Jamiiforums Impact: Ndugu Bakari Jabiri na Serikali wasalim amri

FISADI

Member
Dec 29, 2015
35
13
Haya ndio mambo ninayotaka kuyaona. Siku 3 zilizopita nialianzisha uzi na kulalamika kuhusu utendaji wa kazi wa Wakala wa Mawasiliano wa Serikali kilicho chini Ndugu Bakari Jabiri.

Malalamiko yangu yalilenga kuonyesha jinsi gani serikali ya Magufuli ilivyo lege lege kwenye :

TRANSPARENCY -malalamiko mengi ya wananchi yanatokana na wananchi kutojuzwa au kutopewa taarifa sahihi za kinachoendelea kwenye idara za serikali kama vile ardhi, Brela, Mahakama, sheria, maelezo, na kweingineko. Hapa nazungumzia sio kutoa taarifa za tenda bali miswada (ambayo ilitakiwa iwe kwa kiswahili, planning applications, planning permissions, zoning, ulinzi na usalama, etc.

MAWASILIANO -wafanyakazi wa serikali wamekuwa wakitoa private emails zao za yahoo na hotmail na wanatoa kisingizio kuwa email za kikazi hawazipati au ngumu kuzitazama. Hii ni moja ya njia kuu za urasimu

TOVUTI ZISIKWENDA NA NYAKATI-Nililalamika kuwa serikali na watu wake hawa update websites zao on regular basis. Rightly or wrongly, nilimlaumu Jabiri na kama hahusiki na hili alitakiwa afanye initiative na kutoa tangazo kwa kutumia mgongo wa #hapanikazituu halafu naamini kila idara watafuata maamrisho yake kuwa lazima taarifa ziwe streamlined.

URASIMU WA BRELA: Hii nayo niliazishia uzi na nitaendelea kufuatilia. Malalamiko yangu ni kuwa BRELA ukiingia kwenye website ya BRELA kufanya simple search ya jina la kampuni unaambiwa kuwa huwezi kupata hizo taarifa mpaka ujiandikishe na utoe taarifa zako nyeti kama vile tarehe ya kuzaliwa, ulipozaliwa, kama umeoa au huajaoa, unakoishi na kadhalika. Hii naamini ni urasimu usio na maana kwa sababu search ya kampuni na kujua imesajiliwa lini na shareholding yake ziwe ni taarifa ambazo ni free online kwenye website yao. LAKINI kama unataka kufanya returns,kutaka kusajili kampuni online na kubadili jina la kampuni yako then hapo lazima ujisajili kisha utapaewa namba maalum ya kukuwezesha kufanya hayo mfano huu hapa:

NYS Division of Corporations, State Records and UCC


MATOKEO YAKE:


SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUA PEPE ZA KAWAIDA KATIKA MAWASILIANO YAKE



Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.

Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es salaam.

Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) akitembelea maeneo mbalimbali ya Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao leo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.




Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benjamin Dotto akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam.


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam.




Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza na Watendaji na baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao.


Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini.

“Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu” Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali.

Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano.

“Katika hili ninatoa siku 60 muhakikishe kuwa mnakamilisha kwa Taasisi zilizobaki ili kwa wale watakaopuuzia hatua zianze kuchukuliwa” Ameeleza Mhe. Angella.

Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa Wakala hiyo kuweka mpango wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa kitaaluma watumishi waliopo kazini kwa kujenga utaratibu wa kuwarithisha uzoefu watumishi ili kuendelea kuimarisha ufanisi na utendaji wa Wakala hiyo.

Mhe. Kairuki amewataka kuwa wabunifu katika kuanzisha mifumo mipya ya TEHAMA ili kuimarisha dhana ya Serikali mtandao ili kupunguza gharama hadi kufikia asilimia 5 ya fedha zinazotumika kuendeshea masuala mbalimbali ambayo yangefanywa kupitia matumizi ya TEHAMA.

