James Ole Milya awa kivutio michuano ya wabunge inayoendelea jijini Arusha

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
187
442
Mbunge mstaafu wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara,James Ole Milya leo ameonekana kivutio katika michuano ya wabunge wa Afrika Mashariki inayorindima katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Ole Milya alionekana muda mwingi akiwa amevaa bendera ya Tanzania huku akiwa ameshika vuvuzela mkononi huku akiwaongoza wabunge wa Tanzania kushangilia ushindi kitendo kilichowavutia watu mbalimbali uwanjani hapo.

Tukio hilo limeibua hisia mbalimbali kwa baadhi ya watu uwanjani hapo ambapo Ole Milya alikuwa ni mbunge pekee mstaafu ambaye aliungana na wabunge wa Tanzania katika michuano hiyo kitendo kilichowavutia baadhi ya wabunge akiwemo waziri wa michezo nchini,Innocent Bashungwa.

Ole Milya ameonekana kuungana na wabunge mbalimbali wa bunge la Tanzania ambao walikuwa wakishiriki mashindano mbalimbali katika michuano hiyo.

Mara baada ya wabunge wa Tanzania upande wa wanawake kupata ushindi katika mchezo wa kuvuta kamba baada ya kuishinda timu za Uganda na EALA Ole Milya alionekana akijumuika na kushangilia ushindi na wabunge hao.

Ole Milya anayetajwa kuwania ubunge wa jumuiya ya Afrika Mashariki amekuwa kivutio kwa wabunge mbalimbali ambapo baadhi yao walionyeshwa kufurahia ujio wake uwanjani hapo pamoja na kwamba kwa sasa sio mbunge wa bunge la jamhuri la Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo kitendo cha Ole Milya kuungana na wabunge hao kimewakosha baadhi ya wabunge ambapo baadhi yao wamemtaja kama mzalendo anayependa maendeleo ya michezo hapa nchini.

Hatahivyo Ole Milya baada ya kuulizwa kuhusu ushiriki wake uwanjani hapo alisema kwamba yeye mbali na kuwa mbunge mataafu bado anabaki kuwa Mtanzania na mzalendo na popote bendera ya Tanzania inapopeperushwa atafika kutoa sapoti bila kusubiri.

Mwisho...

5B84B95F-86B7-4388-83DE-EE9D312663C4.jpeg

43C306BA-1D82-42E7-9EB5-99A4888468E0.jpeg

A7884A8D-657A-47BF-9145-E048DBAED295.jpeg

26A5C629-E99A-440A-88B1-002A6550AD2F.jpeg

7F885FCB-9252-4F31-8C05-5E155F6A2661.jpeg

BA417E5A-DD65-4DE0-9ACE-029A79B1C25C.jpeg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom