James Millya pamoja na genge lake anapanga mipango ya kuvuruga uchaguzi wa CCM mkoa wa Arusha

Kigaila Mwandishi

New Member
Sep 23, 2022
2
0
Na Mwandishi wetu,
Arusha.

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe James Millya pamoja na genge lake anapanga mipango ya kuvuruga uchaguzi wa CCM mkoa wa Arusha kama mgombea wake anayegombea UNEC hatoshinda.
Taarifa kutoka kwenye genge hili la kina James Millya zinasema kuwa kwenye vikao mbalimbali ambavyo wamekuwa wakiendelea navyo kwenye wilaya mbalimbali za mkoa wa Arusha hasa kwenye jamii za kimasai pamoja na kufanya siasa za kikabila na matumizi makubwa ya fedha na kuwatukana wagombea wenzao.
Chanzo chetu kinaendelea kusema kuwa Chama mkoa wa Arusha ni kama hawaoni wala kusikia haya mambo yanayoendelea yakiongozwa na James Millya.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Arusha kwa nyakati tofauti wamekuwa wakilalamika kuwa huyu James Millya anaenda kukivuruga tena Chama mkoa wa Arusha kwasababu haaminiki hata kidogo kwasababu hata siku za nyuma ni kati ya watu waliowasumbua baada ya kuongozwa na tamaa zake binafsi na kuhamia upinzani,na wakaendelea kusema kuwa angekuwa na uchungu sana na CCM angeenda kukipambania chama hiki kwenye mkoa wake wa manyara.
Mjumbe mwingine aliendelea kwa kusema kuwa Mbunge huyu wa bunge la Afrika Mashariki ndiye kinara wa kutoa rushwa za mgombea wa UNEC mkoa wa Arusha bwana Sendeu Laizer,na wameendelea kudai kuwa wakati akiwa anatoa fedha hizo amekuwa akiwaambia kuwa yeye ni bingwa wa kupindua meza hivyo wasiwe na wasiwasi.
Mjumbe mwingine kutoka kwenye kundi hili ameendelea kusema kuwa James Millya baada ya kuona kuwa uwezekano wa Mgombea wao ndugu Sendeu Laizer hawezi kupata kura wilaya ya Arusha mjini ameamua kumuita Ally Bananga kutoka Dar Es salaam ili akawasaidie kutafuta kura Arusha kwa malipo na sio kwa maslahi ya CCM,mjumbe huyu anasema kuwa Ndugu Ally Bananga alitumiwa 2,000,000 na James Millya na fedha ilitoka kwa Sendeu Laizer.
Chanzo hiki kinaendelea kusema kuwa watu hawa waliotoka upinzani lengo lao kuu ni kuwaweka mamluki ambao badala ya kuunganisha chama mkoa wa Arusha wanaenda kukipasua vipandevipande na hivyo hata kwa chaguzi zijazo CCM itaenda kupoteza na katika maoni yao wamesema kuwa CCM mkoa wa Arusha kina wajibu wa kumfuatilia na kumuonya James Millya kuwa anachokifanya ni kitu ambacho hakina afya kwa Chama hiki kikongwe na hakuna aliye mkubwa kuliko CCM.
Wajumbe hawa wakaendelea kusema kuwa kwa kitendo cha Chama Cha Mapinduzi kumpa James Millya nafasi ya kuwakilisha Nchi kwenye bunge la Afrika Mashariki isiwe sababu ya yeye kujiona ni mkubwa kuliko CCM na kuwa anaweza kufanya chochote au kupanga safu anavyotaka.
WanaCCM wanahitaji muunganiko na msimamo thabiti kwa ajili ya kukijenga chama hiki na kuhakikisha kuwa kinatekeleza Ilani ya Uchaguzi kikamilifu.
Hivyo pamoja na kuwa James Millya anasubiri kuapishwa kuwa Mbunge wa Africa Mashariki kuna umuhimu wa Chama kutizama nafasi hii waliyompa kwasababu anaitumia vibaya kwa kutengeneza matabaka ya kikabila kitu ambacho sio utamaduni wetu WanaCCM hivyo ni bora Chama kikamtafuta mtu mwingine mwenye uwezo wa kuwaunganisha WanaCCM na Watanzania kwa ujumla wake.
 

Attachments

  • images.jpeg.jpg
    images.jpeg.jpg
    26 KB · Views: 5

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom