James Mbatia (NCCR) amnyang'anya Kafulila nafasi ya U-katibu Mwenezi!

Hata hivyo Leo saa Kumi Hamadi rashid anafungua tawi la CUF kata ya Mabibo -eneo la CHECHINIA sijui kama watapona maana Blugad wameaagizwa kwenda hapo!!!

Hilo tawi kafungua? Au imekuwa kama jana pale Manzese. Seif kiboko, nchi nzima chama hakuna kufanya mkutano hadi aidhinishe yeye na bado tunasema hicho ni chama. Kazi tunayo.
 
Taarifa zilizonifikia Punde ni Kwamba , Jemus Mbatia wa NCCR amemunyang'anya David Kafulila Cheo Cha Ukatibu Wenezi kama Mandalizi ya kumunyang'anya kati na Kukosa Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini mapema February Mwakani. Taarifa kutoka kwa Katibu mkuu Ruhuza inasema ,Barua ya tukio hilo imekabidhiwa kwa mhusika leo mapema!!!

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na Mbatia zinaonyesha kuwa tayari mpango umesha sukwa na CCM kwamba jimbo hilo lirudi mikononi Mwa CCM wakati Mbatia Mwenyewe anajiandaa kupewa ubunge kupitia Afrika Mashariki.

Mpango wa Mbatia unalenga kumuondoa David Kafulila katika Ujumbe wa Halmashauli Kuu ambayo itaketi February Mwakani ambapo tayari Wajumbe hao walisha mpa Mbatia Siku 21 kujieleza juu ya tuhuma za Kibaraka wa CCM.

Kutokana na kafulila Kunyang'anywa Kadi hana sifa ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mbatia na Kwamba mpango wa kumunyang'anya kadi Kafulila utatekelezwa badala ya kumuondoa Mbatia.

Wajumbe Wengi wa Halmashauli Kuu ambao wengi ni wa kuteuliwa na Mbatia wamesha pitiwa na Mulungula wa CCM kumumaliza Kafulila!!!
Mgogoro wa Ubunge Afrika Mashariki Bado unafukuta Ndani ya NCCR ambapo Msaidizi wa Mwenyekiti Danda JUJU naye anautafuta kwa nguvu kiasi cha Kutofautiana na Jemus Mbatia.

Kutokana na Mkakati huu Hali ndani ya NCCR ni tete sambamba na Hali ya CUF ambapo tatizo kubwa ni kuunga mkono CCM

Mwezi uliopita Seif aliitisha kikao Pemba kwenye jimbo la Hamadi Rashid na kuandaa Njama za Kumunyang'anya Kadi Hamadi Rashid lakini njama hizo zikafichuliwa na Blueguard wanao muuunga mkono Hamadi rashid

Bifu hilo limesababisha Seif kutoka Pemba na sasa yupo Lindi kufanya kampeni za Kumuchafua Hamad Rashid huku akipiga Marufuku vikao vyote vya CUF ngazi zote isipokuwa kwa Kibali chake!!
Seif kaandika barua ambayo imesainiwa na Mketo na mabox ya barua hizo yapo makao CUF yanasubiri kwenda mikoani.

Barua hiyo inawataka viongozi wote wa CUF nchi nzima wasifanye mikutano bila kibali cha Seif.

Waraka huo ndio ulimufanya Julias Mtatilo jana kuzuia Ziara ya Hamad Rashid tawi la Kosovo Manzese .

Hata hivyo Leo saa Kumi Hamadi rashid anafungua tawi la CUF kata ya Mabibo -eneo la CHECHINIA sijui kama watapona maana Blugad wameaagizwa kwenda hapo!!!

King King,
Sasa nimekufahamu vizuri, I see!
 
Uroho wa madaraka unawatafuna Kafulila na mwenzake Hamad Rashid walishirikiana na CCM kubadili tafsiri ya Kambi rasmi ya upinzani leo wenzao wanashirikiana na CCM kuwaengua madarakani ndani ya vyama vyao. Ndugu wakigombana..............................................
 
