James 'Whitey' Bulger: Jambazi sugu aliyehusishwa na Mafia Marekani afariki kwa njia ya kushangaza gerezani

BuletAngle

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
689
555
_104104327_gettyimages-644663366.jpg


Jambazi sugu mjini Boston James "Whitey" Bulger amepatikana akiwa amefariki katika jela moja eneo la West Virginia nchini Marekani.
Jambazi huyo mwenye umri wa miaka 89 alifikishwa katika hospitali ya gereza hilo akiwa tayari ameaga dunia muda mfupi baada ya
kuhamishwa kutoka jela la Florida.

Afisa wa muungano wa magereza ameliiambia shirika la habari la Associated Press kwamba kifo chake kinachunguzwa kama mauaji.
Maisha ya Bulger, ambaye alifungwa mwaka 2013 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya watu 11, yaliangaziwa katika filamu kadhaa.

Alikamatwa mjini California mwaka 2011 baada ya kutafutwa kwa miaka 16.
_104106662_tv050294272.jpg

CaptionWhitey Bulger alipowasili gereza la Alcatraz mwaka 1959

Kiongozi huyo wa zamani wa genge la majambazi wa mji wa Winter Hill kusini mwa Boston aliangaziwa katika filamu ya Black Mass
iliyoigizwa na Johnny Depp, na The Departed, ambazo zilishinda tuzo ya Academy kwa picha bora mwaka 2007.

Kifo chake kilitokea siku ambayo alihamishwa katika gereza la Hazelton lililopo West Virginia, ambalo lina wafungwa takribani 1,385.
Vyanzo tofauti vya habari vimeiambia Boston Globe kuwa mfungwa mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano na mafia anachunguzwa
kuhusiana na mauaji ya Bulger.

Inasadikiwa kuwa Bulger alishambuliwa vibaya na wafungwa wenzake muda mfupi baada ya kufikishwa katika gereza hilo.
Kwa mujibu wa runinga ya WFXT-TV,mjini Boston, Bulger aliuawa saa kadhaa baada ya kujumishwa na wafungwa wengine.
_104109590_hi050295846.jpg

Caption Bulger "Whitey" Bulger alipokua kijana mdogo.
_97415642_007_in_numbers_624.png


Wiki iliyopita maafisa wa magereza walikataa kutoa tamko lolote kuhusu hatua ya kumhamisha Bulger ambaye anahudumu kifungo cha maisha katika jela la Florida .
Lakini kwa mujibu wa Globe, Bulger alihamishiwa jela la Florida mwaka 2014 kutoka jela nyingine mjini Arizona baada ya uhusiano wake namshauri wake wa kike kuvutia mamlaka ya magereza.
Maelezo kuhusiana na kifo chake hayajatolewa lakini, maafisa wa magereza wameithibitishia shirika la habari la CBS kwamba kuna tukio la "mauaji" lilitokea Jumanne asubuhi.
"Haya ni mauaji ya tatu katika kipindi cha miezi saba katika gereza hili," Richard Heldreth alisema katika mahojiano ya simu."
_104107612_gettyimages-117158123.jpg

CaptionBulger na mpenzi wake Catherine Greig mjini Boston mwaka 1998.

Taarifa iliyotolewa na idara ya magereza siku ya Jumanne imethibitisha kifo chake akiwa gerezanicustody, na kuongeza kuwa shirika la upelelezi la Marekani,FBI, limeanzisha uchunguzi.

James 'Whitey' Bulger ni nani?
Bulger alizaliwa mwaka 1929 katika familia ya wamarekani wenye asili ya Ireland.
Alilelewa katika kanisa la wakatoliki wa Ireland mjni Boston, ambako alijiunga na genge la Shamrocks,
alianza kwa kuiba magari na baadaye akapanda daraja kwa kuingia kaka uhalifu wa kuiba katika benki.

_104107666_hi050295847.jpg

CaptionBulger akiwa amembeba mtoto anayedaiwa kuwa wa jambazi mwenzake.

Mara ya kwanza alikamatwa kama kama mhalifu mdogo na hatimaye aliendelea kutawala mamlaka ya uhalifu, kama vile kamari, ulaghai,
kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na mauaji.

Baada ya kushtakiwa na kuufungwa kwa kosa la wizi wa mabavu na utekaji nyara alipelekwa katika jela masarufu la Alcatraz
katika kisiwa cha San Francisco
Inasemekana aliipenda jela hilo sana kiasi cha kuitembelea akijidai kuwa mtalii wakati alipokua mafichoni.

Wakati mmoja Bulger, alijaribu kuwapatia silaha wanajeshi wa Ireland kaskazini.
Aliwahi kuwanyonga wanawake wawili kwa kutumia mikono yake na pia kumtesa mwanamume mmoja
kwa saa kadhaa kabla ya kumiminia risasi ya kichwa na kumuua

Inasemekana Bulger hakulipenda jina la utani la Whitey - ambalo lilinatokana na nywele zake nyeupe. Alipendelea kutambuliwa kwa jina la Jimmy.
Shughuli zake za kijambazi ziliimarishwa na maajenti wa wabaya wa FBI ambao walimtumia kupata taarifa kuhusiana na magenge mengine ya uhalifu.

_104107616_gettyimages-1669708.jpg

Caption Nyuso tofauti za Whitey Bulger katika picha za FBI.

William kaka yake Bulger alikuwa mwanasiasa maarufu wa chama cha Democratic na hatimaye alichaguliwa kiongozi wa wa
bunge la seneti kutoka jimbo Massachusetts mwaka 1978 na baadaye rais wa chuo kikuu Massachusetts.

Mwanasiasa huyo alikanusha madai ya kuwa na ufahamukwamba ndugu yake ni mhalifu,
lakini baadaye alikiri kuwa anampenda sana ndugu yake na kamwe hawezi kumsaliti

Bulger alikimbilia mafichoni mwaka 1995 baada ya mmoja wa maajenti wa FBI kumdokezea kwamba kuna mpango wa kumkamata.
Jambazi huyo sugu alikamatwa mwaka 2011 katika eneo la Santa Monica, California, ambako amekuwa akjificha akiwa na mpenzi
wake Catherine Greig.

Bulger alihukumiwa kifungo gerezani mwaka 2013 baada ya kupatikana na msururu wa makoso ya uhalifu,
ikiwa ni pamoja na mauaji 11 katika miji tofauti nchini Marekani katika miaka ya 1970 na 1980.

Serikali ya Marekani iliwalipa wahasiriwa waake fidia ya dola milioni 20 kwa misingi kwamba alitekeleza mauaji hayo chini ya uangalizi wa serikali
Mwaka 2015 kundi la wanafunzi lilitumia somo la historia kumuandikia waraka wa kumtaka aachane na mienendo yake mibaya.
Bulger alionekana kuguswa na waraka huo ambao ulimfanya kuonekana kujutia maisha yake ya zamani aliposema,

"Maisha yangu yameharibika kwa kuishi kipumbavu,"

 
Winter Hill gang.....
Ila huyu jamaa aliua duh alikua katili sana. Ukiangalia ile movie yake na documentary utaelewa kuna watu makatili sana duniani.

Ila alipewa kiburi na vyombo vya ulinzi maana vilimkingia kifua kwa kigezo ni informant wao!!
 
Back
Top Bottom