Jamhuri yawabadilishia hati ya mashtaka washtakiwa wanne, sasa kukabiliwa na wizi na kutakatisha zaidi ya Tsh. Bilioni 1

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,103
Jamhuri imebadilisha hati ya mashtaka dhidi ya washtakiwa wanne akiwemo mke wa marehemu, mtoto wake, wakili wa kujitegemea na mfanyakazi wa benki ya Stanbick ambapo sasa wanadaiwa kuiba na kutakatisha zaidi ya sh. Bilioni moja.

Washtakiwa hao ambao wamebadilishiwa mashtaka leo Julai 21, 2020 ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jandu Constructions and Plumber Ltd, Khairoon Jandu ambaye ndio mke wa marehemu, Zainabu Tharia binti yake, Wakili Mohamed Majaliwa na Meneja wa benki ya Stanbic Inrahim Sangawe.

Mapema leo asubuhi,washtakiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Casian Matembele lakini upande wa mashtaka aliwasilisha maombi ya kuondoa kesi hiyo mahakama chini ya kifungu cha sheria cha 90 (1)cha CPA kwa kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao (Nolle Prosequi)

Uhujumu.jpg
 
Cha kuwakamatia hamna, itakuwa ni mtindo wa kubadili mashitaka mpaka mwisho wa dunia
 
Back
Top Bottom