Kafulila nakuonea huruma ,siku zote binadamu yoyote anaetaka madaraka kwa mkato ni lazima anyolewe
 
Kimsingi, nawapongeza viongozi wa nccr kwa kumvua ukatibu mwenezi kafulila,hii ni kwa sabubu amejifanya anamtuhumu mwenzake huku akijua kuwa yeye ni sehemu ya matatizo ya chama, hii iko wazi kwa kuwa kafulila ameshindwa kuitumikia nafasi hiyo, hivi tujiulize ni nani aliyekuwa anajua kuwa Kafulila ni Katibu mwenezi wa NCCR taifa?jibu ni rahisi, hakuna na iwapo wapo ni wachache ndani ya nccr,sasa tujiulize iweje msemaje wa chama hajulikani halafu tumtetee kuwa ni mchapakazi?huo utakuwa ni uhuni kwa wale wote wanaomtetea kafulila,tumekuwa tukishuhudia na kusikia kuwa makatibu wenezi wa vyama vingine wakizunguka nchi nzima kueneza vyama vyao,Je kafulila alikuwa wapi?Kwa maoni yangu katibu mkuu wa nccr taifa alichelwa kumuondoa katika nafasi hiyo,hakuwa na umuhimu wowote zaidi ya kuchochea migogoro ili awe mwenyekiti .
Big up NCCR kwa kumshughurikia bwana migogoro Kafulila, nashauri kumvua hata uanachama, kumuacha kuendelea kuwa mwanachama wenu mtakuwa mmeonesha utovu wa nidhamu,fukuzeni kabisa kirusi hichoooooooooooooooooo
 
Taarifa zilizonifikia Punde ni Kwamba , Jemus Mbatia wa NCCR amemunyang'anya David Kafulila Cheo Cha Ukatibu Wenezi kama Mandalizi ya kumunyang'anya kati na Kukosa Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini mapema February Mwakani. Taarifa kutoka kwa Katibu mkuu Ruhuza inasema ,Barua ya tukio hilo imekabidhiwa kwa mhusika leo mapema!!!

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na Mbatia zinaonyesha kuwa tayari mpango umesha sukwa na CCM kwamba jimbo hilo lirudi mikononi Mwa CCM wakati Mbatia Mwenyewe anajiandaa kupewa ubunge kupitia Afrika Mashariki.

Mpango wa Mbatia unalenga kumuondoa David Kafulila katika Ujumbe wa Halmashauli Kuu ambayo itaketi February Mwakani ambapo tayari Wajumbe hao walisha mpa Mbatia Siku 21 kujieleza juu ya tuhuma za Kibaraka wa CCM.

Kutokana na kafulila Kunyang'anywa Kadi hana sifa ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mbatia na Kwamba mpango wa kumunyang'anya kadi Kafulila utatekelezwa badala ya kumuondoa Mbatia.

Wajumbe Wengi wa Halmashauli Kuu ambao wengi ni wa kuteuliwa na Mbatia wamesha pitiwa na Mulungula wa CCM kumumaliza Kafulila!!!
Mgogoro wa Ubunge Afrika Mashariki Bado unafukuta Ndani ya NCCR ambapo Msaidizi wa Mwenyekiti Danda JUJU naye anautafuta kwa nguvu kiasi cha Kutofautiana na Jemus Mbatia.

Kutokana na Mkakati huu Hali ndani ya NCCR ni tete sambamba na Hali ya CUF ambapo tatizo kubwa ni kuunga mkono CCM

Mwezi uliopita Seif aliitisha kikao Pemba kwenye jimbo la Hamadi Rashid na kuandaa Njama za Kumunyang'anya Kadi Hamadi Rashid lakini njama hizo zikafichuliwa na Blueguard wanao muuunga mkono Hamadi rashid

Bifu hilo limesababisha Seif kutoka Pemba na sasa yupo Lindi kufanya kampeni za Kumuchafua Hamad Rashid huku akipiga Marufuku vikao vyote vya CUF ngazi zote isipokuwa kwa Kibali chake!!
Seif kaandika barua ambayo imesainiwa na Mketo na mabox ya barua hizo yapo makao CUF yanasubiri kwenda mikoani.

Barua hiyo inawataka viongozi wote wa CUF nchi nzima wasifanye mikutano bila kibali cha Seif.

