Jamii haijawakubali walemavu kwenye siasa-Regia Mtema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamii haijawakubali walemavu kwenye siasa-Regia Mtema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Jul 15, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Salim Said

  “MIMI ni mlemavu wa kimaumbile wala si mlemavu katika kazi, lakini kuna watu ni wazima kimaumbile, lakini ni walemavu kwenye kazi,” hivi ndivyo anavyoanza Regia Mtema katika mazungumzo yake na Mwananchi.

  Mtema msichana ambaye ni Afisa Mafunzo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Kurugenzi ya Organaizesheni, anasema ulemavu wake haumzuii wala kumpunguzia uwezo wake wa kufanya kazi.

  Kielimu Mtema ni muhitimu wa Shahada ya kwanza katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua) kwenye fani ya Sayansi ya Uchumi na Lishe.

  Anasema, amejipatia elimu yake ya Msingi katika shule ya msingi Mchikichini Ilala kuanzia mwaka 1989 hadi 1995, huku elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne akiipatia katika shule ya Sekondari ya Forodhani kuanzia mwaka 1996 hadi 1999 zote za jijini Dar es Salaam.

  Mtema anasema, alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa katika Mchepuo wa Kemia, Biolojia na Lishe (CBN) mwaka 2000, lakini aliomba uhamisho ili kwenda shule ya sekondari ya wasichana ya bweni Machame Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, kwa kuwa kutokana na hali yake alishachoka kusoma shule za kwenda na kurudi.

  “Nilianza kuvutiwa na siasa tangu sekondari, lakini nilishindwa kujiunga na chama chochote cha siasa, kwa sababu sekondari za zamani zilikuwa hazina masuala ya siasa tofauti na sasa, ambapo matawi ya vyama yapo hata katika shule hizo,” anasema Mtema.

  Anasema, akiwa Machame alivutiwa na Chadema, baada ya kutembelewa na Mwenyekiti wa sasa wa Chadema Freeman Mbowe alipokwenda kuwatembelea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2000, wakati huo akiwa ni mgombea ubunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.

  “Nilivutika sana na Chadema nilipokutana na Mbowe alipokuja shuleni kwetu kuomba kura mwaka 2000 akiwa ni mgombea ubunge, alinivutia sana na sera za chama chake, ingawa sikujiunga na chama kwa wakati huo, tena alishinda,” anasema Mtema.

  Baada ya kuhitimu kidato cha tano na sita Mtema anasema, alijiunga na chuo cha kilimo Sua, kuanzia mwaka 2003 hadi 2006 ambapo alifanya, fani ya Sayansi ya Uchumi na Lishe na huko ndiko alikopata uamuzi wa kujiunga na siasa rasmi yani chama cha Chadema.

  “Nilijiunga na Chadema nikiwa Sua mwaka 2005 kufuatia vuguvugu la kisiasa vyuoni,” anasema Mtema.

  Anasema, baada ya kukamilisha masomo yake chuoni hapo, mwaka 2007 aliamua kujiunga na Chadema Makao Makuu akiwa ni Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana na Wanawake, iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wake John Mnyika.

  Anasema akiwa katika nafasi hiyo, alipata uzoefu kwa kujifunza mambo mingi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii huku akipata msaada mkubwa wa mafunzo na maelekezo ya kazi kutoka kwa Mnyika.

  “Awali nilipofika makao makuu kuna wengine walidhani kama sitaweza kufanya kazi na wengine waliona nitaweza, lakini kwa ushirikiano na wenzangu nimefanikiwa sana,” anasema.

  Mtema anafafanua kwamba, baada ya mabadiliko ya uongozi ndani ya kurugenzi mbalimbali za chama chao Januari mwaka huu, aliteuliwa kuwa Afisa Mafunzo katika Kurugenzi ya Oganaizesheni na Mafunzo ya Chadema.

  “Hii ni sababu na ushahidi tosha kwamba kazi zangu zinakubalika kwa kuwa kama hazikubaliki nisingeteuliwa katika nafasi hii hata siku moja,” anajisifia Mtema.

  Anasema, ameamua kujiunga na siasa na kuacha kazi nyingine za kuajiriwa, kwa sababu anaamini kuwa, katika siasa ni rahisi kwa mtu kutoa maoni yake na kusikilizwa pamoja na kufanyiwa kazi kwa haraka.

