'Jamhuri Ya Ukombozi' yaundwa ndani ya Tanzania inahusisha Warundi na Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Jamhuri Ya Ukombozi' yaundwa ndani ya Tanzania inahusisha Warundi na Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Apr 21, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  WATU zaidi ya 200 mchanganyiko wa raia wa Burundi na Tanzania wamepiga kambi katika msitu wa hifadhi ya Igombe, wilayani Uyui na kujitangazia eneo hilo kuwa Jamhuri ya Ukombozi na kutundika bendera yao nyekundu.

  Watu hao wanaoaminika kuwa ni majangili na wateka nyara magari, walijikusanya takribani miezi miwili iliyopita, na kuingia ndani ya hifadhi hiyo katika kata ya Ibiri, Uyui, wakipitia vijiji vya Gilimba, Mkalya na Mirumba.


  Raia wa Burundi inadaiwa wameingilia katika miji midogo ya Kibande, Nyangani, Kilelema, Muyana na hatimaye Dihalo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


  Watu hao wanaodaiwa kujikusanya usiku, walipenya kutokana na miji hiyo kuwa na masoko ya usiku ambayo mara nyingi huanza saa 12.30 jioni na baada ya kuingia nchini kituo chao cha kwanza kilikuwa ni Kaliua wilayani Urambo.


  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa takriban mwezi mmoja sasa, umebaini kuwa watu hao mchanganyiko wa Wasukuma jamii ya wafugaji, Wanyamwezi na Warundi, baadhi yao ni waliokuwa wakihamishwa kutoka hifadhi mbalimbali nchini, hasa Tabora na Shinyanga.


  Aidha, utafiti umebaini kuwa watu hao ni wakatili na wanadai eneo hilo kujitenga na Tanzania.


  Gazeti hili kupitia baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na hifadhi hiyo, limebaini kuwa watu hao wakikamata wananchi huwapora simu na kuwapiga na kisha hutumia simu hizo kuwasiliana na ndugu wa waathirika kudai Sh 200,000.


  Moja ya matukio ya watu hao, ni la kuteka baadhi ya walimu wa shule za msingi karibu na hifadhi hiyo ambapo walimu licha ya mateso waliyopata walipigwa na mapanga nyayoni kiasi cha kushindwa kutembea, wasitoroke.


  Baadhi ya walimu ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, akiwamo kijana aliyejitaja kwa jina moja la Nassoro, walidai kutekwa na kuteswa kabla ya kuwaponyoka saa 9 alfajiri na kutoroka na wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na watu hao kuwatangazia kuwamaliza wakipatikana kwa madai kuwa wamevujisha siri zao kwa Serikali.


  "Niliteswa sana baada ya kukamatwa na kwamba hawa watu licha ya kuishi ndani ya hifadhi hiyo, pia wametundika bendera yao nyekundu na wanajiita Jamhuri ya Ukombozi ya watu waliojitenga ... nilifanikiwa kutoroka usiku saa tisa baada ya wao kulala na wana kiongozi wao waliyemchagua wanapika na kunywa," alisema Nassoro wenye makovu ya kupigwa.


  Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya wananchi hao, baadhi ya wananchi wamelazimika kuhama miji na familia zao kwa muda wakihofia kukamatwa baada ya kutoroka himaya hiyo baada ya kutekwa wakiwa hifadhini humo kurina asali.


  Watu hao inadaiwa wametengeneza magobori zaidi ya 40, wana SMG nne, mishale, mikuki, pinde na nondo tayari kukabiliana na askari wa doria na wananchi wanaopita ndani hifadhi hiyo na wamefunga njia zote za hifadhi na kubakiza moja.


  Aidha licha ya matukio hayo watu hao ambao Aprili 12 mwaka huu, saa tano za asubuhi, almanusura wateke gari la Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, namba SM 3755 baada ya wananchi kuwawahi maofisa wa hifadhi na kuhadharisha wasiingie ndani ya hifadhi hiyo.


  Kwa mujibu wa maofisa Maliasili wa halmashauri ya Uyui, walipewa taarifa juu ya watu hao na ili kujiridhisha kabla ya kuandika taarifa na kuandaa namna ya kuwaondoa, waliamua kwenda ndani ya hifadhi hiyo ili kuthibitisha, lakini walirudi baada ya kuonywa na wananchi.


  Uchunguzi zaidi umebaini kuwa watu hao wamemteua kiongozi wao wanayemwita Magelele Makonda na wana mganga wa kienyeji kutoka Mwandyematongo, Urambo ambaye anawapa dawa ili Serikali isiwaone na kuwaondoa ikiwamo kuwapa kinga dhidi ya risasi.