Waraka huo ndio ulimufanya Julias Mtatilo jana kuzuia Ziara ya Hamad Rashid tawi la Kosovo Manzese .

Hata hivyo Leo saa Kumi Hamadi rashid anafungua tawi la CUF kata ya Mabibo -eneo la CHECHINIA sijui kama watapona maana Blugad wameaagizwa kwenda hapo!!!

wewe ni mtanzania? napata mashaka kwa kiswahili chako!
 
Vigezo saba vya kwanini mbatia ni kibaraka wa ccm. 1.mwaka 2003 alifungua kesi kuweka pingamizi dhidi ya wagombea wa cuf pemba na kusababisha upinzani kupoteza majimbo sita kwa kura ya maruhani. 2.mwaka 2007 baada ya slaa kutangaza orodha ya mafisadi alisema watanzania wote ni isipokuwa wanatofautiana viwango.3.baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 cuf walipokataa kumtambua karume kwakuwa uchaguzi haukuwa huru na haki mbatia alisema kutomtambua karume ni uhaini. 4. Mwaka 2010 kwenye uchaguzi alimwambia mgombea urais wake asiseme sisiemu vibaya kwenye kampeni na jk alipokwenda kawe akakutana na upinzani dhidi ya ccm akasema "kama hamwezi kumpa kura mgombea wa sisiemu ni bora mpeni mbatia kuliko hawa cdm watu wasiotakia mema nchi yetu. 5.baada ya uchaguzi aliposhindwa na mdee akiwa mshindi wa tatu amekwenda mahakamani kupinga matokeo wakati ameshindwa kwa zidio la kura elfu33 6.
 
Hakuna shaka mbatia analipwa na ccm, na mpaka sasa ushahidi uliopo wakati wa kampeni amelipwa chek ya milioni 80 mara nne. Hizo ndizo zenye ushahidi wa nyaraka. Nisingependa kuziweka jamvini kwasasa kwakua huo ni ushahidi utakaowasilishwa mahakamani februari 2012 kesi itaposomwa tena. Misimamo yake sio bure, ndio maisha yake mjini hapa. Sasa kwa kafulila ninaemjua hana uvumilivu na mafisadi. Uliona aliwataja akina zambi bungeni mpaka kesho spika anapotezea. Hataki kutupa majibu yamefikia wapi. Mbatia ana bahati mbaya sana. Huyu dogo hana chembe ya woga anapofanya maamuzi.
 
mbatia ni mfano wa mtu asie penda challenges..kafulila wakimtoa nccr ataenda chadema ..wanaweza wakampokonya kadi akahamia chadema na wananchi wa kigoma kusini ndio wenye final say na wanaweza waka waumbua MBATIA na genge lake la kihuni
Sidhan kama chadema wanahitaji sisimizi wakati huu
 
Vigezo saba vya kwanini mbatia ni kibaraka wa ccm. 1.mwaka 2003 alifungua kesi kuweka pingamizi dhidi ya wagombea wa cuf pemba na kusababisha upinzani kupoteza majimbo sita kwa kura ya maruhani. 2.mwaka 2007 baada ya slaa kutangaza orodha ya mafisadi alisema watanzania wote ni isipokuwa wanatofautiana viwango.3.baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 cuf walipokataa kumtambua karume kwakuwa uchaguzi haukuwa huru na haki mbatia alisema kutomtambua karume ni uhaini. 4. Mwaka 2010 kwenye uchaguzi alimwambia mgombea urais wake asiseme sisiemu vibaya kwenye kampeni na jk alipokwenda kawe akakutana na upinzani dhidi ya ccm akasema "kama hamwezi kumpa kura mgombea wa sisiemu ni bora mpeni mbatia kuliko hawa cdm watu wasiotakia mema nchi yetu. 5.baada ya uchaguzi aliposhindwa na mdee akiwa mshindi wa tatu amekwenda mahakamani kupinga matokeo wakati ameshindwa kwa zidio la kura elfu33 6.

Kweli Mbatia ni pandikizi la CCM!
 
