James Mbatia: NBC kuniita mimi ni mbumbumbu kulitikisa ndoa yangu

Namkumbuka Baba wa taifa mwalimu Nyerere alishawahi kusema wakati ule wa utawala wa mzee wa ruksa, kua kiongozi fulani anaamka tu asubuhi kashauriwa na mke wake halafu nayeye anakurupuka nakusema hivi na vile! Haya ndio ya James Mbatia mke wake kamshauri nenda kadai fidia kiasi fulani! Eti mke wake alimuona hafai!
 
Huyu naye asituzingue kama ndoa yake imetetereka sababu inaeleweka ni tabia yake ya ajabu ajabu.
 
Hivi Mbatia hakubali kuwa yeye ni mbumbu?yeye ndio alikuwa kijana wa kwanza kuwa M/kiti wa Taifa wa chama cha siasa nchini na bado alishindwa kuhamasisha vijana kuingia katika siasa wala kujiunga na chama chake, Mbatia ni mbumbu kwa kuwa aliweka pingamizi kwa CUF uchaguzi mdogo Pemba na kuruhusu CCM kushinda kirahisi hivyo alikwamisha harakati za kukifanya CCM chama cha upinzani, Mbatia ni mbumbu kwa kuwa ndio M/Kiti pekee wa taifa Upinzani aliyegombea jimbo na kushindwa, Mbatia ni mbumbu kwa kuwa chama chake mara nyingi kina pambana na vyama vingine vya upinzani haswa CDM badala ya CCM hivyo anapunguza nguvu ya upinzani

Kwa sasa naishia hapo tu
 
Back
Top Bottom