  “Mimi ni mlemavu, lakini nyuma yangu kuna walemavu wengi, ambao hawajapata elimu kwa sababu mbalimbali zikiwamo mitazamo potofu ya jamii, juu ya watu wenye ulemavu, na kama huna elimu huwezi kuajiriwa, hivyo niliamini kuwa ipo siku moja nipata nafasi ya kuwasaidia japo kufikisha kero zao serikalini,” anasema Mtema na kusisitiza:

  “Nilitaka kuja kuwasaidia wenzangu, kwa sababu kwenye siasa ndio mambo yote yanakofanyika. Utungwaji wa sera, sheria, usimamizi na marekebisho yake yanafanyika katika siasa, nilipenda na mimi niwe miongoni mwa watunga sera, sheria na hata warekebishaji.”

  Akizungumzia changamoto kazini Mtema anasema, kwanza alipata ugumu kutoka katika familia yake kwa sababu hawakuwa tayari mtoto wao ajiunge na kazi ya siasa kutokana na imani waliyonayo kwamba, siasa ni fujo, vurugu na mchezo mchafu.

  “Hofu yao kubwa ilikuwa ni kupoteza maadili kwa sababu wanaona siasa labda ni uhuni na ni kazi isiyo na heshma. Lakini nilitumia ujanja bila ya wao kujua,” anasema na kutoa mfano wa ujanja aliyotumia:

  “Kwa mfano, baba yangu mzazi alijuwa kuwa mimi ni mwanasiasa wa Chadema Makao makuu baada ya miezi miwili, licha ya kuwa nilikuwa nalala nyumbani mwake, nakula chakula chake na nilikuwa napanda gari baadhi ya wakati kwa fedha yake, alikuwa ananiona natoka asubuhi narudi jioni, tena alijua kupitia mtu mwingine sio mimi.”

  Anasema, baada ya kuja walisikitika sana, lakini ilibidi wakubali matokeo na mpaka leo hawaridhiki mimi kuwa mwanasiasa na hii inatokana na tafsiri mbaya ya siasa katika jamii kuwa ni fujo, mikiki mikiki na uovu.

  Mtema anasimulia kuwa, kwa upande wa changamoto kazini, “Nilipoonekana kuwa ni mlemavu maswali yalikuja ataweza kweli? na wengine walikuwa wanaongea pembeni, na kunihukumu kuwa siwezi tu, lakini baadhi waliona naweza kina Mnyika na nimefanya nao kazi vizuri sana.”

  Anasema, kwa wale walimuamini na kumkubali kuwa anaweza, wamethibitisha kwa sababu ndani ya muda wake Chadema ameweza kufanya kazi vizuri, tena wakati mwingine kuliko hata wale waliowazima na wakamilifu wa kimaumbile.

  “Ulemavu wangu ni wa kimaumbile tu lakini si katika kazi,” anasema Mtema.

  Anasema, baadhi ya wakati akipanda Jukwaani kabla ya kuhutubia umati wa watu katika mkutano, huwa anashangiliwa sana jambo ambalo anasema humpa maswali mingi bila ya majibu, iwapo kelele hizo ni za kukubalika kwake au la.

  Mtema anasena amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kazi ya siasa hasa akiwa makao makuu ya Chadema na kwamba matarajio yake kwa sasa ni kugombania nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

  “Nikifanikiwa kushinda nitakuwa nitatengeneza historia kwa sababu nitakuwa msichana na mlemavu wa kwanza Tanzania kuwa katibu mkuu wa baraza la vijana katika vyama vyote,” anasema Mtema.

  Sambamba na hilo, Mtema anasema anatarajia kujitupa Jimboni kugombea ubunge katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kama Mwenyezi Mungu atamueka hai na mzima.

  “Kwa mwaka 2010 ni ngumu kuingia jimboni, lakini matarajio yangu ni kuijtupa huko katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kwa sababu jamii bado haijawakubali ipasavyo walemavu, wanawake na vijana lakini natarajia ikifika muda huo, mwamko utakuwa wa kutosha katika jamii kuhusu sisi,” anasema.

