James Mbatia: "Sisi tumeamua Kuwasamehe Wale wote Waliohusika na Mauaji ya DR.MVUNGI.

Kamanda Francis

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
834
140
Akizungumza Kwenye Ibada Maalum ya Kumwombea Dr.Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi JAMES MBATIA amesema Wao wameamua Kuwasamehe wale Wote waliohusika na Mauaji ya Dr.Mvungi... Chanzo: ITV Habari.
 
Mbatia naye mambo yake kama Mandela!!! Nani kampa mamlaka ya kusamehe watu walioa baba wa familia? Anadhani Mvungi yuko more of NCCR than his family!!!

Kama tumeamua hii ni dunia ya kusamehesamehe tu bora tufunge mahakama sasa.
 
wanawajua ni wakina nani usikute hawajui ndo maana wamewasamehe wao wanasamehe wauaji jk alisamehe wezi wa epa yani huu ushirikiano unakolea je akiwa rais wezi nao atawasamehe?
 
Lakini Jamhuri haitawasamehe kamwe, mkondo wa sheria utafuatwa na mwisho wahuni wote waliofanya ule unyama watachukuliwa hatua muafaka!
 
Mbatia naye mambo yake kama Mandela!!! Nani kampa mamlaka ya kusamehe watu walioa baba wa familia? Anadhani Mvungi yuko more of NCCR than his family!!!

Kama tumeamua hii ni dunia ya kusamehesamehe tu bora tufunge mahakama sasa.

bila kusahau magereza. Anadhani nccr walikuwa wanammiliki dr mvungi, wanasahau ana mke, watoto, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Abarikiwe...
Familia yake na wenye uchungu na kifo chake twataka haki itendeke.
Hata Mungu hasamehi wenye dhambi wasipotubu.
 
Lakini Jamhuri haitawasamehe kamwe, mkondo wa sheria utafuatwa na mwisho wahuni wote waliofanya ule unyama watachukuliwa hatua muafaka!

Kwa bomu la Arusha kwenye mkutano wa CHADEMA,mateso ya Ulimboka,wauaji wa Professor Mwakyusa getini kwake,mateso kwa Kibanda etc,mkono wa serikali una urefu wa birika??!! Wacheni propaganda za kipumbavu!!!
 
Mbowe kaambiwa apeleke video ya warusha bomu akagoma, ile video ingerahisisha kumbaini muhalifu mapema zaidi. Otherwise polisi bado wanaendelea na uchunguzi. Naye akipatikana hatua za kisheria lazima zifuatwe!
 
Mbowe anasubiri apeleke video hiyo mahakamani na wala siyo polisi au ikulu kwa kuwa polisi na ikulu ndio watuhumiwa namba moja.
 
Kusamehe ni wajibu wetu kama wanadamu na si mamlaka. "safisha ubongo ondoa mavi hayo"
 
Back
Top Bottom