James Mbatia: NBC kuniita mimi ni mbumbumbu kulitikisa ndoa yangu

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Na Hellen Mwango

Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi James Mbatia

Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi James Mbatia ambaye anaishtaki Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amedai mahakamani kwamba kitendo cha benki hiyo kumuita mbumbumbu kilisababisha mtikisiko kwenye ndoa yake.
Kadhalika, amedai kuwa baada ya kuitwa mbumbumbu, mke wake alimuona hafai hivyo ndoa yake ikaingia kwenye mgogoro mkubwa na kumuathiri kisaikolojia.
Mbatia alitoa madai hayo jana mbele ya Jaji Imani Aboud, anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Alidai kuwa kashfa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kibenki wa benki hiyo, Joan Schrouder, dhidi yake zilisabisha ndoa yake kuingia matatizoni.

Katika kesi hiyo ya madai namba 236/2003, Mbatia anaidai fidia benki ya NBC ya Shilingi bilioni tano kwa madai ya kudhalilishwa na benki hiyo kwa kumuita mbumbumbu asiyejua masuala ya kibenki.
Mbatia aliwasilisha mchanganuo wa mapato yake ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji Aboud, kufuatiaombi la Wakili NBC Dk. Wilbard Kapinga, anayesaidiana na wakili Alexander Mzikila.
Wakili Dk. Kapinga aliiomba mahakama imwamuru Mbatia awasilishe mchanganuo wa mapato yake hayo tangu akiwa mbunge ili kujiridhisha kiwango cha fidia anayoidai.

Katika mchanganuo huo, wakati akihojiwa na Wakili Dk. Kapinga, Mbatia alidai kuwa wakati akiwa mbunge alikuwa akilipwa mshahara wa Sh. 800,000 kwa mwezi na kwamba alikuwa akilipwa posho ya kujikimu Sh.40,000 huku posho ya vikao ikiwa Sh. 20,000.
Aliongeza kuwa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano alilipwa Sh. milioni 13.5, na kwamba mbali na ubunge, lakini pia alikuwa anaendesha shughuli za kilimo mpaka sasa ambazo kwa wastani kwa mwaka anapata zaidi ya Sh. milioni 57.
Alipoulizwa na wakili Kapinga kuwa kashfa hiyo ilimuathiri vipi akiwa mume wa mke mmoja na pia baba wa watoto, Mbatia alijibu kuwa zilisababisha mke wake kusononeka, jambo ambalo lilisababisha ndoa yao kukosa furaha kwa muda.
Pia Mbatia alidai kuwa kashfa hiyo ilimvunjia heshima si katika familia tu bali pia ndani ya chama anachokiongoza na katika jamii kwa ujumla.
“Nilikutana na watu wa hadhi mbalimbali akiwemo Jaji Mark Bomani, mtu mmoja Solomon Lufunda, na wengine wengi ambao walinihoji kuhusiana na kashfa hiyo,” alisema Mbatia akijibu swali la Wakili Dk. Kapinga kuwa ana ushahidi gani kuwa kashfa hiyo ilizua taharuki katika jamii.

Pia Mbatia alidai kuwa kashfa hiyo ilimvunjia heshima hadi nje ya nchi akidai kuwa chama anachokiongoza kina vyama rafiki njena kwamba walipokuwa wakikutana na viongozi au wawakilishi wa vyama hivyo walikuwa wakimuuliza juu ya kashfa hiyo.
“Mwaka 2004 tuliondolewa katika umoja wa vyama vyenye uwakilishi Bungeni na kashfa hiyo ilikuwa ni moja ya mambo yaliyochangia kuondolewa kwetu,” alidai Mbatia.
Alipoulizwa ni kwa nini adai fidia ya Shilingi bilioni tano na si pungufu au zaidi ya hapo, Mbatia alijibu kuwa aliamua kudai fidia ya kiasi hicho kulingana na nafasi yake.
Hata hivyo, alidai kuwa heshima yake haiwezi kulinganishwa na kiwango hicho cha fedha bali anadai hicho kama kifuta jasho tukwa kuvunjiwa heshima yake.
Katika hatua nyingine, kesi hiyo ilikwama kuendelea baada ya mawakili wa upande wa utetezi kupinga kupokelewa kwa taarifa iliyodaiwa kutolewa na Schrouder kwa waandishi wa habari ambayo ndio msingi wa madai ya Mbatia.

