James Mbatia: Mimi sio Kibaraka wa CCM, nadai Bilioni moja kutoka kwa Mengi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

James Mbatia: Mimi sio Kibaraka wa CCM, nadai Bilioni moja kutoka kwa Mengi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwamakula, Dec 3, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bw Jemus Mbatia ameandika demand note Kwa gazeti la NIPASHE kutaka Reginald Mengi amlipe 1bils kutkana na gazeti lake kuandika habari za Kikao Cha NEC NCCR, ambacho Wajumbe walimutuhumu Jemus Mbatia kuwa ni Kibaraka wa CCM hivyo kumutaka ajieleze kwa kumupa siku 21.

  Baada ya Tamko la NEC na muda aliopewa kuisha, Wajumbe wa Mikoa ya KIGOMA, MBEYA, ZANZIBAR wameunga mkono Mbatia kuondolewa kutokana na kukosa mvuto wa kisiasa na kutoa msimamo wa kuunga mkono CCM!

  Jambo la Kushangaza, James Mbatia hawashitaki Wajumbe wa NEC, wala Wanyeviti katika Mikoa ambao licha ya kuongea na vyombo vya habari, wameandika Waraka na kusaini Wakielezea kuwa Mbatia ni Kibaraka wa CCM(CCM-C)

  Kesi ya kipuuzi kama hiyo, Mbatia amefungua kesi ya kupinga Matokeo ya uchaguzi Jimbo la Kawe ambapo yeye Mbatia alishindwa na Wanawake Wawili na yeye kuwa wa tatu.

  Hata kama NEC watatengua matokeo hayo bado hawezi kushinda!

  Kesi hiyo Mbatia alifungua muda mfupi baada ya aliyekuwa katibu Mkuu CCM BW Yusufu Makamba kuandika waraka kuwataka wabunge wote wa CCM walioshindwa katika uchaguzi 2010 kufungua kesi kupinga matokeo hayo na CCM imekuwa ikifadhili kesi hizo.

  Hata hivyo Yusufu Makamba amejivua Gamba muda mfupi baada ya kuimarisha kambi ya upinzani na alitoa Wosia wa kwenda kuwandalia Makao waliobaki!
   
 2. k

  kabindi JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  la kuvunda halina ubani! Hakuna asiyejua kwamba ni kibaraka! tabia yake tayari ilishamuumbua!
   
 3. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mbatia ni mchumia tumbo, ndo maana mahitimisho yake yote katika kesi anazofungua huwa ni kudai fidia ya mamilioni ya fedha. Kwa mengi ameula wa chuya, hapati hata senti kumi.
   
 4. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]MBATIA: KAMPENI ZA KASHFA HAZINA TIJA KWA UMMA.[/h] 14th September 2010


  Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia
  Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ametoa rai kwa wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa kushindana kwa hoja za kimaendeleo badala ya kashfa zisizokuwa na tija kwa umma.
  Mbatia anayewania ubunge wa jimbo la Kawe, alitoa rai hiyo juzi katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.
  Alikuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za NCCR-Mageuzi, uliohudhuriwa pia na mgombea urais kupitia chama hicho, Hashim Rungwe na mgombea mwenza wake, Ally Omary.
  Mbatia alisema wagombea hao wanapaswa kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu kila wanapokuwa jukwaani, ili hekima, umoja na amani vitumike badala ya kauli zinazoweza kuchochea chuki.
  Mbatia aliwataka wapiga kura kuwa na hekima ya kuchagua viongozi bora na si kuangalia vyama wanavyotoka.
  Mbatia alitaja vipaumbele vya ilani ya chama hicho, vikigusia utawala bora, sekta ya uchumi, huduma za kijamii, makundi ya watu maalumu, vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na usawa wa jinsia.
  Alisema ikiwa NCCR itashinda katika uchaguzi huo, asilimia 30 ya bajeti ya nchi itaelekezwa katika uboreshaji wa elimu.
  Mbatia alizungumzia msongamano uliopo jijini hapa na kuahidi kutumia mbinu mbalimbali zitakazofanikisha kuondokana na kero hiyo.
  Alisema ikiwa NCCR itapata ushindi serikali itaanzisha usafiri imara wa majini na kujenga gati ufukweni wa bahari.
  Alisema usafiri huo utaanzia Bagamoyo-mbweni-Kunduchi-Mbezi beach-Msasani mpaka bandari ya Dar es Salaam.
  Pia alisema serikali ya NCCR itaanzisha usafiri wa reli ikiwa ni mojawapo wa njia za kukabiliana na msongamano jijini humo.
  Alisema usafiri wa reli utawalenga zaidi wakazi wa jijini kutoka Pugu-Gongolamboto-Vigunguti-Buguruni mpaka kituo kikuu cha kati.
  Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordani Rugimbana na Mkuu wa Idara ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa chama hicho, Dk Sengondo Mvungi.
   
