JAMII LEO episode: Hongereni sana JamiiForums

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,975
Kwanza kabisa nianze kwa kuwasalimu wana JF wote, wakubwa kwa wadogo, wakongwe na wageni, wachangiao mada na wasio changia, na wengi wote kwa ujumla. Nimatumani yangu muu wazima kabisa.

Rejea kichwa cha Uzi huu, napenda kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa uongozi mzima wa JamiiForums kwa kutuletea hili wazo jipya la JAMII LEO episode.

Huenda labda JAMII LEO episode leo episodes imeanzishwa kitambo kidogo, lakini kwa upande wangu nimeifahamu leo hii nilipokuwa katika pita pita zangu YouTube nikakutana na hizi episodes ambazo ni mada halisi zilizoandikwa na na kuchangiwa na wana JF ambapo mtangazaji huchagua mada mojawapo makini na kuichambua, huku akimtaja mleta mada na kuzisoma comments na majina ya wachangiaji wa uzi huo.

Kusema ukweli nimefurahishwa sana na huo ubunifu, na naamini ipo siku mtaanzisha tv au radio stesheni yenu na kuufanya mtandao wetu pendwa wa JamiiForums kupasua anga zaidi.

Keep it up JamiiForums.
 
Back
Top Bottom