Jamii na mapambano dhidi ya janga la ukimwi tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamii na mapambano dhidi ya janga la ukimwi tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hengo, Mar 19, 2012.

 1. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtanzania na ninawajibika kwa nchi yangu kama inavyostahhili kwa raia mzalendo yoyote katika nchi yake ikiwa ni pamoja na kulipa kodi na kuheshimu sheria zote za nchi.kwa sababu hiyo napenda kuchukua nafasi hii kutumia haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa mawazo yangu.Tafadhali niacheni niseme, msinizibe mdomo.

  Napenda nitoe maoni yangu juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali katika harakati ya kupambana na janga la ukimwi, yeyeyote mwenye macho atakubaliana nami kuwa serikali imepiga hautua kubwa katika hilo.Mfano kampeni za kuhamasisha kupima nchi nzima,utoajia wa dawa za IRV kwa waathirika nchi nzima,elimu kwa umma kuanzia mashuleni juu ya gonjwa hatari la ukimwi na uhamasisahji wa matumizi ya mipira ya kiume wakati wa kujamiana,kwa dhati kabisa naipongeza serikali kwa jitihada hizo nyingi na nyinginezo.

  Aidha napenda kutoa wasiwasi wangu juu ya utayari wa jamii yenyewe kupambana na janga hili, wasiwasi wangu umekuja baada ya kushuhudia kushamiri kwa biashara haramu ya ngono katika maeneo mbalimali ya nchi, hasa mijini hususani Dar es salaam,mwanza,Arusha na Dodoma.Je, jamii tunalichukuliaje swala hili?Napenda niyataje maeneo machache yanayoongoza kwa biashara hizo,kwa mkoa wa Dar es salaam ni Buguruni,Temeke juu,keko n.k.Dodoma ni katika maeneo ya Dodoma inn,Uhindini katika nyumba ya kulala wageni ya TANZANIA GESTI,Airport, chang`ombe na Chaduru hasa katika virabu vya pombe vya kienyeji vijulikanavyo kwa jina la mabasi mawili.(Naomba mtaje maeneo mengine yanayo onekena kuwa kero kwa hili)

  Hii inadhirisha wazi kuwa wamiliki wa nyumba wanaopangisha wanawake/akinadada wanaojiuza, wanaenda kinyume na harakati za serikali za kuzuia maambukizi na kuenea kwa ugonjwa huo hatari.

  Aidha nimeshuhudia mara kadhaa jitihada za jeshi la polisi kuwakamata machangudoa na kuwafikisha mahakamani, hata hivyo jitihada hizo zina ishia ukingoni kutoka na kutokuwepo kwa sheria ya kuwabana wanaohusika na biashara hiyo pia.

  MAPENDEKEZO:
  1. Napendekeza kutungwa kwa sheria kali itakayowezesha kukamatwa na kuadhibiwa kwa wanaofanya biashara hii na wanaosaidia kufanyika kwa biashara hii.Mfano wanaopangisha vyumba kwa biashara hizo.
  2. Manispaa za miji kuratibu virabu vyote vya pombe za kienyeji kwa kutenga maeneo maalum na kuweka utaratibu wa kukaguliwa ili kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanatumika kwa kuuzia pombe tu na sivinginevyo
  3. Elimu zaidi endelee kutolewa mashuleni na katika jamii juu ya gonjwa hili hatari
  4. Kuwepo kwa mamlaka maalimu ya kuzuai mambukizi ya UKIMWI
  5. kuongeza vituo vya kutolea dawa kwa waathirika pamoja
  Aidha napendkeza jamii tuonyeshe nia ya dhati ya kupambana na gonjwa hili,taifa linaangamia.
   
Loading...