JamiiForums inastahili tuzo, imetusaidia wengi

Sep 10, 2013
335
471
Namshukuru Mungu kwa kuniunganisha na familia hii kubwa, nawashukuru sana wanafamilia wa mtandao huu na zaidi sana waasisi wake.

Hivi majuzi nimepokea zawadi kutoka Marekani kupitia kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA(BAWACHA) na Mbunge wa viti maalumu Suzanne Lyimo.

Alipokuwa kule alikutana na watu waliomuuliza kama ananifahamu, walimpa dola kadhaa, wakaahidi kunisaidia zaidi siku za usoni. Zaidi sana wamenitumia video camera ambayo nitaipokea kesho kutwa. Walinifahamu kupitia JamiiForums.

Kule Norway kuna kijana wa kitanzania ambaye amekuwa akifuatilia tunachofanya huku, mwaka jana alijitolea kulipa ada ya dogo (mwanangu) mpaka amalize darasa la saba, kwa mwaka ni sh.1.7 million.

Zaidi sana kaandika kijitabu kinachohusu harakati zangu chenye title "HARAKATI NA MAWAZO YA KAMANDA MAWAZO".

Kijitabu hiki kinasisimua sana,hata kama ningekiandika mwenyewe nisingekiandika kwa umaridadi mkubwa kiasi hicho.

Nakushukuru sana Andrew.

Ninapotazama nilikotoka na mbio hizi za kisiasa kuna ka umbali kakubwa. Nimejikwaa mara kadhaa, nimewakanyaga wasafiri wenzangu kwa bahati mbaya, kuna wakati flani nilidondoka, ni nyie hao hao marafiki zangu mlioniambia niinuke, nijifute vumbi na nisonge mbele.

Kuna wakati tunatofautiana kimtazamo wa namna ya kuijenga nchi yetu, Tunachachafyana, hitilafiana, zogoana na wakati mwingine lugha zetu zinakuwa Kali kiasi, nawaambieni ukweli vitu vyote hivyo ndo vinatukomaza, vinatukuza na ndiyo maana halisi ya family.

Kwa vile hatujui siku wala saa ya kutoka duniani hapa, leo Shehe mkuu katutangulia mbele ya haki, hatujui kesho ni zamu ya nani! Tusameheane.

Lengo letu kuu liwe moja, kuiona au kuiacha nchi yetu ikiwa sehemu salama ya kuishi, tuache misingi imara kwa wanetu, wabishane lakini wasipigane au kuuana, watofautiane lakini wasiigawe nchi.

Asanteni marafiki, asante JamiiForums.

Jioni njema
 
Vuta picha siku moja JF ikafungiwa kwa muda usiojulikana labda kutokana na sheria mpya ya makosa mtandaoni. Utajisikiaje?

Binafsi nitajisikia vibaya sana kwani JF imenikuza sana kifikra na nimejua mengi kupitia JF hili ndilo jukwaa bora kwangu kwani mitandao mingine huwa nafataga habari za michezo tu.

Natamani siku moja JF waanzishe gazeti kuwasaidia na wananchi wasio kuwa na uelewa na mtandao huu hasa wa vijijini
 
Mkuu,

JF inabadili mtazamo wa mtu negatively to postively.

Hasa mimi nimejikuta nakuwa na uwezo wa kujingea hoja na kuisimamia...

Thanks JF
 
WanaJF,

JF hiki ni chuo tosha.

Mimi binafsi JF imenisomesha mengi na imenijulisha kwa wengi ndugu zangu ambao tumefanya mijadala mingi ingawa wakati mwingine watu huchukuliwa na hamasa na kukwaruzana lakini mwisho wa siku tunarudi kwenye mstari.

Hakika JF inastahahili tuzo kwa elimu inayotoa kwa jamii.
 
Serious!

Hata mimi pia siyo muumini wa mitandao mingine kama facebook n.k zaidi nisipoingia humu JF huwa nahisi kupitwa na mengi!

JF imetuelimisha mengi kwa uhuru mkubwa kushea mawazo yetu hapa! Kilichonivutia zaidi hakuna mizengwe mingi ya kujiunga na kushea mawazo yako kwa uhuru kama ilivyo kwingine!

Ahsante JF
 
Vuta picha siku moja JF ikafungiwa kwa muda usiojulikana labda kutokana na sheria mpya ya makosa mtandaoni. Utajisikiaje?

Binafsi nitajisikia vibaya sana kwani JF imenikuza sana kifikra na nimejua mengi kupitia JF hili ndilo jukwaa bora kwangu kwani mitandao mingine huwa nafataga habari za michezo tu.

Natamani siku moja JF waanzishe gazeti kuwasaidia na wananchi wasio kuwa na uelewa na mtandao huu hasa wa vijijini
Ikifungwa JF lazima tuandamane. Mimi najiuliza kwanini nimechelewa kuifahamu.

Yaaani, we acha tu... JF ni kila kitu
 
Hakika JF ni kiisima cha maarifa.

Binafsi nimeanza kusumbuliwa na matatizo ya macho kwa kutumia muda mwingi kuperuzi JF, na kwa kweli siwezi kuvumilia kutoingia humu kwa kipindi kirefu.
 
Kuna wakati tunatofautiana kimtazamo wa namna ya kuijenga nchi yetu, Tunachachafyana, hitilafiana, zogoana na wakati mwingine lugha zetu zinakuwa Kali kiasi, nawaambieni ukweli vitu vyote hivyo ndo vinatukomaza, vinatukuza na ndiyo maana halisi ya family.

Kwa vile hatujui siku wala saa ya kutoka duniani hapa, leo Shehe mkuu katutangulia mbele ya haki, hatujui kesho ni zamu ya nani! Tusameheane.

Lengo letu kuu liwe moja, kuiona au kuiacha nchi yetu ikiwa sehemu salama ya kuishi, tuache misingi imara kwa wanetu, wabishane lakini wasipigane au kuuana, watofautiane lakini wasiigawe nchi.

Asanteni marafiki, asante JamiiForums.

Jioni njema

Nilitaka niandike Kama wewe, lakin hii shukrani yako imeniwakilisha saana.

JF imenifanye kulipenda taifa langu kuliko chama.

Nimelelewa katika familia ya CCM na mzee wangu alikuwa amenijengea mentality ya kuchagua viongozi kimazoea.

Sasa wana JF wamenijenga Sana na Nina sema nimekuwa nikiwajenga watu wengi wa mtaani about our nation...

JF ni familia kubwa na ukiitumia vzr ni zaidi ya leadership college.

Thanks JF.
 
Back
Top Bottom