Kafulila aenguliwa Uenezi NCCR Mageuzi Send to a friend
Monday, 12 December 2011 20:39
0digg

Leon Bahati
KATIBU Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza amemuengua kwenye nafasi ya Katibu Mwenezi, David Kafulila ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kusini.Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa Kafulila ameondolewa kwenye nafasi hiyo kutokana na tofauti za kimsimamo baina yake na Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizothibitishwa na Kafulila mwenyewe, Ruhuza alichukua hatua hiyo kwa mamlaka aliyopewa na katiba ya NCCR-Mageuzi.

Jana Ruhuza alikiri kumwondoa madarakani mbunge huyo machachari, lakini akasema hatua hiyo haikutokana na mivutano ya kimsimamo baina yake na Mbatia.

"Ni mabadiliko tu ya kawaida ndani ya chama…Nimempa fursa kwa kumpunguzia majukumu ili afanye kazi vizuri zaidi katika jimbo lake," alisema Ruhuza.

Alisema kuwa mabadiliko hayo yalitokana na vikao vya chama ingawa hakueleza ni lini vikao hivyo vilifanyika wala tarehe aliyomuandikia barua Kafulila kumuarifu juu ya uamuzi huo.

"Ni muda mrefu sana. Kwa hapa sikumbuki ni lini nilimuandikia. Lakini muulizeni yeye," alisema Ruhuza akifafanua kuwa mtu atakayechukua nafasi hiyo atatangazwa wakati wowote kuanzia leo.

Mwananchi lilipowasiliana na Kafulila, alikiri kupokea barua hiyo ya kusimamishwa uongozi, lakini akasema kitendo hicho hakikumuhuzunisha kwa sababu kofia aliyo nayo ya ubunge, ni zaidi ya hiyo ya uenezi.

"Nafasi ya ubunge ni ya juu zaidi ikilinganishwa na ya vyeo ndani ya chama. Ndiyo maana hata Mwenyekiti (Mbatia) pamoja na nafasi ya juu ya chama aliyonayo, alikuwa anataka kuwa mbunge, lakini akashindwa," alisema Kafulila.

Alipoulizwa sababu ya kufukuzwa kwake alisema barua hiyo haijaweka wazi suala hilo, lakini akakiri kuwa kuna jambo lililochangia ambalo ni tofauti zake na Mbatia.

"Nafikiri hili linatokana na mikinzano ya tofauti za kimsimamo kati yangu na mwenyekiti," alisema Kafulila alipoulizwa iwapo tofauti zake na mwenyekiti wake ndizo zilizomlazimisha Ruhuza kuchukua hatua hiyo.

Kafulila alisema hana mpango wa kuchukua hatua yoyote dhidi ya uamuzi huo wa katibu mkuu "Nitauheshimu kwa kukaa pembeni ili kumruhusu atakayeteuliwa aanze kufanya kazi."

Kafulila hakutaka kuweka wazi tofauti hizo, lakini gazeti hili liliwahi kuripoti mara kadhaa mikinzano hiyo kuwa ni pamoja na mpango uliodaiwa kufanywa na Kafulila kutaka kumuengua Mbatia kwenye nafasi ya uenyekiti.

Tukio jingine ni lile la Mbatia kusema hadharani kuwa wabunge vijana (Kafulila ni miongoni) hawajui walichotumwa na wananchi kwenda kukifanya bungeni.
 
Tangu mwanzo Mbatia alionyesha kuwa hovyo kiasi cha kushindwa hata kuelezea sera za chama. She is a bad lady so to speak.
 
Vyama vyote vilivyofunga ndoa na CCM lazima vitakufa kama inavyokufa CCM. Gonjwa lile litawamaliza wote, si wanalala kitanda kimoja? Huko magamba EL na JK hapatoshi,huko Appolo Hospital mtu anateketea tartiib, haya wengine wamenuna kunyimwa nishani,wengine wanapinga ongezeko la posho makalio oh sorry za vikao mjengoni wakati wazee wa ndiyooooo wanataka ziongezwe mpaka kilo tano.RAHA TUPU MAJUHA WANAVYO UMBUANA. Natamani 2015 iwe kesho.
 
mbatia ni mfano wa mtu asie penda challenges..kafulila wakimtoa nccr ataenda chadema ..wanaweza wakampokonya kadi akahamia chadema na wananchi wa kigoma kusini ndio wenye final say na wanaweza waka waumbua MBATIA na genge lake la kihuni

Inawezekana pia Kafulila ana matatizo kwani akiwa chadema uliwahi kutokea mfarakano.
 