 5. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  1st December 2011

  [​IMG]
  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia


  Shinikizo la kumtaka Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia, ajiuzulu wadhifa huo, limepamba moto, baada ya wenyeviti wa majimbo tisa ya Mkoa wa Kusini Pemba, kuungana na viongozi wengine wa chama hicho wa mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, kutaka ajiuzulu mara moja.
  Azimio la kumkataa Mbatia, lilipitishwa kwa kauli moja na wenyeviti hao katika kikao chao kilichofanyika mkoani humo jana.
  Wenyeviti hao, ambao majimbo wanayotoka kwenye mabano, ni Idrisa Hassan Shamte (Chambani); Maulid Yusufu Ali (Chakechake) na Haji Suleiman Hamad (Ziwani).
  Wengine ni Hamad Rashid Nassoro (Wawi); Juma Khamis Juma (Mkoani); Maulid Hamad Said (Kiwani) na Walid Khamis Mohamed (Mtambile).
  Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa huo, Yusufu Kapela Majoka, alisema jana kuwa hatua hiyo ilifikiwa na wenyeviti hao, wakiunga mkono msimamo wa wajumbe 28 wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama hicho Taifa wa kutokuwa na imani na Mbatia na hivyo, kutaka asimamishwe au ajiuzulu.Miongoni mwa wajumbe 28 wa NEC waliojitokeza hadharani na kutangaza msimamo wao wa kutokuwa na imani na Mbatia, ni pamoja na wabunge; David Kafulila (Kigoma Kusini) na Felix Mkosamali (Muhambwe).
  Wajumbe hao walitangaza msimamo huo katika mkutano wa NEC, uliofanyika Novemba 5, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, kwa madai kwamba, Mbatia kuwa ni wakala (pandikizi) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo amepoteza sifa ya kuwa kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
  Majoka alisema wenyeviti hao walitoa tamko hilo wakidai kwamba, uongozi wa Mbatia ni mbaya kutokana na kuwa kigeugeu, hali inayosababisha chama kuyumba.
  "Zaidi ya hivyo, uongozi wake umesababisha kuzaliwa makundi mawili katika chama. Hivyo, kikao kimependekeza ajiuzulu, apumzike kama anakipenda chama. Asisubiri vikao. Huwezi kuwa mpinzani, halafu ukatetee na kuunga mkono CCM?" alihoji Majoka.
  Juzi wenyeviti wa NCCR-Mageuzi katika wilaya zote za mkoani Mbeya, walitoa tamko wakitaka Mbatia ajiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kusababisha chama hicho kukosa maendeleo.
  Walitoa tamko hilo zikiwa zimepita wiki chache baada ya viongozi wa NCCR-Mageuzi mkoani Kigoma na wale wa mikoa mitatu ya kisiwani Unguja, kumtaka Mbatia ajiuzulu wadhifa wake kwa madai kwamba, hana dhamira ya kweli ya kukiongoza chama hicho ili kiweze kushika dola.  CHANZO: NIPASHE
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Haya ndio malipo ya usaliti. Kiongozi kijana lakini mpuuzi,atahangaika sana lakini hatafaulu
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Kumbe thamani ya Mbatia ni shilling Billion moja! hapa ndipo sasa ninapoziona busara za Yusuph Manji kumdai Mengi fidia ya shilling 1. Human dignity can not be valued bay money. Huyu ni political loser.
   
 8. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Anataka za mkorogo japo sura imeshaanza kumtupa mkono. Kweli fani hauzeeki
   
 9. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  mbatia kakosea kuwa nccr kwani lzm watammwaga, natmai angeamia chama cha cuf naona wanatabia zinazofanana nae, amekuwa akiipigania pia akijipendekeza sana ccm uku akiipinga CDM hadharani,natmai anatafuta nafasi ya kuolewa na magamba lakini tatizo anatokea upande wa nccr, nakushauri sana ndg mbatia jiunge cuf (CCM B) utafanikiwa iyo ajenda yako
   
 10. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Hiyo paragraph ya mwisho imenichanganya
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi mbali ya siasa, Mbatia ana shughuli gani nyingine ya kumwingizia kipato?
   
 12. February

  February Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu mbatia mnataka akale wapi? Sio kwamba hana akili lakini lazma ajiulize ataishije mjini. Unajua analipwa kiasi gani kutoa tamko la kusaidia ccm? Hapo alipo hauzi nyanya wala sio mtumishi popote lakini anaishi first class. Sasa kuna kazi nzuri kama hiyo? Unajua amelipwa sh ngapi na ccm kufungua kesi kawe?
   
 13. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du!
  Aisee sijui, Zaweza kuwa nyingi!
  Ufisadi una pande nyingi.
   
 14. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa zilizonifikia Punde zinaonyesha kuwa 80% ya Wajumbe Wa NCCR Mageuzi walioketi kikao Leo Mjini Dodoma (Jirani na Makao Makuu CCM) Wamepitisha Jemus Mbatia Ang'olewe Uenyekiti Taifa Kwa sababu ni Kibaraka Wa CCM.

  Taarifa zimebaini kuwa Jemus Mbatia alijaribu kumwaga pesa nyingi kwa wajumbe hao kupitia kwa Moses Machali (0713 102971) na kufanikiwa kwa 20% tu.