Upande wa madai ukiongozwa na Dk. Sengondo Mvungi, akisaidiana na Wakili Mohamed Tibanyendela, uliiomba mahakama hiyo iipokee taarifa hiyo wakati shahidi wa pili wa upande wa mashtaka, Mwandishi Nelson Goima, akitoa ushahidi.
Akiongozwa na Dk. Mvungi, kutoa ushahidi wake, Goima ambaye alikuwa akimtetea Mbatia, alidai kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na Mkurugenzi huyo wa NBC.
Alidai kuwa wakati huo alikuwa ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la NIPASHE na kwamba siku hiyo Septemba 17, 2003, Mkurugenzi huyo wa NBC, aliwaeleza kuwa lengo la mkutano huo ni kuweka sawa juu ya kauli ya Mbatia.
Baada ya upande wa mashtaka kuomba shahidi huyo aiwasilishe mahakamani ili aisome taarifa hiyo iliyotolewa kwa waandishi wa habari, Wakili Kapinga na Mzikila waliipinga wakidai kuwa haionyeshi kuwa imetolewa na nani na inaelekezwa kwa nani.
Pingamizi hilo lilizua mvutano mkubwa ambao haukufikia mwafaka na hivyo Jaji Aboud, kuahirisha kesi hiyo hadi leo.
Katika madai yake, Mbatia anadai benki hiyo ilimtukana hivyo baada ya kuanika kile alichodai ufisadi katika uuzwaji wake kwa Kampuni ya ABSA kutoka Afrika Kusini mwaka 2000.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa mfululizo leo na kesho ambapo shahidi wa pili wa upande wa mdai, Goima atatoa ushahidi wake.
CHANZO: NIPASHE
 
All the best Mbatia. Ila unatakiwa uwe na counselor wako wakuku guide na kukufanya uone makombora ya kisiasa ni ya kawaida
 
Pamoja na madai na ulalamishi wote huo, bado Mbatia amepoteza hadhi yake katika jamii kutokana na ukigeugeu wake. Haeleweki hasa anasimamia nini katika siasa zinazoendelea sasa hivi nchini !
 
Mke wako hawezi kusikiliza watu wengine kuhusu umbumbumbu wako Mbatia..

Anyway kumbe ni dili la kupata fedha za mahakama
 
Pamoja na madai na ulalamishi wote huo, bado Mbatia amepoteza hadhi yake katika jamii kutokana na ukigeugeu wake. Haeleweki hasa anasimamia nini katika siasa zinazoendelea sasa hivi nchini !

Vyovyote vile lakini nampongeza sana kwa kuiona hii opportunity na kuitumia, Watanzania wengi sana uwa wanapoteza fursa kama hizi na kubakia tu kulialia njaa, opportunity kama hizi zinajitokeza kila siku katika maisha yetu ya kawaida, go Mbatia go...
 
Pooooor mbatia! Haya sasa kanishtaki na mimin nimekuita masikiini

Ebu acheni mawazo ya kizamani, kudai fidia sio umaskini na wala sio ujinga bali ni ishara ya akili iliyokomaa na inayochemka vizuri, hapa Mbatia anazifukuzia Billion 5 kirahisi kabisa...
 
ebu acheni mawazo ya kizamani, kudai fidia sio umaskini na wala sio ujinga bali ni ishara ya akili iliyokomaa na inayochemka vizuri, hapa mbatia anazifukuzia billion 5 kirahisi kabisa...
usiwe mpuuzi wewe, nilikuwa nakurespect sana ila umeongea pumba hapa. We vipi, unamjua mbatia au unamsikia tu?
 
safi sana anautumia umbumbu wake kujijengea heshima na kuwakomesha wasema hovyo hao wageni wa NBC ila anaweza kupeta ? Wacha tuone .Je ana ushahidi wa madai ya ndoa yake kuwa mashakani anaweza kuutoa mahakamani ?Maana inabidi kuthibitisha hilo kwamba his marriage was in a danger zone kwa mtamshi hayo .
 
Mr drama king! So full of himself! Wakati wa uchaguzi alitaka kufungua kesi kwa chadema kwa kumkashifu pia,hivi iliishia wapi?
 
​msimuhukumu mbatia kwa yaliyopita muhukumuni kwa jambo linaloendelea sasa....hongera mbatia kwa kutumia mahakama kwani watanzania wengi wananyanyaswa lakini wanaogopa kwenda mahakamani
 
hapa ishu si kupoteza hadhi ya kisiasa. Hii kesi ya 2003 inakuja kuanza leo? Hapo utaona kuwa jamaa kachacha na anatafuta mtaji tu
 
safi sana anautumia umbumbu wake kujijengea heshima na kuwakomesha wasema hovyo hao wageni wa NBC ila anaweza kupeta ? Wacha tuone .Je ana ushahidi wa madai ya ndoa yake kuwa mashakani anaweza kuutoa mahakamani ?Maana inabidi kuthibitisha hilo kwamba his marriage was in a danger zone kwa mtamshi hayo .

duh. umesema jambo, beyond reasonable doubt
 
duh. Umesema jambo, beyond reasonable doubt

hii ni kesi ya madai anabidi athibitishie mahakama on balance of probability.ingekuwa ni criminal case ndio wangeitaji aprove beyond reasonable dòubt!
 
Pooooor mbatia! Haya sasa kanishtaki na mimin nimekuita masikiini

hivi kama mtu hujui kusoma na nikaprove hujui kusoma kumbe natakiwa nikulipe bn 5.hapo nbc waprove umbumbumbu wake and this stupid case is closed,.ccm wamemtoa kwenye payroll yao huyo
 
Mbona anafungua kesi za madai kila leo....
Na mahesabu yake Bilioni tanotano... ipi ameisha-pull thru?
 
Back
Top Bottom