Taarifa zilizonifikia Punde ni Kwamba , Jemus Mbatia wa NCCR amemunyang'anya David Kafulila Cheo Cha Ukatibu Wenezi kama Mandalizi ya kumunyang'anya kati na Kukosa Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini mapema February Mwakani. Taarifa kutoka kwa Katibu mkuu Ruhuza inasema ,Barua ya tukio hilo imekabidhiwa kwa mhusika leo mapema!!!

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na Mbatia zinaonyesha kuwa tayari mpango umesha sukwa na CCM kwamba jimbo hilo lirudi mikononi Mwa CCM wakati Mbatia Mwenyewe anajiandaa kupewa ubunge kupitia Afrika Mashariki.

Mpango wa Mbatia unalenga kumuondoa David Kafulila katika Ujumbe wa Halmashauli Kuu ambayo itaketi February Mwakani ambapo tayari Wajumbe hao walisha mpa Mbatia Siku 21 kujieleza juu ya tuhuma za Kibaraka wa CCM.

Kutokana na kafulila Kunyang'anywa Kadi hana sifa ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mbatia na Kwamba mpango wa kumunyang'anya kadi Kafulila utatekelezwa badala ya kumuondoa Mbatia.

Wajumbe Wengi wa Halmashauli Kuu ambao wengi ni wa kuteuliwa na Mbatia wamesha pitiwa na Mulungula wa CCM kumumaliza Kafulila!!!
Mgogoro wa Ubunge Afrika Mashariki Bado unafukuta Ndani ya NCCR ambapo Msaidizi wa Mwenyekiti Danda JUJU naye anautafuta kwa nguvu kiasi cha Kutofautiana na Jemus Mbatia.

Kutokana na Mkakati huu Hali ndani ya NCCR ni tete sambamba na Hali ya CUF ambapo tatizo kubwa ni kuunga mkono CCM

Mwezi uliopita Seif aliitisha kikao Pemba kwenye jimbo la Hamadi Rashid na kuandaa Njama za Kumunyang'anya Kadi Hamadi Rashid lakini njama hizo zikafichuliwa na Blueguard wanao muuunga mkono Hamadi rashid

Bifu hilo limesababisha Seif kutoka Pemba na sasa yupo Lindi kufanya kampeni za Kumuchafua Hamad Rashid huku akipiga Marufuku vikao vyote vya CUF ngazi zote isipokuwa kwa Kibali chake!!
Seif kaandika barua ambayo imesainiwa na Mketo na mabox ya barua hizo yapo makao CUF yanasubiri kwenda mikoani.

Barua hiyo inawataka viongozi wote wa CUF nchi nzima wasifanye mikutano bila kibali cha Seif.

Waraka huo ndio ulimufanya Julias Mtatilo jana kuzuia Ziara ya Hamad Rashid tawi la Kosovo Manzese .

Hata hivyo Leo saa Kumi Hamadi rashid anafungua tawi la CUF kata ya Mabibo -eneo la CHECHINIA sijui kama watapona maana Blugad wameaagizwa kwenda hapo!!!

Hivi ndivyo vyama vinavyopigania Demokrasia nchini Tanzania lakini maneno na kauli zao zinaonyesha ndani ya vyama kuna Ufalme tena kama wa Mswati wa Swaziland siyo Malkia wa Uingereza! Yaani mtu anaamka tu na kumnyang'anya mwenzake madaraka? Hivi hakuna utaratibu wowote wa kunyang'anyana madaraka? Hivi Kafulila alipewaje hayo madaraka? Hakuna utaratibu wa kupeana madaraka ni mtu mmoja anaamua kukupa na kukunyang'anya (one individual has the power of hiring and firing)!!

Yaani mtu hawezi kufanya mkutano hadi mtu Mmoja atoe ruhusa?

Kweli Demokrasia kazi ninyi acheni demokrasia iitwe Demokrasia.
 
Back
Top Bottom