Jamiiforums is accessible worldwide. Tunawaomba mtusaidie kuitangaza vema Tanzania yetu walau mara moja tu kila mwezi (Tarehe15 au 28)

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Kama umekuwa ukifuatilia threads zangu nyingi za humu jamiiforums nimekuwa nikishauri mbinu mpya na mbadala ambazo zinaweza kutumika katika kuitangaza vema nchi yetu hususan kupitia njia za kwenye mitandao ya kijamii/social media platforms.

Leo ombi langu kubwa lipo kwa uongozi wa jamiiforums ambao kwa heshima na taadhima zote ninawaomba wao pia washiriki katika campaign hii kuitangaza vema nchi yetu walu mara moja tu kwa kila mwezi aidha iwe Tarehe 15 kati kati ya mwezi au Tarehe 28 ya mwisho wa mwezi.

Ninapendekeza, kuwa na tangazo (banner) la kivutio chochote cha utalii baada ya comment/reply ya kwanza ya kila thread au kwenye homepage baada ya hayo maneno "recommended" na "trending"
View attachment 1170064
Ninafahamu fika ya kuwa hii ni biashara and when it comes to business nothing goes for free, ila tunawaomba kwa heshima na taadhima and for the sake of Patriotism, just help us on this.

NB: NSSF naombeni fao langu la mkupuo kwa maana maisha ni magumu sana huku mtaani. Mungu anawaona mjue?

OUR MOTTO
==========
KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YAKO UNAANZA NA WEWE. JIULIZE UMEIFANYIA NINI LA MAANA NCHI YAKO MPAKA LEO HII.
Watangaze nini sasa?
 
Back
Top Bottom