  Mbali na kuwa Afisa Mafunzo wa Chadema Mtema ni Mkurugenzi wa Vijana na Michezo katika Chama cha Walemavu Tanzania (Chawata).
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hongera sana, Ihope your courage will inspire others tujoin poilitics..umeonyesha njia..
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  This is ridiculous! yaani wapewe tuu kwa sababu ni walemavu?

  haya ndio mambo ya kurudishana nyuma kama yale ya VITI MAALUM VYA WANAWAKE

  kila mtu anajua kuwa wanawake uwezo wao ni mdogo (YES IVE SAID IT) na kama hamuamini huku JF mna wanawake wangapi ambao wanakuja kubadilishana mawazo nasi humu..lakini enzi za UTAMU ahhhh utawaona....na bila kusahau MICHUZI kwa sababu kule kuko light weight


  Si maanishi wote lakini wengi wao they are just sub standard na hao waliojitahidi kusoma na kupata nafasi nao ni useless...hili tatizo kubwa mno Tanzania...

  kwanza ngoja nitafute ile thread ya upendeleo kwa wanawake

  And please msitake kupoint out eti fulani mbona mwanamke na anachangia humu...upuuzi mtupu huyo ni jamaa sema ana majina mpaka ya kike
   
  Last edited: Jul 15, 2009
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  GT ndio unataka kutwambia humu kuwa hakuna wanawake wanaochangia? ...

  hakuna sababu ya kuwa na viti maalum vya wanawake au viti maalum vya walemavu katika siasa wala katika kazi za kawaida.
  mwanamke na mlemavu akae katika nafasi kwa mujibu wa uwezo wake na sio kwa kuwa tu ni mwanamke au mlemavu.

  wako wanawake wengi tu ambao wana uwezo sawa au kuliko wanaume ambao wamepata nafasi za juu kwenye vyuo vikuu, taasisi mbali mbali na serikalini.

  Nafikiri wanawake wenye uelewa wanachopigania ni kupata haki yao pale wanapostahili na sio kupewa haki ya mwanamme kwa kuwa tu yeye ni mwanamke.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Apr 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  GT vipi tena Mkuu?
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I am sure now GT ameshajibiwa na Regia went for the jugular, she contested bila kuomba feva and whatever the outcome, to me she is a winner
   
 7. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ametuonyesha njia na ninakwambia yule tapeli mteketa na ccm kilombero wanajuta kukutana regia wa mtemanyenja, binti wa kindamba jasiri kuliko mama lwakatere, mahiri zaidi ya celina kombani makini kuliko tunavyodhania.

  Tulijange,tulijangee, tulijangi nakaka x2 tulijange,tulijangee, tulijangi nakaka x2 tuwoni ndembu tunyuminyumi!!! Regia wimbo huu ni national anthem kwa mndamba hususani tunapokuwa ktk vita mathalani ya hii kwako. Ktk halilyoyote ya matokeo nakusihi waombe wamama na wazee hapo ifakara muuimbe wimbo, mimi nakuimbia licha ya kuwa niko dar kiroho tupo nawe. Big up mhaja wangu, mulungu akutangi muhumbu. Tili vandu mulungu ka patali ila daima atakupigania.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  GT vipi tene bro!! kuna thread zinginekule waweza kuchangia bro!
   
 9. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nashauri technical team ihamie kilombero haraka iwezekanavyo...
   
 10. N

  Nampula JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usikate tamaa dada.......huo ndio mwanzo wa mapambano na waswahili wanasema mwanzo mgumu............keep it up one day itatike tu.
   
 11. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya madai ya huyu binti ni ya UONGO. Mbona mwenzio, Salum Barwani wa CUF ambaye ni ALBINO kashinda kule Lindi?

  Watu hawatoi kura kwa sababu ya ulemavu wako, bali kwa ushawishi wako. Nilimuona huyu mdada pale Movenpick kwenye ule mdahalo wa wagombea vijana and there was nothing special about her anyway. Nitaishia hapo na ku:tape: bakuli langu!
   
 12. H

  Haika JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Akishindwa ni kwa kuwa hajaeleweka, na si kwa kuwa ni AU si mlemavu wa kitu fulani.
  Inawezekana pia alimuona mzima wa viungo na mlemavu wa vitu vingine akaeleweka zaidi.
  unajua unaweza kuwa na pointi za muhimu sana lakini presentation yako ikakuangusha vile vile.
  ila muhimu usikate tamaa.
  ukiwa mlemavu wa viungo si lazima kila kitu utakacho upate, dunia haiko hivyo, you get some you loose some.

  Hongera dada, tuwakilishe hata na sie ambao ulemavu wetu haupigiwi debe, wala kuchezewa kidedea walemavu wa ...
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Tuna mengi ya kujifunza kwako dada na Kiongozi wetu! RIP dada yetu Regia Mtema!
   
Loading...