James ole Millya, Mawazo na Bananga wapokelewa kwa shangwe Jimbo la Lushoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

James ole Millya, Mawazo na Bananga wapokelewa kwa shangwe Jimbo la Lushoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbelwa Germano, May 26, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima Mkuu,

  Kamanda James ole Millya akiongozana na Makamanda wengine Kamanda Mawazo (diwani wa CCM wa kata ya Sombetini aliyejiunga na CDM), pamoja na mjumbe wa zamani wa UVCCM Arusha Kamanda Bananga jana walipokelewa kwa shangwe na wananchi wa jimbo la Lushoto katika mkutano wa hadhara uliofanyika karibu na benki ya NMB.

  Aidha Kamanda Millya alifungua matawi matano (kitivo,Milemeleni, dochi (tawi la wanafunzi wa IJA), na matawi wawili eneo la Magamba). Baada ya ufunguzi wa matawi kamanda Millya alikuwa na mazungumzo na wanafunzi wa chuo kishiriki cha Tumaini (Sebastian Kolowa) na kugawa vyeti kwa wanachama wa CDM wanaotarajia kumaliza chuo mwezi wa saba.

  Kivutio kikubwa ilikuwa kwa Mama mmoja mashuri aitwaye kighenda ambaye alidata na maneno ya Kamanda Bananga na kuanza kuhamasisha kwa nguvu wanawake kuunga mkono CDM.Kamanda Millya alisema amefurahihwa na ujio ule kwani hakutegemea kupata mapokezi makubwa.Kamanda Mbelwa aliongoza mashambulizi ya uhamasishaji kwa kushirikiana na Katibu wa Wilaya kamanda Kisandu.

  Kamanda Millya na wenzake waliondoka jana jioni kuelekea kwenye mkutano wa CDM akienda kuungana na makamanda Mbowe, Dr.Slaa na wengine.

  Viva CHADEMA!
   
 2. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sorry ni Bananga
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  weka picha.
   
 4. h

  hans79 JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Hata kama hujaweka picha taarifa yako yajieleza, ila kwa kama utaweza ziweke hizo picha.
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Huyu dada kighenda ni wa zamani sana umenikumbusha mbali sana sana kumbe bado yupo?
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Mbelwa.Taarifa yako imetulia sana.Mimi ndiyo naelekea Jangwani
   
 7. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kanzi nzuri,ila lushoto karibu na bank ya nmb hakuna kiwanja hebu niweke sawa hapo
   
 8. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mbelwa katika ujenz wa chadema tanga nimeanza kukuba bro, hiyo id ni jina lako halisi?
   
 9. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni eneo mbele ya benki ya NMB mkuu karibu na soko kuu
   
Loading...