Jamhuri ya Muungano - Nilikuwa silifahamu hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamhuri ya Muungano - Nilikuwa silifahamu hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chifunanga, Jan 4, 2011.

 1. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  ..... Wale wanaojaribu kukwepa mjadala wa kina juu ya muundo wa Muungano siku zote hutumia hoja kwamba eti hakuna Serikali ya Tanganyika na hivyo isingewezekana kufanya mazungumzo kati ya Serikali hiyo na ile ya Zanzibar .

  Hoja hii ni dhaifu, maana yoyote yule atakayeulizwa Muungano huu ni wa nani na nani, atajibu ni wa Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar . Hawa ndiwo waliofanya mkataba. Sasa kama kweli Serikali ya Tanganyika haipo, nani kaifuta na vipi? Lakini muhimu zaidi Waswahili wanasema, “Yalopita si ndwele tugange lijalo”. Kama kweli kuna nia ya kuuenzi, kuulinda na kuuimarisha Muungano, basi tuangalie namna ya kuirejesha Tanganyika katika nafasi yake ili mjadala wa Muungano huu upate wenyewe wa kuujadili.

  Haikufutwa

  Katika makubaliano ya kimataifa yaliyounda Muungano, ambayo hata hivyo katika muda wote wa uhai wa Muungano yamekua hayafuatwi, hakuna kifungu hata kimoja kilichotoa au kuagiza kwamba Serikali ya Taganyika ifutwe kwa mujibu wa makubaliano hayo. Serikali ya Tanganyika , kama ilivyo ile ya Zanzibar , imelindwa na kifungu Na. (V) pale kinaposomeka kwamba:-

  The existing law of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their existing territories. Kinachosemwa hapa ni kwamba “Sheria ziliyopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kufanya kazi katika maeneo yao ”


  Wataalamu wa Katiba na sheria wanafahamu kwamba Katiba ndio ‘sheria mama’ ya sheria zote na hivyo Katiba ya Tanganyika imelindwa na inapaswa kuwepo na Serikali yake iwepo, pamoja na viongozi wake kuwapo na kusimamia mambo yasiyokua ya Muungano.

  Katiba na sheria za Tanganyika ndizo zilizotakiwa zitumike katika eneo la Tanganyika kwa yale mambo yaliyokuwa hayamo kwenye Muungano. Hiyo ndio tafsiri ya ‘ina maeneo yao ’.

  Hicho kipengele chekundu mi nilikuwa sikifahamu, wadau mnasemaje kuhusu hili?

  naomba kuwakilisha
   
 2. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu ya Tanganyika imeenda wapi? Kama ilifutwa, ni nani aliifuta na kwa mamlaka yapi? mbona ya zanzibar bado ipo?
   
Loading...