Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,173
- 27,223
Nimeona na mimi niweke neno kwenye haya masuala ya kuhusu Magufuli na mambo yake na jinsi serikali ilivyokuwa.
Lakini naona kama jamii imegoma kabisa kuhusu Magufuli chochote kinachosemwa kuhusu Magufuli na ndio maana bado nguvu kubwa na pesa inatumika kupambana nae.
Jibu la harakaharaka la wanaosema ni kuwa "Magufuli alilisha watu uongo", huenda ikawa kweli au la
Lakini ni uongo gani huu ambao watu hata kwa macho ya kawaida washindwe kuuona na wakubali kukaa nao hadi leo? Huwa tunasema uongo baada ya muda huumbuka. Ila mbona mambo bado? Na nguvu inazidi kutumika na muda unayoyoma.
Haya yote yanayosemwa sasa yalisemwa sana mwaka jana kuhusu Magufuli tena zaidi ya hivi, lakini kwa nini jamii kubwa bado imegoma? Ikiwa mwaka huu nao utapita kwa jamii hii kugoma, nini kifanyike? Kwa maana maneno yote yameshaisha, ila bado ngoma ndio kwanza mbichi. Itumike njia gani nyingine? Au huenda wanaosema ndio tatizo?
Najaribu kuwaza nguvu kubwa imetumika na bado inatumika kwa kutumia wanasiasa, wanaharakati, magazeti na waandishi wengi wakongwe kupambana na marehemu na zimeandikwa makala na mada za kila aina zaidi hata ya 1000, lakini kwa nini bado wanashindwa? Hoja ya msingi kwenye mada yangu ndio ipo hapo.
Ni kweli tumekubali kupambana na kivuli Cha marehemu mwaka wa Pili Sasa, Ila bado tunashindwa?
Niliwahi kujua Magufuli ana nguvu kubwa kwa kuwa yupo hai, ili sikuwahi kujua Magufuli ana nguvu kubwa hivi akiwa amekufa.
#SSH 2025# kazi iendelee#....