Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,092
========
Mtangazaji: Wewe umeuonaje mpka sasa uongozi wa Mama Samia Suluhu Hassan?
James Mbatia: Ndugu Samia Suluhu Hssan aliingia madarakani ile tarehe 19/03/2021 na akala kiapo kwa taratibu ambazo zimeweka na akatoa ahadi ambazo tuliamini kwamba atazitekeleza na akatoa ahadi ya kukuza demokrasia hapa Tanzania na kukuza uchumi maana alikili kuwa uchumi uchumi wetu umeshuka.
Katika kuleta maendeleo endelea aliahidi kuliponya Taifa, kuponya majeraha yaani kulileta Taifa pamoja, lakini badala ya kulileta Taifa pamoja ameanza kulipalanganya tena, kwa mfano kauli yake aliyoitoa Morogoro kwamba kuna watu wamenza kuleta chockochoko, kuzungumza maedneleo ya nchi yako au kuwa na mawazo mbadala sio chokochoko ile ya kusema kwamba tujenge uchumi kwanza wakati yeye mwenyewe ametuandikia kwamba atakaa na wenzeke wana siasa tuzungumze madhila yaliyotokea huko nyuma na namna gani ya kulileta Taifa pamoja.
Mama aliahidi na ahadi ya muungwana ni vitendo usipojenga uaminifu watu wakishaanza kukushuku, ameongea na vijana. wazee, wakina mama na viongozi wa dini tunampongeza, amefika kwa wanasiasa anasema tusubiri kwanza tujenge uchumi, tujenge nchi Hayati Magufuli naye alisea hivyohivyo kuwa subirini nanyoosha nchi najenga uchumi. Yeye ameingia madarakani anasema uchumi umesinyaa, uchumi una hali mbaya ndiyo hayo mambo ya tozo anaweka sasa uchumi uko kwenye hoi bin taaban.
Namshauri ndugu Rais kuwa rasilimali iyokubwa kuliko zote duniani ni rasilimali watu. Rasilimali kubwa zaidi ni kuleta watu pamoja kwa ajili ya maendeleo endelevu alete watu pamoja. Lakini sisemi hivyo ila wapo vijana, swala la vijana kukosa ajira, umasikini uliokithiri na swala la tabaka la kubwa la watu kuwa hawana kitu na watu wache kuwa nacho. Pia swala la watu wengine kujina kama wao ndio wenye haki zaidi ukiwa upinzani wanakuona kama daraja la pili la kwanza ni wa chama tawala.
Tunaona Waziri Mkuu anafanya mikutano ya hadhara, Rais anafanya mikutano ya hadhara, sekretarieti ya CCM inafanya mikutano ya hadhara ila upinzani mnaambiwa mikuta ya hadhara hairuhusiwi hii nchi itakuwa ya aina gani? Mambo kama haya yanazidi kuligawa Taifa. Kariakoo imeungua moto ni majanga kwenye taifa, shule zinaungua moto ni majanga kwenye taifa na hatijaambiwa vizuri huku tuna COVID 19 mambo kama haya yanazidi kuleta chuki kwenye Taifa na watu watafany avitendo visivyostahili. Mtendee mwingine kama unavyotaka kutendewa.