Jamii inayonizunguka inanipa mawazo sana ndugu zangu

trica

Member
Aug 31, 2020
73
154
Habarini ndugu zangu, naombeni niwape mkasa wangu kidogo ili walio nizidi umri na wenye busara wanishauri kwenye ili ninalopitia, maana nina ongozwa na mawazo sana na nashindwa kuiona kesho yangu ilio bora

Kwanza kabisa umri wangu ni miaka 30 kwa sasaivi, nimetokea katika familia ya ufukara mkubwa (ata elimu yangu ya o-level nilisomeshwa na wilaya kitengo cha elimu), nina mpenzi ambaye nimekaa nae kwenye mahusino miaka 5 sasaivi (nimetangulia kusema ivyo vitu viwili ili nielezee kinaga ubaga kinachonisibu)

Mpaka muda huu wa miaka iyo 30 sina familia (sina mtoto), rafiki zangu wengi wameoa, wana watoto na familia zao ila kwa upande wangu imekuwa tofauti kidogo, kwa huu umri nilionao napata ujumbe mwingi sana kutoka kwa marafiki na baadhi ya ndugu kuniuliza vipi nafikilia nini kuhusu kuwa na famili (nabaki na mawazo ndugu zangu)

Ndugu zangu muda mwingi katika maisha yangu nimeutumia shuleni, nilipomaliza form-four sikubahatika kuchafaulu kwenda advance level, ilinibidi kufanya vibarua vya hapa na pale na kuweza kufanikisha kupata pesa ya kusoma level ya certificate, baada ya kumaliza certificate nikaanza kupambana tena na vibarua vya hapa na pale kwa mwaka mzima na kupata pesa ya kusoma diploma, baada ya kumaliza diploma katumia tena mwaka mzima kupambana kufanya vibarua na kupata pesa ya kusoma degree (nashukuru mungu kwa level ya degree nilipata mkopo wa asilimia 96%) na zile pesa zilinsaidie kwenye mambo yangu mengine

Nilimaliza chuo level ya degree mwaka 2018 (mpaka ivi sasa bado natafuta ajira bila mafanikio yeyote yale)

Kwa sasa najifanyia vibarua vyovyote vinavyokuja mbele yangu, iwe ni kuchimba misingi ya nyuma, kukusanya kuni na kuuza kwa wakaanga samaki, kuchotea watu maji, na kadhalika (nk).

Nimeishia kupata ela ya kula tu, jamii, marafiki, ndugu wakiniambia kuhusu kuoa uwa wananiweka kwenye wakati mgumu sana nashindwa la kufanya.

MAHUSIANO.
Nina girfriend wangu nilikutana nae kipindi nasoma diploma mwaka wa mwisho yeye akiwa anasoma form 5 (PCB), akuweza kuendelea hakuweza kubahatika kwenda levele ya degree alienda kusoma diploma baada ya kumaliza from six, na alimaliza diploma mwaka jana mwezi wa 10.

Mimi na uyu bnti tumepitia up and down nyingi sana, mwaka jana niliisi mwenzangu amebadilika baada ya kuona mawasiliano yetu hayapo kama kipindi cha nyuma, na nilikuwa nikimuuliza mwenzangu anakuwa mkali sana, ilinilazimu nimuache uku nikiwa na uchungu sana moyoni maana ni binti niliyempenda sana sana (kumbuka wakati nipo nae uyu binti muda wote huo ndugu zake nilikuwa nawaona kwenye picha tu akiwa-post), ila rafiki zake baadhi nilikuwa nawafahau, baada ya kuaamua kukaa pembeni (nilifuta mawasilino yake kabisa) baada week 3 alikuja kunitafuta, aliniomba msamaa kwa yaliotokea na nikamsamehe kabisa tukaendelea na mahusiano mpaka ivi sasa

Mwaka huu mwezi wa saba aliniomba niende kwao nikaonanae na ndugu zake, nikamuone baba yake na mama yake (ndugu zangu nilipata kama woga flani ivi, maana sikutegemea awe na ughafla wa kuniambia vile) ni kweli nampenda aswaaa, alianza kunipa simu niongee na mzazi wake wa kike (mama yake) alisema ameshamuambia mama yake kuwa mimi ni rafiki yake

Kuna siku mama yake aliniambia ni lini nitakwenda kuwasalimia (maana wazazi wake wanakaa mkoa wa kaskazini), nilimpanga tarehe ya kwenda kuwasalimia, tarehe ikafika nikafika kwao, nilipokelewa vizuri sana sana sana, nilitambulishwa kwa ndugu zake wengi tu. sikuwahi kufika kwa yule binti ila baada ya kufika nikajionea mwenyewe, kwao ni watu wenye uwezo kifedha, kifupi wanajimuda aswaa, nikaanza kama kukosa confidence ivi.

Mwezi huu uyu binti anakwenda kusoma chuo kikuu, matokeo bado hayajatoka ya chuo (selection),

Huyu binti tangu nimeenda kwao ni mtu ambaye ametokea sana kunipenda zaidi ya kipindi cha nyuma kabisaaa, kila ninachosema kwake anakuwa yupo tayari, ila issue inakuja kwenye mambo yafuatayo.

Anakwenda kusoma chuo (hapa pananiogopesha kama penzi letu litaendelea kudumu)
kuhusu kumuoa yupo tayari kabisaa ila tatizo linakuja upande wangu sina kazi kabisa kwa sasa (nabagaiza sana sana) kwenye miangaiko yangu kupata ela ya kula
ila pia anaonyesha kuitaji japo sana sana sherehe, hapa napo pananipa mawazo

Mpaka sasaivi ni binti amekuwa akiniheshimu, akinisikiliza tunahishi vizuri sana pasipo shida yeyote ile, ni binti amabaye uwa ananitamkia maneno haya "Siitaji pesa wala kitu chochote kutoka kwako, ila nahitaji tuje kuishi maisha mazuri, pambana unavyojua ki-alali kikubwa tuje kuishi maisha mazuri" aya maneno yake uwa yanazunguka sana kichwani mwangu.