  Hata hivyo imebainika kuwa Wajumbe Walipokea pesa hizo zinazotajwa kutokea CCM lakini bado wakamulipua Mbatia.
  Baada ya Kikao hicho Mh Mose Machali ameshangaa sana Matokeo hayo baada ya kutumia fedha nyingi!!!

  Juzi Jemus Mbatia alimwaga pesa kama hizo Mkoa wa Mara ili luhujumu Mkutano ambao unatajwa ulivurugika baada ya Wajumbe kuwa wakali!!

  Pia Zipo Taarifa kuwa Jemusi Mbatia ameficha Hati ya Kiwanja Cha Makao Makuu kama maandalizi ya kuhujumu NCCR wakati Mgogoro unaendelea.

  Watu Wa karibu na Mbatia wanasema hataki Kuonyesha ilipo hati hiyo mpaka ajihakikishie Usalama wake!!!
   
 15. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=2]Mbatia apewa siku 21 kujieleza NCCR[/h]


  Na Muhibu Said
  6th November 2011
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia


  HalmashauriI Kuu(NEC) ya Chama cha NCCR-Mageuzi, imempa Mwenyekiti wake, James Mbatia, siku 21 kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na baadhi ya wanachama kwamba, ni pandikizi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndani ya chama hicho.
  Agizo hilo ni miongoni mwa maazimio kadhaa ya NEC yaliyofikiwa kwa kauli moja na idadi kubwa ya wajumbe wa halmashauri hiyo, katika kikao chake kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 50, lakini kinyume cha kawaida, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuhudhuria.
  Azimio hilo dhidi ya Mbatia lilisomwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Samuel Ruhuza katika kikao hicho na limezingatia kanuni za chama zinazotoa fursa kwa mwanachama mtuhumiwa kujitetea.
  Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinaeleza kuwa hoja kuhusu tuhuma hizo, iliwasilishwa katika kikao hicho na Mjumbe wa NEC kutoka Tanga, Mbwana Hassan.
  Hoja hiyo imesainiwa na wajumbe 28 wa halmashauri hiyo, ambao kwa kauli moja wanataka Mbatia ajiuzulu uenyekiti wa chama hicho kutokana na tuhuma zinazomkabili.
  Kwa mujibu wa habari hizo, kati ya wajumbe waliohudhuria kikao cha jana, ni wajumbe 10 tu ndio wanaodaiwa kumuunga mkono Mbatia kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho, huku wengine waliosalia wakiwa hawana upande.
  Kutokana na agizo hilo, Mbatia sasa anatakiwa kujibu tuhuma hizo na kuwasilisha majibu hayo kwa Katibu Mkuu. Katibu Mkuu baada ya kuyapokea, atawasilisha kwa Kamati ya Maadili ya Chama na kisha kupelekwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika Februari, mwakani kwa ajili ya maamuzi.
  Habari hizo zinasema kuwa baada ya azimio hilo kupitishwa na NEC, Mbatia aliomba kutendewa haki kwa kupewa muda wa kutosha kujibu tuhuma zinazomkabili.
  Imeelezwa kuwa awali, viongozi waliokuwa wamekaa meza kuu walijaribu kuzuia hoja inayohusu tuhuma dhidi ya Mbatia kujadiliwa katika kikao hicho. Hata hivyo, idadi kubwa ya wajumbe walipinga hatua hiyo na kushinikiza ijadiliwe.
  Mvutano kuhusu suala hilo uliendelea baada ya Mbatia kugoma kujibu tuhuma zinazomkabili.
  Jambo lingine lililotaka kulipua kikao hicho, ni madai kwamba, kulikuwa na mabaunsa waliokuwa wamekodiwa na baadhi ya wanachama kwa lengo la kutisha wajumbe na kuleta vurugu.
  Hali hiyo ilimfanya Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali, kutishia kuwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, ili alete askari kwa ajili ya kuwashughulikia mabaunsa hao.
  Mkosamali, ambaye ni mjumbe wa NEC, alifikia hatua hiyo baada ya baadhi ya wajumbe kutaka mabaunsa hao waondolewe, huku baadhi ya viongozi wakipinga suala hilo.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 16. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lafudhi uliotumia inaonesha wewe ni askofu msaidizi wa jimbo la kwa Kagame?
   
 17. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,913
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Kama hawamtaki anaona tatizo gani kujiweka pembeni kisha ajipange upya?
   
 18. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hivi Jemus Mbatia Hana Washauri???
   
 19. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Yusufu Mkamba mimi Binafsi nampenda sana Kwa Sababu amefanya kazi kubwa ya kubomoa CCM hadi kusababisha kujivua Gamba!!!
  Unakumbuka Wakati wa Kikao Cha kujivua Gamba yeye aliomba Udhuru Kwenda kwenye Msiba??

  Je Unaonaje sasa NEC wanaweza kumutoa LOWASSA????
   
 20. only83

  only83 JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180

  Piga chini huyo...tupate chama kingine chenye nguvu kwa ajili ya kuwashughulikia magamba....
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...