Jamii kuchanganya kati ya kampeni za uchaguzi na kufanya mikutano ya kisiasa

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
114
174
kampeni za uchaguzi ni njia ya mgombea wa kiti cha urais, ubunge na udiwani au chama chake au wakala wake kuwasiliana na wapiga kura na kuwaeleza sera zake kwa ajili ya kuomba ridhaa yao ya kuchaguliwa kuwawakilisha.

Kama hiyo haitoshi tuliona kuwa utaratibu wa kampeni za wagombea urais, ubunge na udiwani, unakitaka kila chama cha siasa au mgombea kabla ya kuanza kampeni, kuandaa mapendekezo ya ratiba ya kampeni na kuiwasilisha kwenye ngazi husika inayosimamia na kuratibu kampeni.

Mapendekezo ya ratiba hiyo yataonyesha tarehe, muda na mahali mikutano ya kampeni itakapofanyika na msimamizi anayehusika baada ya kupokea mapendekezo hayo, ataitisha kikao cha vyama vyote vya siasa vyenye wagombea kupitia na kukubaliana kwa pamoja kuhusu mapendekezo ya ratiba ambayo itatumika katika kampeni.

Hata hivyo, imeibuka sintofahamu katika miezi ya hivi karibuni inayotokana na baadhi ya vyama vya siasa kushindwa kutofautisha kati ya mikutano ya kampeni za uchaguzi na kufanya mikusanyiko au mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Kifungu cha 53 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, kinaeleza kuwa “kwa kuondoa shaka na bila ya kujali masharti ya kifungu cha 40 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, Sura ya 322 na kifungu cha 11 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1993, tangazo la kampeni litachukuliwa kuwa ni kibali kwa wagombea wa vyama vya siasa vinavyowadhamini wagombea hao kuitisha na kuhutubia mikutano ya hadhara kwa madhumuni yaliyoelezwa katika aya ya (b) ya kifungu kidogo cha (1).”

Aya hiyo ya (b) ya kifungu kidogo cha (1) inasema “Mgombea yeyote au mtu yeyote kwa ridhaa au idhini ya mgombea au chama cha siasa kilichomdhamini mgombea, anaweza kuitisha au kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata hiyo kwa madhumuni ya kushawishi kuchaguliwa kwa mgombea au kuendesha kampeni ya hadhara au ya nyumba kwa nyumba”.

Hata hivyo, Tume imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi na wanasiasa ambao wamekuwa wakichanganya kati ya kampeni za uchaguzi na kufanya mikutano ya kisiasa, ambayo Serikali imeisitisha ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.

Kwa kuwa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Siha na Kinondoni na udiwani katika kata 10 za Tanzania Bara, zimeanza siku chache zilizopita, tumelazimika kufafanua kwa undani suala hilo.

Kifungu cha 40 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, Sura ya 322 kilichotajwa katika kifungu cha 53 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kinabainisha mamlaka iliyopewa Jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko au maandamano.

“Itakuwa halali kisheria kwa Jeshi la Polisi…, pale ambapo askari polisi msimamizi anaona inafaa kufanya hivyo kwa manufaa ya umma;...kutoa amri na kuzuia au kuweka kizuizi katika barabara za umma,…au kufanyika kwa mikusanyiko au maandamano katika barabara za umma na mitaa….”

Katika kifungu cha 11 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1993, Msajili wa Vyama vya Sisasa amepewa mamlaka ya kukitaka chama cha siasa kinachotaka kufanya kikao au kuandaa mkutano wa hadhara, kutoa notisi ya saa 48 kabla ya kikao kwa Ofisa wa Polisi wa aneo husika.

Lengo la kutaja vifungu hivyo vya Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, Sura ya 322 na Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1993 ni kueleza kuwa, pamoja na sheria hizo kuzipa Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa, mamlaka ya kuzuia vikao na mikutano ya vyama vya siasa, unapofikia uchaguzi kifungu cha 53 (2) kinatoa ruhusa kwa vyama vya siasa na wagombea kufanya mikutano ya kampeni katika eneo ambalo uchaguzi unafanyika.

Lakini, kikubwa ambacho mara zote Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekuwa ikikisisitiza hasa wakati wa kampeni za chaguzi ndogo, ni kuzingatia kifungu cha 53 (2) cha Sheria ya uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, ambacho kinasisitiza idhini ya mgombea au chama cha siasa kuitisha au kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata husika kwa madhumuni ya kushawishi kuchaguliwa kwa mgombea au kuendesha kampeni ya hadhara au ya nyumba kwa nyumba na si vinginevyo.

Itakumbukwa kuwa, kwa nyakati tofauti hapa nchini, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhani, amekuwa akisisitiza kuhusu ruhusa inayotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo kuwa ni kufanya kampeni za uchaguzi kushawishi kuchaguliwa kwa mgombea na si mikutano ya kisiasa iliyozuiwa kwa mujibu wa vifungu viwili vilivyotajwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom