James Mbatia Kusimamishwa NCCR Mageuzi, Mrema anasemaje? Mbatia alihusika kumtoa Mrema NCCR, isije ikawa anavuna alichopanda!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Mtu unaweza kumfanyia jambo baya mwenzako halafu unasahau. Ukifika wakati wa kuvuna uovu uliopanda mtu hulalamika sana na kutafuta huruma kwa watu!! Lakini ni wazi kuwa Mbatia alishiriki kumng'oa Mrema pale NCCR Mageuzi akishirikiana na wenzake!! Alichokifanya kinamrudia. Namshauri aende kuomba radhi kwa Mrema kwanza.

Kumbukeni pia Sharif Hamad (marehemu) alishiriki kumtoa Mapalala (mwanzilishi wa CUF) pale CUF tena kwa kumdhalilisha mno. Yaliyomtokea Sharif Hamad pale CUF naye kujikuta ametolewa kwa hila na yule mnyamwezi wa Tabora (aliyetengua barua ya kujiuzulu) wote bado tunayakumbuka.

Wazungu husema "what goes around comes around). Mbatia asishangae yanayomkuta, ni mavuno halali ya upandaji wake katika siasa, kama ambavyo Sharif Hamad naye alivuna kwa stahili yake mapando aliyopanda katika sisa.

Ni onyo pia kwa chama kikongwe!! kitafakari kinavyopanda kwenye siasa.
 
Hamna kitu kama hcho, ni nadharia tu za watu wazembe na vilaza wa kufkri
Unakijua laklini alichokifanya Mbatia kwa Mrema wakiwa wote NCCR Mageuzi? na kile alichokifanya Seif Sharif Hamad kwa James Mapalala Mwanzilishi wa CUF!!
 
Back
Top Bottom