Jamhuri yakata rufaa kupinga Tido Mhando kuachiwa huru

Ndipo ninapokuuliza kuwa ZItto alipokuwa Mwenyekiti wa PAC walimtuhumu pia huyu Tiddo na wakamuita kwenye kamati wakamuhoji, je nao walikuwa wanataka kumkomesha kisa aliwapa nafasi wapinzani?
Zitto alimtuhumu? Au wana lumumba wenzako baada ya kuona anawaumiza na kipindi chake? Zitto hakuwahi kumtuhumu bali alihojiwa na kamati. Kuhojiwa na kamati sio kutuhumiwa na ndio maana wao hawakumuona na tatizo ila mkaamua kibabe kumpeleka mahakamani, ameshinda kesi bado mnakata rufaa. Mkimfunga ndio wakulima wa Korosho wataacha kudai pesa zao?
 
Zitto alimtuhumu? Au wana lumumba wenzako baada ya kuona anawaumiza na kipindi chake? Zitto hakuwahi kumtuhumu basi alihojiwa na kamati. Kuhojiwa na kamati sio kutuhumiwa na ndio maana wao hawakumuona na tatizo ila mkaamua kibabr kumpeleka mahakamani, ameshinda kesi bado mnakata rufaa. Mkimfunga ndio wakulima wa Korosho wataacha kudai pesa zao?
Inaonekana akili yako fupi sana kijana! Kitendo cha kuitwa tu na PAC aje atoe maelezo ni wazi kuna sehemu waliona ina uwalakini sasa kama alifanya alifanya tu na Mahakama ndizo zitathibitisha hilo na kama Makahama Kuu ikimkuta na hatia yeye si ataenda kukata ruaa kwenye mahakamani ya Rufani au? mbona unalilia sana wakati hiyo hipo kwaajili ya kutoa haki
 
Siku tatu tangu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando aachiwe huru upande wa jamhuri umekata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama hiyo ilimwachia huru Mhando na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye alisema sababu za kumwachia huru kuwa ni mikataba minne aliyoingia haikuwa na nguvu ya kisheria kwani haikusainiwa na wahusika akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Lakini Jamhuri wanadai mashtaka yao ni hayo hayo kwamba mikataba hiyo iliingiwa bila kufuata utaratibu.

Pia wanadai kwamba kuingiwa kwa mikataba hiyo isiyofuata utaratibu kulisababisha Kampuni ya Channel Two Group kufungua kesi na Serikali ikalipa mawakili Sh milioni 887.1 ambayo ni hasara iliyosababishwa na mshtakiwa.

Katika kesi hiyo Tido alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.

Chanzo: Mtanzania
Hao kina jamhuri wamezoea kugaragazwa mahakamani, hivyo naamini mahakama kuu itakazia hukumu ya mahakama ya Kisutu
 
Inaonekana akili yako fupi sana kijana! Kitendo cha kuitwa tu na PAC aje atoe maelezo ni wazi kuna sehemu waliona ina uwalakini sasa kama alifanya alifanya tu na Mahakama ndizo zitathibitisha hilo na kama Makahama Kuu ikimkuta na hatia yeye si ataenda kukata ruaa kwenye mahakamani ya Rufani au? mbona unalilia sana wakati hiyo hipo kwaajili ya kutoa haki
Nina uhakika wewe kiuhalisia uwezo wako wa kifikiri ni mdogo sana. Sin shaka ni wale mnaoshinda ofisi za wilaya za Chama kuomba buku buku za kula. Kama unabisha njoo Inbox nikuthubitishie kama una ujasiri.

Narudi tena Kamati kazi yake ni kuhoji na sio kutuhumu. Haiwezi kukutuhumu halafu ikakuhoji yenyewe na kutoa maamuzi. Waliotuhumu ni wana kijani baada ya kuumizwa. Ndio shida ya elimu ya form 4 failure kupewa kazi ya kutetea chama mitandaoni ni weupe kabisa.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake 6 kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.
_
Washtakiwa hao wameachiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 lakini baada ya kuachiwa, vigogo hao waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh.Bilioni 1.16 wamekamatwa tena. #MillardAyoUPDATES
 
Siku tatu tangu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando aachiwe huru upande wa jamhuri umekata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama hiyo ilimwachia huru Mhando na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye alisema sababu za kumwachia huru kuwa ni mikataba minne aliyoingia haikuwa na nguvu ya kisheria kwani haikusainiwa na wahusika akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Lakini Jamhuri wanadai mashtaka yao ni hayo hayo kwamba mikataba hiyo iliingiwa bila kufuata utaratibu.

Pia wanadai kwamba kuingiwa kwa mikataba hiyo isiyofuata utaratibu kulisababisha Kampuni ya Channel Two Group kufungua kesi na Serikali ikalipa mawakili Sh milioni 887.1 ambayo ni hasara iliyosababishwa na mshtakiwa.

Katika kesi hiyo Tido alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.

Chanzo: Mtanzania

Poor mzee wa watu Tido. Sasa mwite Jakaya awe shahidi wako mahakama ya rufaa. Kesi itakuwa imeisha. Ni mithili ya kesi ya Jamhuri dhidi ya Balozi Prof Mahalu. Alipoitwa Mkapa mahakamani na kesi ikafwekelewa mbali.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nina uhakika wewe kiuhalisia uwezo wako wa kifikiri ni mdogo sana. Sin shaka ni wale mnaoshinda ofisi za wilaya za Chama kuomba buku buku za kula. Kama unabisha njoo Inbox nikuthubitishie kama una ujasiri.

Narudi tena Kamati kazi yake ni kuhoji na sio kutuhumu. Haiwezi kukutuhumu halafu ikakuhoji yenyewe na kutoa maamuzi. Waliotuhumu ni wana kijani baada ya kuumizwa. Ndio shida ya elimu ya form 4 failure kupewa kazi ya kutetea chama mitandaoni ni weupe kabisa.
Ungekuwa una akili usingeanza kuishutumu Serikali kukata rufaa, kumbuka kinachoifanya serikali ikate rufaa ni hikohiko ambacho wakina Zitto walikiona kina walakini na hakuna sehemu nimesema kamati ilitoa hukumu.!! Ushahidi wako weka hapa kama kweli unajiamini huko DM unataka kuficha nini ufipa fc?
 
Dah yan nchi hii nimejua jinsiwatu wanavyopenda wengine waharibikiwe ilihali ukweli wote wanaujua sasa Tido amefanya nn hasa cha kumkatia rafaa

Sent using Jamii Forums mobile app

CCM Hoyeee tunaishi kwa visasi . Mtalimia meno for sure na bado sana ndiyo kwanza majeshi yanakuwa rallies kumalizia ngwe ya mwisho hatjui yatatokea yapi .
 
Muacheni huyu Mzee apumzike kwa amani. Kumkatia rufaa ni kumpa mawazo ambayo yanaweza kufupisha maisha yake.
 
Wamuache mzee wa watu akapumzike.
Jk ulimtoa bbc kuja kumdhalilisha mzee wa watu na ujuzi wake?please nenda ikulu ukaombe mzee Tido asisumbuliwe alirudi tanzania kwa heahima yako na TBC kikawa chombo cha uhakika cha habari.Mzee Tido ana EXPOSURE
Nimejifunza kitu, mwanangu akipata kazi ulaya na akawa ana performance ya kazi ya hali ya juu, nitamwambia ole wako Rais wa Tanzania aje akurubuni uje Tz kupewa kazi sijui cheo na ukubali yaani ole wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom