JamiiForums ilivyotimiza ndoto za viongozi wengi na shukrani ya mateke kama fadhila

paliemba

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
445
212
Habari ya sikukuu wadau na wasalimu kwa jina la yule aliyeziumba Mbingu na nchi.

Nakumbuka mimi nimekuwa memba wa JamiiForums tokea mwaka 2006 wakati ule tulipokuwa tuna pata internet kwa njia ya desk top, sisi wengine tulikuwa mpaka tuingie internet cafe na kulipa shilingi 1,000 kwa nusu saa kwani simu kali enzi hizo ilikuwa motorola L6.

Nimesema nikikuwa mwanachama mwaminifu saana kwani kila nilipo ingia internet kwa ilikuwa ni lazima nichungulie walau dakika NNE tu. Najua wengi wata uliza mbona ID yangu inaonekana ni mpya? Kwa kweli ni mpya kwasababu mimi nimekuwa mwanachama mwaminifu nje ya jukwaa nadhani kwa kusema hivo nimeeleweka.

SASA TWENDE KATIKA MADA HUSIKA:

Kama mada inavyo someka na nilivyo jaribu kuelezea walau kiufupi, nikweli kabisa kwamba katika kipindi cha uchaguzi na hasa baada ya uchaguzi nilikuwa nikitumia muda mwingi kufuatilia mijadala na hoja mbalili zilizo kuwa zikiendelea hapa JamiiForums kwani kwa kipindi chote nilichokuwa mwanachama nje ya jukwaa nilikuwa nimejiridhisha sana kwamba taarifa nyingi zilizokuwa zikitolewa humu JamiiForums kwa kiasi kikubwa zilikuwa na ukweli ingawaje sio zote.

Baada ya uchaguzi sisi wengine ambao tunaishi maeneo ya huku sindelela kwa bibi yake Alikiba walau tulikuwa tunapisha macho humu JamiiForums ili kufahamu matokeo mabalimbali kote nchini.

Lakini kitu ambacho niligundua ni kwamba kulikuwa na mchezo mchafu ulio fanywa na baadhi ya watu humu JamiiForums kwa kujifanya kupendekeza majina ya watu wanaoamini kwamba kama wangeteuliwa wangalifaa au kama si kufiti kabisa katika baraza la mawaziri katika serikali hii ya hapa kazi tu.

Kitu kilicho kuja kunistua zaidi ni pale nilipokuja kuona takribani 70% ya mawaziri pamoja na nafasi zao za uteuzi zimeakisi hoja na maoni ya kuhusu mapendekezo ya wanajamii forum wengi.

Kiukweli nilishindwa kupata jibu la haraka kuhusu hali hiyo. Kama kweli mheshiwa rais wetu alipitisha jicho huku JamiiForums na akaona kwamba pengine si vibaya kujaribu kuisikiliza na maoni ya watanzania wengine wanapendekeza nini na kisha akayafanya kama sehemu ya maamuzi je muheshiwa alikosea?

Na kama jibu hakukosea je miongoni mwa wateule waonadhani JamiiForums ni kichaka cha uhalifu na kwamba tupigilie misumari ya kichwa hii ndio fadhila stahiki kwa jukwaa lenye manufaa kwao kama hili?

Kiukweli imenifanya nikumbuke mengi yalio kuwa yakitokea kabla na hata baada ya uchaguzi. Mungu ibariki Tanzania watie hekima wanao tuongoza kwa manufaa ya mama TANZANIA.

Hongera saana JamiiForums kisima cha fikra pevu na mahali pekee pa kujifunza mambo mbalimbali ya kidunia.

Hongereni sana waasisi wote wa JamiiForums.

Wenu kapuku PALIEMBA.
 
Nimesoma mpaka mwisho nikajua ungewataja!! But oooops!!
Mkuu labda umeingia humu kwa malengo maalumu lakini kama ulikuwa mwachama mwaminifu humu hiyo oooooops ungempa shemeji awapikie watoto asubuhi.
 
1482864265947.jpg
 
Back
Top Bottom