  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Uyui, hadi sasa inahaha kutokana na maisha ya wananchi wa eneo hilo kupatwa hofu juu ya mali zao na ililazimika kwenda kuhoji wananchi jirani na hifadhi hiyo Aprili 8 mwaka huu kubaini ukweli na baada ya kujiridhisha inaandaa taarifa kupelekwa ngazi za juu serikalini.


  "Ni kweli kuna watu zaidi ya 200 katika hifadhi ya Igombe wameunda Jeshi lao na kujitangaza kwamba ni nchi, inayojiita
  Jamhuri ya Ukombozi na wanamiliki silaha kali huku nyingine wakiwa wameunda wenyewe." alisema ofisa huyo kwa masharti ya kutoandikwa jina gazetini.

  Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Anthony Ruta, alikiri kupata taarifa za watu hao katika msitu wa Hifadhi ya Igombe na kwamba hawezi kutoa taarifa yoyote sasa hadi Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya itakapotoa taarifa ya uchunguzi wao.


  Hata hivyo, aliopoulizwa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa alisema ni mapema kuzungumzia suala hilo kwani bado utafiti unafanyika kubaini ukweli wake.


  "Kuna watu wanaendelea kufuatilia suala hilo mjini Nzega ambako wanalifanyia kazi na baada ya hapo nitatoa taarifa rasmi,” alisema Mkuu wa Mkoa ambaye aliwahimiza wananchi wa maeneo hayo kutokuwa na wasiwasi kwani Serikali inalifanyia kazi.


  Source: Gazeti la Habari Leo
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Ni wezi? kundi la watu 200? sipati picha, ebu mlio karibu ifuatilieni hii, isije ikawa watu wamechoka na CCM kwa style hii, mkabaki kusema wezi!

  "watu hao wamemteua kiongozi wao wanayemwita Magelele Makonda na wana mganga wa kienyeji kutoka Mwandyematongo, Urambo ambaye anawapa dawa ili Serikali isiwaone na kuwaondoa ikiwamo kuwapa kinga dhidi ya risasi" !!!!!!!!!! majimaji?

  Halafu wanajiita jamhuri ya ukombozi ili hali watu wanawaogopa? kuna uthibitisho wa wizi? au je hawataki kuongezeka wawe zaidi ya 200? naona kama kuna hofu na uzushi tu, polisi wamestarehe zao. Usije kukuta ni watu wema kabisa na wanaitakia mema nchi hii, kilichowachanganya ni kuwa wameichoka CCM basi!

  usikute Chadema na CUF wanakaribishwa kwenye jamhuri ya ukombozi! Mtikila hatakiwi akiziona bunduki atagwa kwa kila raia! LOL!
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Airstrike tuu... wastake kutuletea upumbavu wao hapa.. this is not Rwanda or Congo.. any treasonable offence kama hii should be dealt with severely.
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Vibaka tu hao! Wana dhahabu na almasi za kuwapa wamarekani wawape machine guns! Samabaratisha hao!
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mwaka 1997 kule biharamulo kulikuwa na kundi la wanyarwanda walikua wanavamia vijiji na kuiba mali na mifugo na kuua watu lakini liliangamizwa kwa makombora usiku mmoja na yeyote aliyajaribu kujiokoa aliangukia mikononi mwa vijana waliokuwa wamejichmbia karibu na maficho hayo.

  Nashauri uchunguzi ufanyike na serikali ibaini walipo na wingi na waamue ni silaha gani itumike kuwamaliza kabisa.
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  wasilete upuuzo hapa, wauwawe mara moja
   
 7. shugri

  shugri Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is serious--so are they rebels- wow i never thought that i will ever live to see my country in a crissis,
  Serious actions should be taken to the, they are threating the soverignity of my country.
  Where do they get the guts to do so? or the information imeongezwa chumvi?
   
 8. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ndio mabomu ttunayoyatengeneza, hilo ni eneo moja, lakini katika kila eneo sasa hivi kuna vikundi vya vijana choka mbaya, toka asubuhi wanakaa tu wanapiga soga, wenyewe wanajiita day worker(daiwaka) wanachoongoa wanajua wenyewe lakini all in all wamekata tamaa na maisha wako willing kufanya chochote
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Waziri wa ulinzi anasemaje kuhusu hilo?:shock:
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri serikali i act haraka ikichelewa haya majangili yatazidi kujiimarisha maana watu zaidi ya 200 si mchezo ni kikosi kizima wangekuwa 20 au 30 tunaweza kusema polisi tu inaweza kuwadhibiti.
   
