Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,427
Jamii hii ya Shona ilikuja Kenya mwaka wa 1959 kama missionaries yaani watu wanaoeneza injili. Sasa wameishi Kenya bila uraia kwa miaka 62 na hivi leo wamepata uraia kamili na hata kupata vitambulisho. Hii inafuatia Jamii la Wamakonde kutokea Msumbiji waliopata uraia huo miaka michache iliyopita. Ni vizuri wamepata vitambulisho maana hapa Kenya kitambulisho ndicho kila kitu. Huwezi hata kutumia Mpesa bila kitambulisho.