James Mbatia: Tuna viongozi mapunguani hapa Tanzania

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Kuna wanasiasa Mapunguani neno punguani ni mtu asio na akili sahihi, tumekuwa tunazungumzia Muafaka wakitaifa kuna wanasiasa mapunguani kabisa wanadhani ni kukaa mezani kugawana madaraka na vyeo, sisi tunataka Muafaka kwaajili ya nchi yetu, Machinga, Mama mjamzito, Elimu yetu.

Msajili wa vyama akatangaza kwamba shughuli za vyama zisimame kwa muda japo mamlaka haya hana ila kesho yake chama cha Mapinduzi wakaanza ziara Kanda ya kusini na Msajili akanyamaza kimya, huu ubaguzi huu hauvumiliki na ubaguzi huu ni upunguani kabisa.

James Francis Mbatia
M/kiti NCCR-Mageuzi

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli ofisi ya msajili lazima itakuwa imejaza punguani wengi sana. Mambo wanayofanya, tena yaliyo kinyume cha katiba, hakuna mwenye akili anaweza kufanya. Ni punguani pekee yake ndiyo anaweza.

Wewe fikiria mtu anataka mfanye kikao kujadiliana kama mfuate sheria au muivunje. Huyo atakuwa mzima?
 
Kwa kweli ofisi ya msajili lazima itakuwa imejaza punguani wengi sana. Mambo wanayofanya, tena yaliyo kinyume cha katiba, hakuna mwenye akili anaweza kufanya. Ni punguani pekee yake ndiyo anaweza.

Wewe fikiria mtu anataka mfanye kikao kujadiliana kama mfuate sheria au muivunje. Huyo atakuwa mzima?
Hiyo ofisi ya maafisa vipenyo-ccm. Inajua harakati zozote za mabadiliko hazitaiacha salama hiyo ofisi.
 
Mbatia tafadhali! Siyo wanasiasa wote ni mapunguani!! Kwa mujibu wa Haji Manara LABDA wanasiasa ambao ni mashabiki wa yanga!! Msikieni wenyewe hapa!! Mnaomwelewa tuelewesheni!

 
Binafsi anayosema ni Kweli ingawa na yeye kuna kipindi huwa namuweka kwenye kapu moja na hao wenzake.
Nasikia aliambiwa atapewa majimbo, akakengeuka🤣
images (3) (17).jpeg
 
Anatamani sana muafaka wa kisiasa!! Ila sijui kama ni anajiona kama tunavyomwona!! Mbabaishaji flani vile!! Maneno mengi vitendo sifuri!!
Kuna siku alimind sana.pale Msimbazi baada ya kuzuiliwa kufanya kikao cha ndani. Aliwabwatukia wote Rais, RC, Waziri na genge loote la maccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom