Jamii Forums: JIWE lililokataliwa na waashi lakini sasa ndilo jiwe kuu na Msingi wa Habari Tanzania

CCM na serikari yake wote ni majuha dunia nzima sasa inajua, JF ni sehemu ya wahuni leo hii kila kitu wanaanya kwa kutumia kilichomo JF, hongera manyerere jackton kwa kuwapa wa kina Kova intelejensia ya kumkamta Ludovic Joseph. siipendi serikali ya dhaifu a.k.a fastjet
 
Wanaosema JF ni chombo cha wahuni ni watu wasijua kinachoendelea...
Hata Misri kwa Mubarak hakuamni mitandao kama inasema kweli.
Haifuati DINI wala CHAMA cha SIASA
Kwani hata leo hapatawaliki kwa sababu ya Mitandao ya Kijamii na sio Misri tu kwenye hukumu ya Mashabiki wa Mpira na matatizo ya Brotherhood bali Mashariki ya kati
Ni CHINA tu ndio wamedhibiti
 
Jamii Forums sio mtandao wa kihuni lakini ni mtandao wenye memba wahuni toka vyama vyote,dini zote na jinsia zote cha msingi tuwapinge tuwaelimishe na ikiwezekana wadhibitiwe ili wasichafue jukwaa hili.
 
Ile dhana ya Polisi Jamii, wangeongeza na Polisi Jamii Forums kama acknowledgment. Manna JF imekuwa reliable sources ya information nyingi ambazo ni nyeti. Long live JF.
 
Serikali inatumia JF kwa tuhuma zinazowalenga CHADEMA tu, kwa zinazowalenga CCM hazitumiki, angalia leo Mwema anasema uchunguzi wa wtekaji wa Dr. Ulimboka haujakamilika ndo maana hakuna aliyepelekwa mahakamani, lakini wa Lwakatare umekamilika na yuko mahakamani
 
Kinachofurahisha ownership ya habari inamhusu blogger mwenyewe na wasomaji bravo JF
 
JF siyo mali ya Chadema wala CCM wala Cuf wala NCCR Mageuzi.

JF ni jukwaa huru kila mtu anaeleza fikra zake.

Pro-Chadema JF kwa akili zao wanadhani JF ni mali ya Chadema.
 
Masisiemu ni manafiki sana na yana ndimi mbili yote (mashetani), anzia mwenyekiti wao wa chama taifa mpaka mabalozi wa nyumba kumi
 
Wana JamiiForums, mnakumbuka vizuri jinsi mtandao huu ulivyopingwa vikali na watesi wa haki za binadamu hapa Tanzania (CCM na Serkali yake) tangia misingi yake yaani JamboForums.

Serikali na Taasisi zake karibia zote hasa JESHI la polisi lilikuwa mstari wa mbele kusema hii JF ni ya wahuni bila kusahau viongozi wengi wa serikali wakiwepo wabunge wa CCM kama MAMA G. LWAKATARE aliyetaka JamiiForums ifungiwe.

Leo hii tunaona mkurugenzi wa usalama wa CHADEMA yuko mahakamani tena serikali ikidai ina ushaidi kutoka JamiiForums.

Swali langu ni lini Serikali ilitangaza kuwa JamiiForums siyo chombo cha wahuni tena?

Je, sitakuwa sahihi kusema kuwa JamiiForums ni jiwe lililokataliwa na waashi ambalo sasa ni jiwe kuu la pembeni?

:tape2:

Samahani Dr ni huyu nayemfahamu wa Business School kama ni wewe nimefurahi kuona mchango wako mimi ni mwanafunzi wako Dr
 
stone that they build refuse, will always be the head corner stone!

Ilitakiwa isome "But the stone that the builder refuse, shall be the head corner stone" kiswahili chake "Jiwe lilo washinda waashi ndio jiwe kuu la pembeni"

Teh teh....
 
sidhani kama inaweza kutokea kirahisi ccm ikawa na mtazamo chanya dhidi ya jf, kinachotokea ni kutapatapa kwa ccm. sawa mtu aliesombwa na mafuriko anatafuta hata unyoya ajishikize lakini ndio anazidi kusombwa.....poleni ccm kila kitu kinamwisho wake...mmebakiwa na maafisa polisi wa ngazi ya juu tu ambao ni makada wenu, na ndio wanaowasaidia mipira ya kupumulia.!!!
 
jamii forums ni kama uwanja wa taifa timu zote zinacheza lakini kuna timu mbili pinzani nazo ni cdm na ccm. timu nyingine zinafuta cuf, nccr na tlp
 
Back
Top Bottom