Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Marcio maximo ni kocha wa zamani wa taifa stars. Alikuja nchini mwaka 2006 ili aifundishe timu ya taifa, mara baada ya kuingia mkataba wa kazi na serikali, akaanza kazi pale uwanja wa karume.
Aliyekuwa rais wakati huo akaenda kuyatazama mazoezi ya timu ya taifa. Akashangazwa kumuona kocha huyo akifungua laptop yake na kuanza kueleza program zake za kikazi. Rais akasikika akisifia jinsi ambavyo kocha huyo anavyoweka kila kitu kwenye laptop.
Baada ya siku chache kupita, mimi nikiwa na wadau kadhaa pale ilipokuwa break point ambayo inatazamana na millenium towers, tulimsikia kocha maarufu wa soka jamhuri kihwelu akiponda sana kitendo cha mkuu wa nchi kumsifia kocha wa taifa stars eti kwa sababu anahifadhi taariifa zake zote kwenye laptop yake.
Jamhuri kihwelu maarufu julio kwa uongeaji wake ilibidi kila mtu aliyekuwa akinywa chai na kupata supu asubuhi ile acheke, kwani aliponda sana jinsi ambavyo rais mstaafu aliyepita alivyotekwa kirahisi sana na ufanyaji kazi wa marcio maximo.
Julio alikuwa sahihi kabisa kuwasilisha mshangao wake kwa watu siku ile ya jumamosi. Na nadhani alichokisema kimeendelea kuwa sahihi kabisa. Rais mstaafu alikuwa kutwa kucha akiwasifia viongozi wa taasisi kubwa kwamba wanafanya mambo makubwa!, Lakini mfano wa taasisi hizo ni hii ya tcra, ambayo tumeambiwa kuwa kwa mwaka zinapotea shilingi bilioni 400 kwa sababu tu kuna kodi nyingi ya matumizi ya ndani ya simu ambayo haikusanywi.
Nadhani afrika kwa ujumla katika karne hii haihitaji tena kiongozi mwenye uvivu wa kutopenda kusoma mambo kwa undani, kiongozi asiyedanganywa na laptop, kiongozi asiyekuwa mwepesi kusifia vitu bila ya kuenda mbali zaidi kwa maana ya kutanguliza uzalendo kwanza.
Inashangaza kumsikia mkuu kabisa wa nchi anasifia taasisi halafu cag anakuja kusema kuwa taasisi hiyo hiyo ni mzigo kwa uchumi wa taifa!. Ludovick utuoh alionekana mzigo wakati wa awamu ya nne, kumbe tatizo hakuwa yeye. Profesa assad japo aliteuliwa na rais mstaafu lakini atakuja kuwa mtu maarufu sana katika awamu ya tano, na sababu ni ushirikiano chanya atakaoupata, ushirikiano ambao mtangulizi wake utouh hakuweza kuupata.
Jamhuri kihwelu alikuwa sahihi kabisa kumshangaa mkuu wa nchi akipumbazwa na jinsi ambavyo taarifa za kazi za maximo zilivyokuwa zikiwekwa kwenye laptop. Aina hiyo ya wakuu wa nchi ambao wanayaangalia mambo kijuu juu tu, ni mzigo wa bara hili.
Wanahitajika wale ambao hawapumbazwi na vitu vidogo vidogo bali wanaangalia mustakabali mzima wa kazi yao.