Jamii ya Kimataifa yalaani veto ya Marekani dhidi ya matakwa ya walimwengu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamii ya Kimataifa yalaani veto ya Marekani dhidi ya matakwa ya walimwengu

Discussion in 'International Forum' started by abdulahsaf, Feb 20, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamii ya Kimataifa yalaani veto ya Marekani dhidi ya matakwa ya walimwengu [​IMG]Hatua ya utawala wa Rais Obama wa Marekani ya kupiga kura ya veto dhidi ya muswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililoungwa mkono na nchi 14 wanachama wa baraza hilo kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina imeutikisa tena ulimwengu na kufuatiwa na laana chungu nzima.
  Ijumaa ya jana tarehe 18 Februari Marekani ilipiga kura hiyo ya veto dhidi ya maamuzi ya jamii nzima ya kimataifa ya kupinga ujenzi wa nyumba za walowezi wa Kiyahudi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kama kawaida ikaushajiisha zaidi utawala ghasibu wa Israel kudumisha ujenzi huo.
  Nchi 14 wanachama wa Baraza la Usalama hata waitifaki wakubwa wa Marekani na Israel yenyewe zimeunga mkono azimio hilo kutokana na unyama na uovu wa utawala wa Tel Aviv. Hata hivyo uamuzi huo umekumbana na kura dhalimu ya veto ya Marekani.
  Hatua hiyo ya viongozi wa White House imepingwa si na nchi za Kiislamu na Kiarabu pekee bali jamii nzima ya kimataifa.
  Siasa za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina zimekuwa zikitekelezwa kwa miaka mingi na viongozi magaidi wa Israel. Mwaka 1967 wakati wa vita vya siku sita, utawala wa kigaidi wa Israel ulikalia kwa mabavu eneo la Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan, Ukanda wa Gaza na Baitul Muqaddas Mashariki na kuanza kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo hayo.
  Ujenzi huo wa vitongozi vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina umeambatana na kuporwa ardhi na mashamba ya Wapalestina na kulazimishwa wananchi hao kuwa wakimbizi katika maeneo mengine. Katika kipindi chote cha miongo minne iliyopita utawala haramu wa Israel umekuwa ukitekeleza siasa za kuvuruga muundo wa kijamii na kijografia wa ardhi za Palestina kwa maslahi ya Wayahudi.
  Nukta ya kutiliwa maanani hapa ni kuwa wakati utawala haramu wa Israel ulipoghusubu ardhi za Palestina mwaka 1967, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio nambari 242 ambalo ni miongoni mwa nyaraka muhimu mno za kihistoria za baraza hilo. Azimio hilo linaitaka Israel iondoke katika ardhi za Palestina bila masharti yoyote. Tangu wakati huo hadi hii leo, Baraza la Usalama na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa yamepasisha maazimio mengi yanayolaani ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ambayo yamewekwa kwenye hifadhi za nyaraka za kale na kupuuzwa kutokana na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo ghasibu. Kwa miongo kadhaa sasa Marekani imekuwa ikipiga kura ya veto kukwamisha maamuzi yote muhimu ya jamii ya kimataifa yanayoulamu utawala wa Kizayuni wa Israel au kulaani ukatili na jinai za utawala huo dhidi ya wananchi wa Palestina.
  Kura ya sasa ya veto ya Marekani dhidi ya maamuzi ya kimataifa na ya kibinadamu yanayotetea taifa lilalodhulumiwa na kukandamizwa la Palestina imezidi kuweka wazi unafiki wa kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Barack Obama aliyewadanyanya walimwengu kwamba amekuja kusahihisha makosa ya huko nyuma ya siasa za Marekani ya kutetea domokrasia, uhuru na haki za binadamu.
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Si ajabu kwangu kuona marekani ikipiga veto kuzuia azimio lolote lenye maslahi na Israel, ikumbukwe hatua alizozifikia Yitzhak Rabin na Yasser Arafat miaka ya 90 ambapo PM huyo wa Israel aliuawa. Napata dhana kwamba hali ya mashariki ya kati huenda ikaja kuamuliwa kwa vita kali na mbaya maana dialogue zote za mediation huishia KUZUIWA kwa kura za veto, hii si haki kwani Palestinians are always sufferring at their own home.
  Na si ajabu kuona Marekani ikitumia turufu yake katika eneo lenye maslahi yake pia, haijalishi ni nani aliye madarakani awe ni Democrats au Republican lengo lao ni moja tu. Tusahau kidogo amani ya hapo Gaza strips na west bank kwa sasa.
   
 3. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Magaidi wakubwa wote.viva israel .
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  ukitaka kuwa Rais wa marekani lazima ule kiapo mbele ya wazee wa kiyunani kwenye misitu ya anakonda kwamba utailinda na kuitetea israil na uzayoni kwa gharama yoyote.kwa hiyo waislamu msitegemee chochote cha maana kutoka kwa ndugu yeniu baraka huseni obama.
   
Loading...