Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,415
2,000
Huyo bwana ni muongo sana, Magufuli kwa alivyoamuru Lema asote rumande miezi minne yote bila dhamana kinyume kabisa cha sheria na akaamuru Sugu afungwe jela bila hata kosa sasa kuamuru akina Rugemalira wafutiwe kesi ndio angeshindwa.

Magufuli huyu huyu ndiye aliyeamuru wale wabunge wa Chadema watiwe hatiani na wakalimwa faini kubwa hata bila kosa lolote, sasa kuwafutia kesi akina Ruge ndio angeshindwa..!!

Acheni ushabiki wa kijinga, wakati wa utawala wake, Magufuli alikuwa akizitumia mahakama kuwakomoa wabaya wake jambo ambalo Mwenyezi Mungu alilichukia sana na akaamua kumshushia rungu.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy

Qwy

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
5,513
2,000
Sasa unataka kusema Magufuli ndio anaendesha kesi ama?

Wakati mara kadhaa alikuwa akimuagiza DPP kufuta kesi ambazo hazina ushahidi wakutosha.

Au we mwenzetu ulikuwa kuziwi usikii.
Hakuna aliyekuwa na uwezo wa kupinga utashi wa Jiwe, kama watu waliuawa, walishambuliwa kwa silaha za moto, watu walipotea na vyombo vya dola viliogopa kuchunguza kwa kuwa walijua ni directives kutoka kwa mkulu DPP angethubutu wapi kukinzana naye.
Jiwe hasafishiki hata mfanyeje, madhila aliyosababisha ni makubwa mno na majeraha aliyowaachia baadhi ya watu hayatapona maisha yao yote. Inaumiza sana watu waliteswa na kuuawa(by direct or indirect order) kutoka kwa Jiwe lakini kuna baadhi ya wanufaika wa mateso, unyang'anyi na mauaji yaliyofanyika wakati wa utawala wake wakijitutumua ku justify udhalimu wake.
Utawala wa Jiwe judiciary na bunge havikuwa huru kabisa, no wonder katiba mpya inapigiwa kelele sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom