Jamii ya leo: Eti mtoto wa masikini ndio anatakiwa kusoma

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,565
2,000
Jamii ya leo imejijengea imani kwamba njia pekee ya mtoto wa familia maskini kutusua katika maisha ni kusoma na kupata elimu zaidi.

Huku wakiamini watoto wa familia zenye uwezo wao wana njia mbadala za kutusua si lazima waende shule

Hata wazazi utawasikia wakisema mwanetu "soma kwa bidii baba uje utusaidie"

Mtoto huyu aliyetokea katika familia maskini atajijengea hofu na pressure katika akili kuhusu lengo lake katika kusoma na siku zote hatayafurahia maisha yake kwasababu atajiweka busy muda wote kwa ajili ya kutimiza matwaka ya wazazi wake

Mtoto anapewa jukumu kubwa na lengo lake na akili yake ikiwa ni kwamba nasoma ili nipate maisha mazuri baadae. Anakuwa na msongo katika usomaji wake hata akili yake hushindwa kutulia.

Imani ya jamii ya Leo kwa watoto matajiri ni kwamba wao hata wasiposoma kwa bidii wazazi wao wana kipato kikubwa hawahitaji elimu.

Na ndio maana watoto wa kitajiri husoma for leisure and pleasure wakituliza akili zao na kufurahia maisha yao ya shule kwasababu wazazi wao hawakuwabebesha majukumu ya kusoma kwa ajili ya familia.
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,575
2,000
Ngumu sana hii mada ku comment, ukizingatia kweli kuna wengine tumetoka kwa wazazi wachovu, na ni elimu ndo at least imetufungulia njia ya maisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom