James Mbatia: Viongozi wengi wa Serikali wamekumbwa na upunguani wa uelewa wa mambo

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi bwana James Mbatia akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo hii ametolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye hotuba ya Rais na kauli ya Spika Job Ndugai

Mosi, Suala la akiba ya pesa za kigeni ameiomba serikali wabadili kauli yao ya kuwa tuna dola za marekani bilioni elfu sita yaani kimahesabu ni trilioni sita, China tu kama Taifa lenye pesa nyingi za kigeni wana dola za marekani trilioni tatu tu

Mheshimiwa Mbatia amesisitiza mahesabu ni tatizo kubwa sana kwa viongozi wetu kwani hata pesa za mkopo wa uviko wanazojengea vyoo vya wanafunzi wanamshukuru Rais kwa msaada wakati hilo ni deni la Taifa, Hata Rais akiondoka kama alivyoondoka Magufuli na deni kubwa la Taifa, Deni la Taifa ameliacha kwa wananchi na serikali yao

Wananchi ndio watatakiwa kulipa madeni haya tena kwa pesa za kigeni, Hivyo James Mbatia anashangaa Rais kusema Tutaendelea kukopa bila kuangalia nani atalipa madeni haya ambayo pesa zake hazizalishi kitu, Mbatia amesisitiza ni lazima kuangalia uwezo wa wananchi kulipa madeni hayo

James Mbatia, Ni aibu kwa viongozi karne hii ya ishirini na moja kujenga vyoo kwa pesa za mkopo wa uviko halafu wanaandika kwenye ukuta wa Choo "Ahsante uviko 19" kama jambo la Furaha kumbe ni vichekesho

James Mbatia, Ni aibu viongozi wa serikali toka ngazi ya Taifa mpaka kata kila wakati kusema ahsante Rais umetoa pesa za flyover, mara barabara mara afya wakati ni pesa za watanzania na hata kama ni mkopo ni deni la watanzania. Rais yeye hana pesa za kujenga barabara au flyovers labda kama Rais anauza madawa ya kulevya

Pili, Ni upunguani umeshajijenga na tunazidi kuharibu watoto wa Taifa hili kutokana na upunguani wa viongozi wetu ambao wanashindwa kuelewa maana ya mkopo na deni la Taifa, James Mbatia amesisitiza baada ya watu kujibu hoja za Job Ndugai wao wanatafuta personal attack kwa Ndugai

James Mbatia, Anasisitiza upunguani wa viongozi ndio unapelekaea watu kushindwa kujibu hoja na kukimbilia kumtukana Job Ndugai, Tatizo la upunguani linawafanya viongozi washindwe kupima hoja kama Job Ndugai amekosea, Je usahihi ni upi amehoji bwana Mbatia

Tatu, James Mbatia amesisitiza somo la hesabu hata Bungeni ni tatizo kwa wabunge wengi sana, Ndio maana mambo yanaposomwa kuhusu hesabu wengi hawaelewi, James Mbatia amesisitiza Kuwa viongozi wanaandaliwa
 
Kwakweli inashangaza sana fedha za mkopo wanajengea madarasa na vyoo

Wakati tuliambiwa tozo hiyo ndio kazi yake.

Tozo inatumika katika nini???

Kwanini serikali badala ya kujikita katika kukusanya mapato inakimbilia kukopa tu??

Kwanini serikali inawaogopa wafanyabiashara mpaka wakipandisha bei kiholela ipo kimya tu??

Je ndio tuseme kwamba wafanyabiashara ndio wanaoongoza nchi kwa sasa??
 
Punguani mkuu namjua😁😁😁
mnuy65432.jpg
 
Hoja zako nzuri sana zina mashiko.....
kuna wakati huwa nawaza sijui tumerogwa !!
ama hatujielewi
 
Kwakweli inashangaza sana fedha za mkopo wanajengea madarasa na vyoo

Wakati tuliambiwa tozo hiyo ndio kazi yake.

Tozo inatumika katika nini???

Kwanini serikali badala ya kujikita katika kukusanya mapato inakimbilia kukopa tu??

Kwanini serikali inawaogopa wafanyabiashara mpaka wakipandisha bei kiholela ipo kimya tu??

Je ndio tuseme kwamba wafanyabiashara ndio wanaoongoza nchi kwa sasa??
Naona dishi limekukaa sawa sasa 🤣
 
Mbatia siku hizi kama kachanganyikiwa tu, sijui ni uzee,, kutwa kudandia viishu visivyo na kichwa wala mguu.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
James Mbatia, Ni aibu kwa viongozi karne hii ya ishirini na moja kujenga vyoo kwa pesa za 7mkopo wa uviko halafu wanaandika kwenye ukuta wa Choo "Ahsante uviko 19" kama jambo la Furaha kumbe ni vichekesho
 
Back
Top Bottom