Akizungumzia kuhusu ununuzi wa vifaa vya TEHAMA serikalini ameitaka Wakala hiyo kutoa ushauri ili kudhibiti mianya ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha katika kununulia vifaa hivyo kwa gharama kubwa wakati vinaweza kupatikana kwa bei ya kawaida.

“katika hili Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika katika upotevu wa mapato muhakikise mnazisaidia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika masuala ya ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili mifumo inayonunuliwa iwe na manufaa kwa wananchi na thamani halisi ya fedha”

Amesema Serikali itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kupitia mtandao ili wananchi waweze kupata huduma hizo mahali walipo kwa gharama nafuu na kutoa wito kwa watumishi wa Wakala ya Serikali mtandao (e-Gov) kuwa wabunifu katika kutengeneza programu mbalimbali na mifumo salama itakayowasaidia wananchi kupata huduma.

Aidha, katika hatua nyingine ameitaka e-Gov kuendelelea kujenga uwezo katika kudhibiti dharura na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika matumizi ya TEHAMA na kuitaka Wakala hiyo iendelee kulifanyia kazi suala la kuwezesha mifumo ya Serikali kuzungumza kati ya taasisi moja hadi nyingine ili huduma zote ziweze kupatikana katika eneo moja na kuondoa urudufu wa mifumo iliyopo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Gov) Dkt. Jabiri Bakari akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala hiyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali toka kuanzishwa kwake Julai 11, 2012 imeendelea kupata ufanisi katika uimarishaji wa Serikali Mtandao.

Amesema kuwa Wakala hiyo inaendelea kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinawafikia wananchi kupitia mtandao mahali walipo na kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo la huduma zote za Serikali kupatikana chini ya dirisha moja.

Aidha amesema kuwa Wakala ya Serikali Mtandao itaendelea kuhakikisha kuwa usimamizi wa viwango vya matumizi ya TEHAMA katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali vinazingatiwa.

MICHUZI BLOG: SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUA PEPE ZA KAWAIDA KATIKA MAWASILIANO YAKE
 
Good job! Tuendelee kuwaonyesha mapungufu yao ili wafanye kazi
 
Inawezekana ikawa ni coincidence tu.

Kwenda egovt ilikuwa kwenye plan ya Kairuki.
 
hata ndalaichako alipigiwa debe na jf
ni ukweli usiopingika hapa jf kuna mambo mengi mazuri yanayojadiliwa na ambayo watendaj wanapoyasikia huyafanyia kazi.

good job jf
 
JF ina impact kubwa sana sana kwa wananchi na taifa. mapinduzi mengi ya kiuchumi na kisiasa hapa nchini kwetu yamepitia medium ya jf. ni jambo la kuwapongeza sana wamiliki wa mtandao huu.
 
..kuna jamaa anaitwa @Game Theory nadhani suala hili alilipigia kelele wakati wa utawala wa JK, lakini wahusika wakaweka pamba masikioni.
 
Serikali inashindwaje kuwa na active websites za idara na taasisi zake huku watu wameajiriwa kufanya kazi hizo? Ndio ule uzembe wetu na uvivu tuliouzoea
 
Ni aibu sana kuja kufundishwa kazi yako na waziri. Hata ubunifu wa kufanya kazi umetutoka sasa, tumekuwa wabunifu wa kuiba hela za wananchi tu.
 
Whaaat? Yaani hii Taasisi ilianzishwa July, 2012 then haina tangible deliverables mpaka leo? 4 years down the line, kweli? Huyu Jabiri naye ni jipu.
 
Whaaat? Yaani hii Taasisi ilianzishwa July, 2012 then haina tangible deliverables mpaka leo? 4 years down the line, kweli? Huyu Jabiri naye ni jipu.

Labda hakupewa adidu za rejea? Na kumbuka utawala uliopita Kila mmoja alikuwa ni king wa eneo lake
 
Last edited:
Back
Top Bottom