Theb
JF-Expert Member
- Jan 25, 2019
- 3,929
- 7,268
Habara za siku wa ndugu..?
Napenda kuwapa haka kaandiko tena tujifunze kidogo kupitia maendeleo ya wenzetu wa bara ulaya. Andiko hili litaangazia baadhi ya mapinduzi yaliyotekelezeka kule ulaya na yakawapa maendeleo waliyoyafikia ambayo sote tuna ya husudu. Baadhi ya mapinduzi hayo ni kama mapinduzi ya kwenye kilimo, mapinduzi kwenye mfumo wa utawala, teknolojia na viwanda.
Mapinduzi katika kilimo
Mnamo karne ya 17 kuendelea mpaka karne ya 19 barani ulaya walifanya mapinduzi makubwa kwenye kilimo.
Mfano. Waliboresha baadhi ya mbegu. Waliboresha mfumo wa umwagiliaji mashambani na waliweza kuachana na mifumo ya uzalishaji wa kizamani kwa ujumla na kuanza kuzalisha kwa kutumia zana za kisasa.
Mapinduzi katika viwanda.
Hapa pia watu wa bara ulaya walifanikiwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye viwanda. Mnaomo karne ya 18 ilianzia Wingereza na kusambaa mataifa mengine. Kwenye viwanda walifanya maboresho yafuatayo. Matumizi ya mashine zilizoboreshwa zaidi viwandani, mfumo wa wafanyakazi ukabadilishwa ikawa na kuzingatia ujuzi wa mtu na zingine matumizi ya umeme kwenye uzalishaji pamoja na makaa ya mawe viwandani kuendesha mashine yakatejelezeka.
Mapinduzi katika sayansi na teknolojia
Pia waliweza kufanya mapinduzi kwenye sayansi na teknolojia. Mfano walianza kuboresha huduma za mawasiliano na kutengeneza magari, mashine, na vitu vingine
Mapinduzi katika mfumo wa utawala.
Barani ulaya pia walifanikiwa kufanya mapinduzi ya kimfumo kwenye utawala. Waliachana na mfumo wa kidikteta kwa baadhi ya mataifa na kuanza mfumo wa kidemokrasia. Hapa tunaona mfano french revolution nakadhalika.
Faida za mapinduzi hayo ambazo zinafanania na sababu za kuleta maendeleo kwenye jamii yoyote ile
(i). Miundombinu bora yenye ufanisi na kuwezesha shughuli za mawasiliano na usafirishaji.
Hapa tunaangazia barabara, usafiri wa anga, njia za reli, usafirishaji wa majini na mawasiliano kwa ujumla. Hivi vyote hurahisisha shuhuli za uzalishaji na kuchochea maendeleo
(ii). Uongozi bora katika jamii.
Ili jamii yoyote ipate maendeleo lazima iwe na viongozi bora wenye kutambua na kuongoza vema taifa au jamii na kusimamia maslahi na utekelezaji wa miradi na huduma za kimaendeleo.
Mfano viongozi lazima wawe na sifa zoote za kiongozi bora, wasiwe wala rushwa, wawe wavumilivu na waaminifu, wazalendo na wawajibikaji.
(iii). Elimu bora yenye kutuletea wataalamu mbalimbali.
Pia taifa lolote ili lipate maendeleo lazima liwe na mfumo bora wa elimu itakayo saidia kuzalisha au kutengeneza wataalamu wa idara zote. Hapa mfano wahandisi, waalimu, watu wa afya, mafundi, wanasayansi, wataalamu katika kilimo, wataalanu katika michozo na burudani nakadhalika. Yote hii itarahisisha kupata nguvu kazi kutoka kwa watu wa taifa husika.
(iv). Idadi ya watu iongezeke.
Pia lazima tuwe na idadi kubwa ya watu ambao hao ndio nguvu kazi ya taifa letu. Hivyo hasi lazima tuboreshe huduma za kiafya, elimu za uzazi ili kupunguza idadi kubwa ya wanaofariki. Hii itasaidia pia kupata soko la ndani katika uzalishaji wa mazao na bidhaa za viwandani.
(v). Matumizi sahihi na bora ya rasilimali tulizonazo.
Pia ili tupate kupiga hatua kimaendeleo lazima tuzitumie rasilimali zetu kwa manufaa ya taifa kwa ubora na usahihi utakao tupatia maendeleo. Mfano wa rasilimali zetu nchini ni madini, makaa ya mawe, mafuta kama yakigundulika, milima moja wapo mlima Kilimanjaro na aridhi pia tuliyonayo.
(vi). Hali ya hewa iliyopo nchini.
Nchi yetu imebahatika kupata kuwa na aina tofauti za hali ya hewa mfano kuna ukanda unakua na baridi, joto na hali ya kawaida. Hii husaidia ustawishaji wa mazao tofauti tofauti nchini yatakayo saidia kukuza kilimo na biashara.
(vii). Sayansi na teknolojia itumike katika shughuli zote za uzalishaji. Mfano uboreshaji wa mbegu na zana za kilimo , viwandani pia.
Yafuatayo ni mambo yanayokuwa kikwazo katika maendeleo ya jamii yoyote ile.
(i). Ubaguzi uwe wa kijinsia, kidini kikabila au kimaeneo.
(ii). Uongozi mbovu au usimamizi mbovu.
(iii). Kukosa wataalamu wa ndani na kutegemea wataalamu wa nje tu.
(iv). Miundo mbinu mibovu
(v). Kutokubali mawaza mbadala. Hususani kwa viongozi wetu miaka nenda suala la kukosoana lina onekana ni uadui. Hatuwezi kuwa bora bila kukosoana na kuongezeana fikra tofauti tofautim
(vi). Kutokujali haki za binadamu. Hili nalo ni.tatizo hususani nchi zetu za Afrika watawala wengi hawajali haki za raia wao kitu kinachopelekea wawekezaji kuogopa kuwekeza na kutilia mashaka juu ya usalama wao.
(vii). Kukosa viongozi wenye maono katika kuliendeleza taifa. Taifa lolote lazima liwe na viongozi wenye maono kimaendeleo. Mwl Nyerere aliwahi kusema tuna maadui wa kubwa watatu ambao ni umaskini, ujinga, na maradhi bado nchi yetu haijawa na huduma bora jambo.linaloongeza umasini.
Hitimisho.
Nimeonesha kwa uchache mapinduzi yaliyotokea barani ulaya ambayo yamepelekea wao kupiga hatua kimaendeleo katika jamii zao. Hivyo hasi jamii zetu za bara la Afrika hatuna budi kutekeleza mapinduzi hayo hususana kwenye, kilimo nchini, mfumo wa kuongoza nchi zetu, mifumo ya elimu zetu, sayansi na teknolojia na mapinduzi ya viwanda. Asilimia kubwa ya bishaa tunazotumia nchini huzalishwa mataifa ya ughaibuni hilo liangaliwe kwa upana bila kujali maslahi ya watu wachache au kikundi fulani.
Yapo mengi ila hapa nimetoa kidogo ya yale mengi