 11. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Yupo bizee na Uraisi Zanzibar!
   
 12. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapa kazi ndogo2, wa2 200 sio wengi kiasi cha kuitisha nchi, hapa ni ku-apply2 ile "nia 2nayo, sababu 2nayo na uwezo 2nao". Chapa wa2 wapumbavu kama hawa, waziri mwenye dhamana ya ulinzi anatakiwa kuwajibika haraka hapa kabla hawaja ongezeka na kujenga netwek kubwa.
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Swala hilo wanalifanyia upembuzi yakinifu. Sasa huko watawachapa je? kama sehemu hiyo inaruhusiwa kuishi watu.?
  Inabidi swala walipeleke kwa Rais alipigilie sahihi.Harafu waende bungeni kulipitisha
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hiyo protokali mbona ndefu sana inaweza kuchukua miezi mingi ukitaka kunywa supu ya mbwa inywe ya moto ikipoa utasikia harufu yake.
   
 15. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wasiwasi wangu ni kwamba kadiri tunavyochelewa kuwadhibiti watu hao ndivyo wanavyojiimarisha na vita ya Kongo na Burundi ya maporini ndio inaandaliwa ndani ya mipaka ya nchi yetu. Leo ni 200, kesho watakuwa 2000 na keshokutwa 20,000 nk Chonde chonde watanzania hatujazoea kupigana kijeshi, waache wakurya wachapane wenyewe kwao.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Anasimamia maflati yake ya kupangisha hana muda kwani ameshindwa hata kutoa ripoti ya Mbagala aliyoahidi!!
   
 17. b

  bonvize Senior Member

  #17
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ni vizuri kuangalia jambo hili katika upeo mpana zaidi,kwa kuwa hata nchi ambazo hazina utulivu sasa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe zilianzia kwenye vikundi kama hivi ambavyo vilikuwa na nia ya ukombozi kutokana na unyonyaji unaofanya na kikundi kidogo cha watu kilichopatiwa thamana ya nchi kwa hila na mbinu chafu (kwa mf CCM).
  Kutokana na watu kukata tamaa halitakuwa jambo jipya kuona vikundi kama hivi vikiibuka kutoka pembe tofauti za nchi yetu kwa kuwa watu wamepoteza imani na watu waliopewa dhamana kwa hiyo wanaweza kukabidhi imani yao ha kwa wehu kama hao.
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  sasa protokoli gani ,watafuata maana polisi wanajiandaa kukabiliana na mgomo wa wafanyakazi.?
   
 19. Bright

  Bright Member

  #19
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani mabadiliko ya kisiasa si yapo ya aina nyingi na yanatokea kutoka na mazingira yaliyopo. Kama jamaa wanaleta ukombozi wa nchi nzima sasa wasiwasi wa nini kwa raia wema. Kwani matunda ya Zenji 1964 na MauMau Kenya ni yapi? Na hizi taarifa za idadi yao, kuwa na silaha kali, wafugaji, ujikusanya usiku - sijui mchana wanakuwa wapi - bado zinahitaji uchunguzi kweli? Isije kuwa ni mgogoro wa ardhi - wafugaji na wakulima.
   
 20. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ni kweli suala hili liangaliwe kwa upana wake. Niliwahi kuandika humu kuwa hivi sasa wadanganyika wanakosa kiongozi kama kinjeketile atakayewaambia risasi zitageuka maji, na watamfuata; kwa maana wamechoka na hali hii mbaya ya maisha. Sasa isije ikawa kuna mtu kishajitokeza; kwa hakika anaweza kupata wafuasi wengi katika muda mfupi sana, maana mtu ambaye hana uhakika wa kula hata mlo mmoja, na wakati huo huo anasikia mbunge analipwa zaidi ya 100,000 kwa kikao cha siku moja, anasikia watu wamekwiba fedha nyingi na bado hawachukuliwi hatua, na wakati huo huo yeye anaambiwa nchi ni maskini; akiambiwa njoo tuna silaha za kutufanya tupate milo mitatu kwa siku hakika atakubali kujiunga nao; kwake kuwa msituni akauawa huko ni sawa kwani hata bila ya kuwa msituni yupo anakufa taratibu na 'amani' yake.
  Wakati tukitafuta namna ya kuwaangamiza watu hawa mara moja, tuwe tayari pia kushughulikia mafisadi ambao wanaweza kuwa sababu ya watu hawa kujiunga pamoja!
   
Loading...