Kuna muda pia nawaza, nimuache nikatafute binti mwingine uko nyumbani kwetu nianze nae maisha kwa kuoana kwa kutoa maali tu kwao, nianzishe familia kuliko kuanza kusubiliana na uyu ambaye kwanza anataka sherehe (ananisikiliza kote ila kwenye kufunga ndoa ambayo sherehe akuna anaonekana kutokuwa tayari).

Nampenda sana sana, ila kuna muda nakosa amani binafsi, umri unakimbia sana ndio kitu kinanipa mawazo pia.

Samaani kwa uzi mrefu, mbarikiwe
 
Kuna muda wasiwasi wako unaweza kuwa ndio maradhi yako halaf kuna muda wasiwasi huohuo unakua ndio akili

Achana kuwaza ndoa ikiwahujajipanga, hakuna mzazi atataka kumuozesha mtu ambaye anabahatisha maisha

Pambana mbaba usichoke kupambana mradi binti kasema atakusubiri bas muamini
 
Pambana upate pesa ili uwe na maisha mazuri, Kama nayeye amekwambia upambane pambana kweli, usifikirie ndoa kabla hujajipanga...kuhusu yeye kwenda chuo Kama anajielewa basi ataendelea kukuvumilia Hadi atakapo hitimu, ila kuwa jasiri na uache uoga.
 
Tulia mkuu, acha binti aende chuo wakati wewe unaendelea kupambana. Kama kweli una bidii, mpaka akifikia kumaliza chuo utakua umepiga hatua kimaisha.

Kuna wakati umasikini unatufanya tuogope vitu vizuri. Kwakua anakupenda na anakuheshimu, inatosha kabisa kumpambania. Don't give up brother!
 
Mkuu tafuta hela tafuta hela tafuta hela akienda chuo akikutana na ma lecturer vijana wadogo Wana pesa watakuibia chap Kama huna pay

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tafuta hela tafuta hela tafuta hela akienda chuo akikutana na ma lecturer vijana wadogo Wana pesa watakuibia chap Kama huna pay

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Na uwakika hii comment imemvunja moyo. Bro lets look on positivity, demu kashakiri wacha ngoma ichezwe sasa kwa demu kwenda chuo na mwana apambane kitaa. Siku yeyote atapata kazi na hizo hofu zilizomjaa zitabaki historia
Mtoa mada pambana mdogo wangu
 
Na uwakika hii comment imemvunja moyo. Bro lets look on positivity, demu kashakiri wacha ngoma ichezwe sasa kwa demu kwenda chuo na mwana apambane kitaa. Siku yeyote atapata kazi na hizo hofu zilizomjaa zitabaki historia
Mtoa mada pambana mdogo wangu
Ni kweli mkuu lakini Kama umefika chuo utaelewa Nini namaanisha chuo Kuna stunts nyingi mnoooo ni Bora kumwambia ukweli ajiandae kisaikolojia

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli mkuu lakini Kama umefika chuo utaelewa Nini namaanisha chuo Kuna stunts nyingi mnoooo ni Bora kumwambia ukweli ajiandae kisaikolojia

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Nishapita huko naelewa sana mkuu. Demu kakiri anampenda jamaa na hajari hali yake kwasasa na jamaa nae kakiri kuwa anampemda demu. Demu ni lazima aende chuo hakuna alternative nyingine and the guy is psychological tortured because he is ain't in a position to change the situation sasa huu ni ujinga kuwaza kitu ambacho huwezi kukifanya kwasasa.

Ndiomana namwambia ili aweze kuyaacomodate hayo yote aendelee kufanya vibarua vyake huku akitafuta ajira akifanikiwa hofu aliyonayo itapotea na mambo yataenda vizuri.
 
Nishapita huko naelewa sana mkuu. Demu kakiri anampenda jamaa na hajari hali yake kwasasa na jamaa nae kakiri kuwa anampemda demu. Demu ni lazima aende chuo hakuna alternative nyingine and the guy is psychological tortured because he is ain't in a position to change the situation sasa huu ni ujinga kuwaza kitu ambacho huwezi kukifanya kwasasa. Ndiomana namwambia ili aweze kuyaacomodate hayo yote aendelee kufanya vibarua vyake huku akitafuta ajira akifanikiwa hofu aliyonayo itapotea na mambo yataenda vizuri.
Sawa mkuu kijana apambane Sana uvumilivu una kikomo

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Miaka 30 bado mtoto sana
Bill gates alioa akiwa na miaka 40
Jitulize..achana na haraka..

Binti nenda nae hadi itakavyokuwa..
Usianze fanya maamuzi Kwa hofu
Ushauri mzuri Sana kijana sijui ana machepere ya wapi umri bado wa kuoa anaanza kupanic yeye apambane kusaka hela tu Dem Kama atasepa aende tu yeye bado ana biiig room

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Sawa mkuu kijana apambane Sana uvumilivu una kikomo

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Yeah cha msingi apambane, yatakayotokea huko mbele akili ya kudeal nayo atakuwa kashazipata. Sio sasa hivi anababaishwa na uwezo wa wazazi wake, mara demu anataka sherehe tatu demu anaenda chuo wasiwasi umemjaa. Sasa alitakaje? Alitaka awe fukara kama yeye? Asiende chuo?

Point ya demu "waje kuishi maisha mazuri baadae" naye aichukulie hiyo kama catalyst or an inspirational point towards his hustling.
 
Back
Top Bottom