Jamii ina changamoto gani ambazo tukizibadilisha itakuwa fursa ya biashara?

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
929
1,276
Wakuu heshima kwenu, nipo mahali sahihi kwa wakati sahihi, na jukwaa sahihi. Tupo watu wengi humu zaidi ya 10000, so hebu tupeane mawazo, huenda mimi sikuwa nayo, mwenzangu akawanayo. Jamii yetu inachangamoto gani zinazohitajika kutatuliwa, ambapo changamoto hizo hupelekea kupata fursa ya biashara.

Nakuomba kuwa huru kuzitaja na ikipendeza ukaweza na solution yake, naamini wadau wanapata mawazo ya kuanzisha biashara kuhusu mtaji sio kigezo, kigezo changamoto ipi itaweza kutatuliwa na kupeleka kupata fedha. Naanza na mimi, kwa sasa kwa mkoa wa Dar kuna changamoto ya wadada wa kazi, hivyo endapo utaanzisha day care naamini utapata watu wengi saana, ila hiyo day care ilenge watu wa kipato cha chini na cha Kati.

Nina uzoefu kwa hilo na linanipa faida, maana niliacha kuuza viatu nikaamia kwenye day care Mungu si Athumani wala Kingwendu, kukunja laki tano sita kwa mwenzi si haba. Panapo majaaliwa nitakuja na mchanganuo na hatua nilizozipitia kuanzia moja hadi mia moja kuweza kumiliki Nussery School and Day Care.

Turudi kwenye mada wadau tufunguke, karibuni
 
Changamoto 75% zishataturiwa ila hao walio tatua hizo changamoto nao wamejitengenezea changamoto automatically... Ukiweza kuwa tataria unafanikiwa maana pesa washakuwa nazo wao na wanapenda kuingiza zaidi ukirahisishia njia ya kuzipata zaidi utazipata nawe.
 
hapo hapo kwenye hilo tatizo ulilolizungumzia, la ukosefu wa wadada wa kazi za nyumbani.

Solution nyingine kwa tatizo hilo, unaweza kuanzisha ka kampuni fulani hivi ambako ni kama "Dalali", una tafuta wadada ambao wanasaka kazi, unawa link na familia zinazotafuta wadada wa kazi. Hapo unaweka labda gharama ya ku link ni elfu 50 tu. ukiji brand vizuri ukajitangaza, its a matter of time kabla hujaanza kukusanya mamilioni.

kitu cha muhimu ni kuwafanyia vetting kidogo hao wadada, jaribu kuwaita ofisini kwako uwafanyie "interview" kuona kweli wana basics skills, ikiwemo maadili na uaminifu. (hii inahitaji uwe mjuzi wa saikolojia kidogo). Hii itakusaidia familia utazozipatia wadada wa kazi wakutangaze kwa wengine, kwa kuwa umewapa suluhisho la kudumu juu ya tatizo lao.
 
Changamoto, ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo, solution; kuwe na Agency itakayo tafuta kazi zile za temporally ama longterm .. ,skilled ama unskilled specific kwa wahitimu wa vyuo na college .... wengi wa wahitimu Hata humu hawachagui kazi ila hawajui pa ku turn to...
 
Kwani ukosefu wa ajira unasababumishwa na nini hasa?

Nijuavyo ni kwamba Demand ni ngogo sana hasa kwenye sekita za viwanda ambazo ndo zinaajiri watu wengi, tuna viwanda vya vyerehani tu, tunahitaji viwanda vikubwa kama A to Z arusha yenye kuajiri watu 10,000 plus
Changamoto, ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo, solution; kuwe na Agency itakayo tafuta kazi zile za temporally ama longterm .. ,skilled ama unskilled specific kwa wahitimu wa vyuo na college .... wengi wa wahitimu Hata humu hawachagui kazi ila hawajui pa ku turn to...
 
Jamii nnayoishi Ina changamoto ya wamama/vijana wengi kutokuwa na kazi za kuwaingizia vipato.

So nikaamua kuwaletea fursa ....na kuwakopesha mitaji Means nawaletea samaki wanakopea wanakaanga wanauza wananipa changu...vijana wanachukua dagaa kila mtu gunia ananiletea hela ! Naona Kama wananyanyuka!
 
Shida ni elimu ya darasani inamuandaa mtu kwenda kuwa tegemezi wa ajira ya kuajiriwa mbaya zaidi haimpi mtu hata ways za kuwa competitive kwenye ajira anayoimbambania mfano niambie wasomi wa ngapi wa level za degree wamekuwa aggressive kwenye soko la ajira nje ya nchi hakuna ila wasomi wa ngapi wa nje ya nchi yetu wamekuwa agressive kwenye soko letu la ndani la ajira ni wengi sana...

Mpaka ilifika mahali mkuu wa nchi ikambidi haoji iweje hizo nafasi wanapewa watu wa nje humu ndani hakuna? Mfn: tuna chuo kama COET ila umuhimu wa wasomi wa chuo hicho kwa nchi hii ni sawa na hakuna as despite wao ni ma engineer but mapinduzi gani ya sector yao wamefanya hata tanzania ikajivunia kuwa nao zaidi ya wao kwenda kulilia ajira serekalini a time unaona kabisa elimu yetu ina mapungufu flani sehemu flani SUA angalao ....

Sasa hapo unategemea jamii yetu kunufaika??!.poleni wale niliowagusa but hayo ni mawazo yangu based kwa kile nilichojifunza na kujionea
 
Back
Top Bottom