, watengeneze banner wapost? Sidhani kama unawaza sawasawa. Huo Uzalendo ungeanzia website ya Ikulu au Website za Serikali. Mshaona JamiiForums ndo Mnyonge wenu wa kuwafanyia Matangazo bure halafu hela za Matangazo mkale nyie? Msitamani vitu msivyo na uwezo navyo. Siku zote mwatangaza wapi?

Nawashauri JamiiForums wasithubutu hata kutoa nafasi moja ya Tangazo bure.

Watu waliozoea vya bure bwana.. Jana juzi nliwatafuta niwape mchango wa mwenge hamjapokea simu
 
Achana na maneno ya dhihaka kwenye serious issues. Be matured
Hahaha kwa mtizamo wako dhihaka ni ipi hapo?! Tanzania kujulikana au Kuwa font page mtandao wa CNN kwa kumkamata Kabendera?, Lisu alipopigwa risasi pia Dunia ilituweka font page, Azory alipotekwa na kupotezwa hadi leo tunafahamika, sijui nani anadhihaki nini?!
Unamtangazia nani Tanzania asiye ifahamu?! Kwani hili Taifa ni jipya duniani humu?!
Kila siku nasikia Magufuli wapo wanaosema ni rais bora duniani, sasa anapate rank hiyo kama Tanzania haijulikani?!
 
Kizuri kinajiuza, kibaya kinajitembeza. Umekiri the forum is world wide, yanayo andikwa yanafika mbali. Washauri wahusika na hii nchi wafanye mazuri machoni pa wengi, maandiko nayo yataelezea uzuri, nao wa nje watayasoma. Kinyume chake unataka wakipake sukari kidonge cha shubiri.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Kama umekuwa ukifuatilia threads zangu nyingi za humu jamiiforums nimekuwa nikishauri mbinu mpya na mbadala ambazo zinaweza kutumika katika kuitangaza vema nchi yetu hususan kupitia njia za kwenye mitandao ya kijamii/social media platforms.

Leo ombi langu kubwa lipo kwa uongozi wa jamiiforums ambao kwa heshima na taadhima zote ninawaomba wao pia washiriki katika campaign hii kuitangaza vema nchi yetu walu mara moja tu kwa kila mwezi aidha iwe Tarehe 15 kati kati ya mwezi au Tarehe 28 ya mwisho wa mwezi.

Ninapendekeza, kuwa na tangazo (banner) la kivutio chochote cha utalii baada ya comment/reply ya kwanza ya kila thread au kwenye homepage baada ya hayo maneno "recommended" na "trending"
View attachment 1170064
Ninafahamu fika ya kuwa hii ni biashara and when it comes to business nothing goes for free, ila tunawaomba kwa heshima na taadhima and for the sake of Patriotism, just help us on this.

NB: NSSF naombeni fao langu la mkupuo kwa maana maisha ni magumu sana huku mtaani. Mungu anawaona mjue?

OUR MOTTO
==========
KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YAKO UNAANZA NA WEWE. JIULIZE UMEIFANYIA NINI LA MAANA NCHI YAKO MPAKA LEO HII.
nasikitika kukuambia kuwa kuipamba Tanzania ni kazi ngumu kama kupamba mavi maua.
 
Hili jambo linatakiwa lifanywe na wizara au taasisi husika kupitia kwa watu wao wa Public Relations/ Marketing. Waombe naombe nafasi ya kuweka tangazo lao kulingina na makubaliano yao na JF.
 
unajiona mzalendo ufala tu kuwa mzalendo kwenye familia yako .akina lissu wazalendo halisi wanapigwa risasi unakuja na viushauri vyako vya kijinga jinga
 
Back
Top Bottom